Mfalme Daudi alioa binti ambae bado hajavunja ungo (-12), kwanini hili halipigiwi kelele kama ilivyo kwa upande wa Mohammed?

Mfalme Daudi alioa binti ambae bado hajavunja ungo (-12), kwanini hili halipigiwi kelele kama ilivyo kwa upande wa Mohammed?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Bwana Yesu asifiwe wakuu, wasalaam waleikum

Uzi huu kwa namna yoyote sihamashi ndoa za mabinti wadogo bali ni kuwekana sawa tu kwamba katika zama za kale tamaduni hazikuruhusu tu upande wa Mohammed kwa kiasi kikubwa waarabu kuoa mabinti wadogo bali ni hata kwa waisrael na mababu zetu wa hapa Afrika, hivyo ninatoa elimu kuweka mambo sawa.

Kumekuwa na hali iliyozoeleka baadhi ya wakristo wakihoji ni vipi Muhammad alioa msichana mdogo ila kwa upande wao wanasahau kujihoji ni vipi watu kama Mfalme Daudi akiwa na miaka 90 alioa msichana mdogo wa rakribani miaka 9 hadi 10.

Katika biblia tafsiri za lugha zingine zimetambua tu kwamba mfalme daudi alioa binti mdogo pasipo kuweka wazi ni rika lipi na sijui kwanini hawakuweza kuweka hata kwenye mabano.

Mfalme Daudi, wakati alipokuwa mzee sana takribani miaka 90, watumishi wake walimfunika kwa mablanketi, lakini hata hivyo, hakuweza kupata joto. Kwa hivyo wakamwambia, “Bwana wetu mfalme, afadhali tukutafutie msichana akutumikie na kukutunza; alale pamoja nawe kusudi akupatie joto.”

Daudi muda huo alikuwa tayari mzee sana takribani miaka 90, akaoa binti wa miaka takribani 9 ama 10, kwa uzee alionao Daudi kwa miaka hio ilikuwa ngumu kufanya tendo na binti lakini binti aliweza kulala nae kitanda kimoja kwajili ya kumpa joto pekee pasipo kufanya s*x.

Mabinti wenye miaka chini ya 12 walijulikana kama NA’ARAH ( נַעֲרָה ) - hawa ni mabinti ambao waliweza kuolewa na wafalme ama viongozi wa dini wa hadhi ya juu (high priests) katika falme ya israel, ikumbukwe kwa wakati huo tamaduni za Israel ilikuwa kwamba binti akishafika miaka 12 na kuaga rika la NA’ARAH hapo ilikuwa ndio umri wa kuolewa, sijajua ilikuwa vipi mabinti wadogo wa miaka 13 hadi 15 wanaolewa na hata Mariam kuwekwa mimba kimiujiza akiwa bado binti mdogo (toho inanisita kuamini) lakini kwa dunia ya sasa huo umri hatuwezi kukuelewa,

Maandiko yenye mfano wa hao mabinti chini ya miaka 12 kuolewa mfano wake ni huu hapa 1 wafalme 1: 2-3. kwa lugha zingine wametafsiri ni binti mdogo na wengi kwa mazingira ya kisasa tunaweza vuta picha ni binti wa miaka 19 lakini neno lililotumika katika maandiko ya ki israel yameonesha wazi kabisa binti alieolewa ni chini ya miaka 12 a.k.a NA’ARAH ( נַעֲרָה )

1679755907954-png.2565239
 
kwa nilichoona hadi sasa ni mambo mengi sana waisrael na waarabu walifanana kwenye tamaduni isipokuwa tu kwavile ukristo ulikulia zaidi ulaya, wazungu wakagoma kuingiza vitabu vyenye tamaduni za ki israel kwenye biblia maana tamaduni za israel zilikuwa tofauti na zao, tamaduni za israel ziliruhusu kuoa zaidi ya mke moja, utaratibu wa urithi, mazishi ni tofauti na tamaduni za ulaya, mambo ya ndoa yamerahisishwa, n.k.
 
MFALME DAUDI HAKUFANYA NGONO NA BINTI HUYO
1 Wafalme 1:1-4
[1]Mfalme Daudi alikuwa mzee, mkongwe katika siku zake, nao wakamfunika nguo, lakini asipate moto.
Now king David was old and stricken in years; and they covered him with clothes, but he gat no heat.

[2]Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, Bwana wangu mfalme na atafutiwe kijana mwanamwali; naye asimame mbele ya mfalme, amtunze; alale kifuani mwako, ili bwana wangu mfalme apate moto.
Wherefore his servants said unto him, Let there be sought for my lord the king a young virgin: and let her stand before the king, and let her cherish him, and let her lie in thy bosom, that my lord the king may get heat.

[3]Basi wakatafuta kijana mzuri mipakani mwote mwa Israeli, wakamwona Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme.

So they sought for a fair damsel throughout all the coasts of Israel, and found Abishag a Shunammite, and brought her to the king.

[4]Naye kijana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; walakini mfalme hakumjua.
And the damsel was very fair, and cherished the king, and ministered to him: but the king knew her not.
 
Hakuoa, bali alikuwa ni binti wa kumpa joto kwa tamaduni za kiyahudi kwa wakati huo. Pia hakuwahi kulala naye kimapenzi.
 
When King David (reigned c. 1005–965 BCE) ages and his health fails, a beautiful young woman is sought throughout Israel to lie in his bosom and keep him warm. The king does not have sexual relations with Abishag (I Kgs 1:4).
 
Habari zenu, Bwana Yesu asifiwe.

Mimi ni mkristo lakini linapokuja suala la ukweli huwa napenda kuujua kama ulivyo bila kuweka hisia zangu kuziba ziba kitu nachoona kibaaitia dosari ikiwa kipo upande wangu au kukandia zaidi kitu ambacho naona kinatia dosari ikiwa kipo upande mwengine

Huwa nashangaa sana napoona upande moja unalaani wengine bila wao kujichunguza vizuri na kutambua kwamba mzani wa hayo malalamiko ume balance pande zote.

Katika biblia tafsiri za lugha zingine zimetambua tu kwamba mfalme daudi alioa binti mdogo pasipo kuweka wazi ni rika lipi na sijui kwanini hawakuweza kuweka hata kwenye mabano.

Mfalme Daudi, wakati alipokuwa mzee sana takribani miaka 80, watumishi wake walimfunika kwa mablanketi, lakini hata hivyo, hakuweza kupata joto. 2Kwa hivyo wakamwambia, “Bwana wetu mfalme, afadhali tukutafutie msichana akutumikie na kukutunza; alale pamoja nawe kusudi akupatie joto.”
Katika tafsiri ya maandiko kwenye lugha fasaha iliyotumika ni kwamba huyo binti alikuwa wa miaka chini ya 12, yawezekana alikuwa na miaka 10 tu.

Mabinti wenye miaka chini ya 12 walijulikana kama NA’ARAH ( נַעֲרָה ) - hawa ni mabinti ambao waliweza kuolewa na wafalme ama viongozi wa dini wa hadhi ya juu (high priests) katika falme ya israel, ikumbukwe kwa wakati huo tamaduni za Israel ilikuwa kwamba binti akishafika miaka 12 na kuaga rika la NA’ARAH hapo ilikuwa ndio umri wa kuolewa, sijajua ilikuwa vipi mabinti wadogo wa miaka 12 hadi 13 wanaolewa lakini kwa dunia ya sasa ni kosa kubwa sana,

Maandiko yenye mfano wa hao mabinti chini ya miaka 12 kuolewa mfano wake ni huu hapa 1 wafalme 1: 2-3. kwa lugha zingine wametafsiri ni binti mdogo na wengi kwa mazingira ya kisasa tunaweza vuta picha ni binti wa miaka 19 lakini neno lililotumika katika maandiko ya ki israel yameonesha wazi kabisa binti alieolewa ni chini ya miaka 12 a.k.a NA’ARAH ( נַעֲרָה )

1679755907954-png.2565239
Pamoja na kwamba unajinasibisha na ukristo, lakini swali ulouliza ni “ambiguity” kwenye muktadha wa imani hizo mbili.

Kama wewe ni mkristo, unamfananishaje Mfalme Daudi na Mtume Muhammad wa waislam? Tafadhali jaribu kufananisha apple 🍎 kwa apple 🍎.

Wewe ni muislam na umeshajuwa udhaifu wako ulipo ndiyo maana umejidai kuwa wewe ni mkristo. Shame on you!
 
Daudi hakufanya ngono na Binti huyo.
When King David (reigned c. 1005–965 BCE) ages and his health fails, a beautiful young woman is sought throughout Israel to lie in his bosom and keep him warm. The king does not have sexual relations with Abishag (I Kgs 1:4).
Ishu ni kwamba tamaduni za Isreal ziliruhusu wafalme na viongozi wa juu wa dini kuoa mabinti ambao bado hawajabalehe, kuhusu kulala nao ama kutolala nao yalikuwa ni maamuzi binafsi,

Pia ikumbukwe hapo Daudi alikuwa mzee sana yapata miaka 90 anaoa binti wa miaka kama 10 ama 9, kitendo cha kumuoa ni tiketi ya kuweza kufanya tendo la ndoa ila kwavile pengine alikuwa mzee sana hakuweza hata kuperform.
 
Ni kweli kuwa katika Biblia, tafsiri za lugha zingine zinatofautiana kuhusu umri wa binti ambaye Mfalme Daudi alimwoa. Hata hivyo, katika tafsiri ya kisasa ya Biblia ya Kiswahili, hakuna tafsiri inayotoa maana ya kwamba alikuwa mtoto mchanga au mwenye umri mdogo sana.

Ingawa tamaduni za zamani zilikuwa tofauti na za sasa, ni muhimu kutambua kuwa kuolewa kwa wasichana walio na umri mdogo ni kinyume cha sheria na maadili ya jamii nyingi za leo. Ni vyema kutafsiri maandiko kwa kuzingatia maadili na kanuni za jamii ya sasa.

Kwa hivyo, badala ya kutumia maandiko kama kisingizio cha vitendo ambavyo havikubaliki kimaadili, ni muhimu kuzingatia kanuni za maadili na sheria za nchi husika.
 
Hili nalo tatizo jingine.Kwahiyo unajaribu kusema kwamba watu wa zama hizi waanze kumkosoa mfalme Daudi ambaye hayupo sasa au ?sijaelewa!("Huwa nashangaa sana napoona upande moja unalaani wengine bila wao kujichunguza vizuri")

Maisha ya Daudi na miongozo ya ukristo kuna uhusiano upi sasa?.Daudi alikuwa mtu kama wewe hakuwahi kutoa maelekezo yoyote kuhusu maisha ya mwanadamu, isipokuwa tu ujumbe ambao alitamka kwa kinywa chake ambao ulitoka kwa Mungu ndio unajumuishwa katika miongozo ya ukristo.Ukristo haungozwi na misingi ya maisha ya mtu fulani aliyetajwa kwenye biblia.Ukristo ni ujumbe wa mwenyezi Mungu kwa wanadamu aliotoa kupitia watumishi wake(David among of them) na sio maisha yao.Sasa unataka wakristo waseme nini kuhusu maisha ya mfalme Daudi?

Kasome vitabu vya Nyambari kwanza ndugu hivi vya dini vigumu.
 
Ngoja kina aposto wamalize kupakana mafuta, watakuja sasa hivi.
 
Aseee kumbe
Tamaduni za zamani kwa sehemu kubwa zilifanana kwenye mambo ya kuoza mabinti wadogo, kuwacheka waislam kwamba Muhammad alioa binti mdogo ni kigezo tosha kujua mtu hajui utamaduni wa waisreal hata kwao wafalme na viongozi wa juu wa dini walioa wasichana wadogo,

Mariam mama yake Yesu labda alikuwa na nafuu huenda alizaa akiwa na miaka 14 ama 15, na hapa ni Mungu aliweza kuiweka mimba kimiujiza ndani ya tumbo la Mariam, Yusufu aliekuwa kashamuoa Mariam huku ndoa ikiwa na mda mchache bila kumuingilia alidhani Mariam kamsaliti ila alipooteshwa ndoto akaelewa.
 
MFALME DAUDI HAKUFANYA NGONO NA BINTI HUYO
1 Wafalme 1:1-4
[1]Mfalme Daudi alikuwa mzee, mkongwe katika siku zake, nao wakamfunika nguo, lakini asipate moto.
Now king David was old and stricken in years; and they covered him with clothes, but he gat no heat.

[2]Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, Bwana wangu mfalme na atafutiwe kijana mwanamwali; naye asimame mbele ya mfalme, amtunze; alale kifuani mwako, ili bwana wangu mfalme apate moto.
Wherefore his servants said unto him, Let there be sought for my lord the king a young virgin: and let her stand before the king, and let her cherish him, and let her lie in thy bosom, that my lord the king may get heat.

[3]Basi wakatafuta kijana mzuri mipakani mwote mwa Israeli, wakamwona Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme.

So they sought for a fair damsel throughout all the coasts of Israel, and found Abishag a Shunammite, and brought her to the king.

[4]Naye kijana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; walakini mfalme hakumjua.
And the damsel was very fair, and cherished the king, and ministered to him: but the king knew her not.
Mada ifungwe
 
Uzi huu kwa namna yoyote sihamashi ndoa za mabinti wadogo bali ni kuwekana sawa tu kwamba katika zama za kale tamaduni hazikuruhusu tu upande wa Mohammed kuoa mabinti wadogo bali ni hata kwa waisrael na mababu zetu, hivyo ninatoa elimu.

Kumekuwa na hali iliyozoeleka baadhi ya wakristo wakihoji ni vipi Muhammad alioa msichana mdogo ila kwa upande wao wanasahau kujihoji ni vipi waru kama Mfalme Daudi akiwa na miaka 90 alioa msichana mdogo wa rakribani miaka 9 hadi 10.

Katika biblia tafsiri za lugha zingine zimetambua tu kwamba mfalme daudi alioa binti mdogo pasipo kuweka wazi ni rika lipi na sijui kwanini hawakuweza kuweka hata kwenye mabano.

Mfalme Daudi, wakati alipokuwa mzee sana takribani miaka 90, watumishi wake walimfunika kwa mablanketi, lakini hata hivyo, hakuweza kupata joto. Kwa hivyo wakamwambia, “Bwana wetu mfalme, afadhali tukutafutie msichana akutumikie na kukutunza; alale pamoja nawe kusudi akupatie joto.”

Daudi muda huo alikuwa tayari mzee sana takribani miaka 90, akaoa binti wa miaka takribani 9 ama 10, kwa uzee alionao Daudi kwa miaka hio ilikuwa ngumu kufanya tendo na binti lakini binti aliweza kulala nae kitanda kimoja kwajili ya kumpa joto pekee pasipo kufanya s*x.

Mabinti wenye miaka chini ya 12 walijulikana kama NA’ARAH ( נַעֲרָה ) - hawa ni mabinti ambao waliweza kuolewa na wafalme ama viongozi wa dini wa hadhi ya juu (high priests) katika falme ya israel, ikumbukwe kwa wakati huo tamaduni za Israel ilikuwa kwamba binti akishafika miaka 12 na kuaga rika la NA’ARAH hapo ilikuwa ndio umri wa kuolewa, sijajua ilikuwa vipi mabinti wadogo wa miaka 13 hadi 15 wanaolewa na hata Mariam kuwekwa mimba kimiujiza akiwa bado binti mdogo (toho inanisita kuamini) lakini kwa dunia ya sasa huo umri hatuwezi kukuelewa,

Maandiko yenye mfano wa hao mabinti chini ya miaka 12 kuolewa mfano wake ni huu hapa 1 wafalme 1: 2-3. kwa lugha zingine wametafsiri ni binti mdogo na wengi kwa mazingira ya kisasa tunaweza vuta picha ni binti wa miaka 19 lakini neno lililotumika katika maandiko ya ki israel yameonesha wazi kabisa binti alieolewa ni chini ya miaka 12 a.k.a NA’ARAH ( נַעֲרָה )

1679755907954-png.2565239
Hakuna mtu anaitwa mfalme Daudi Mtanzania, au kwa Karne za Sasa. Hakuna mtu mwenye uthibitisho kwamba mtu huyo alikuwepo. Hivyo hatuwezi kujaribu maadili na mafundisho yetu kwa kufuata hadithi za vitabu vya kuletewa
 
kwa nilichoona hadi sasa ni mambo mengi sana waisrael na waarabu walifanana kwenye tamaduni isipokuwa tu kwavile ukristo ulikulia zaidi ulaya, wazungu wakagoma kuingiza vitabu vyenye tamaduni za ki israel kwenye biblia maana tamaduni za israel zilikuwa tofauti na zao, tamaduni za israel ziliruhusu kuoa zaidi ya mke moja, utaratibu wa urithi, mazishi ni tofauti na tamaduni za ulaya, mambo ya ndoa yamerahisishwa, n.k.
Ufafanuzi kuntu
 
Back
Top Bottom