Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,324
..winter haizoeleki hata ukae miaka mingapi huko ulaya.
..kwa umri wake Sultani anatakiwa apumzike mahali penye hali ya hewa ambayo ni rafiki kwa watu wa makamo yake.
..Jamshid kuendelea kuteseka na winter ukimbizini Portsmouth, wakati anaweza kurudi kwao Zanzibar, ni mfano dhahiri wa mtu anayetema asali na kufakamia pilipili.
..SULTANI asiendelee kukataa kwao, na kuwa sawa na MTUMWA.
Nimekuuliza umewahi kumuona mtu anatema asali na kutamani pilipili naona unajikanyaga tu. Labda nikupe kilicho chepesi kwako JE UMEWAHI KUMUONA MTU ANATOROKA PEPONI NA KUKIMBILIA MOTONI?
Je mtu huyo atakuwa taamam kiakili?