Matokeo ya wanafunzi bora, yaani kumi bora [ 10 ] - kuanzia darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita yameanza kutangazwa rasmi mwaka 2016, kipindi cha rais John Pombe Magufuli.
Kabla ya hapo, yaani tangu kuundwa kwa Baraza la mitihani [ NECTA ], mwaka 1964 hadi mwaka 2015. Matokeo ya wanafunzi bora kwa hatua zote yalikuwa hayatangazwi.
Hivyo basi, huyu mwanafunzi anayetambulika kwa jina la Elias Kihombo, anayejinadi kama mwanafunzi aliyeongoza kidato cha sita mwaka 2006 sio yeye na ni tapeli kama walivyo matapeli wengine.
Ili kuondoa sintofahamu na kuzuia watu wa aina hii kwenye jamii na hata kutambua wale wanafunzi bora walioongoza kihalali tangu mwaka 1964 hadi mwaka 2015 kupewa haki zao kama wasifu wa kitaaluma.
Kama ilivyofanyika kwa mwaka wa 2016, 2017, 2018 na 2019 chini ya mamlaka ya rais yaani "Presidential Decree Order" au maarufu kama "OPD" tungeomba ifanyike vivyo hivyo kwa matokeo ya wanafunzi bora kwa miaka iliyopita, yaani kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 2015.
Hii itasaidia kuondoa makandokando yaliyokuwepo na yanayoendelea kuwepo kwenye baraza la mitihani [ NECTA ]. Kwani matokeo ya shule katika hatua zote - yaani darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita yamekuwa yakikumbwa na udanganyifu na ulaghai wa kutisha!
Ukanda! Ukabila! Udini! Na hata rushwa zimekuwa ni nyenzo katika upangaji wa matokeo ya wanafunzi kwa hatua zote za elimu.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kipindi cha mwaka wa 2005 hadi mwaka 2015, ambapo elimu ya Tanzania ilikuwa ni kama soko huria "Tanzania Education System was a form of a modernised market - the more you pay, the higher you score". Yaani anayelipa pesa nyingi ndiye anayepata matokeo mazuri bila ya kujali uwezo wa mwanafunzi husika.
Kwahiyo kutangaza matokeo ya wanafunzi bora kwa miaka ya nyuma itasaidia sana wahitimu waliopita kufahamu wasifu wao wa kitaaluma.