Mfalme Faisal II wa Iraq aliuliwa 1958 na wanajeshi wake katika mapinduzi

... Unauliza chanzo cha mauwaji kwa waarabu? Ni jadi yao kuinukiana na kumalizana sababu ya fitna na husda tu. Ndio zao.
Kuna jamii gani katika wanaAdam ambayo hakuna mauaji? Ambapo watu hawakupinduana au kuua viongozi wao kwa tamaa za madaraka au sababu zengine?
 
Hawanaga hata sababu za maana Mzee! Soma historia ya Ottoman uone ndugu alipopata ufalme alivoinukia na kuwamaliza ndugu zake wa karibu! Ni watu wa ajabu kidogo; angalau ustaarabu wa kileo ndio umewabadiilisha.
Kwanza WaOttoman sio Waarabu. Labda useme unawalenga Waislam. Hata kama wangekuwa Waarabu, yaliyotokea kwao (kupinduana na kuuwa watawala) yalitokea na hutokea katika jamii zote za WanaAdam. Sijui kwanini hujawa muadilifu.

Ustaarabu wa kileo? Unamaanisha nini unaposema hivyo? Unamaanisha wa Kimagharibi sio? Unajua ni watawala wangapi wameuawa au kunusurika kuuawa katika huo "ustaarabu wa kileo" unaousemea? Unajua kwanini Marekani Viongozi wao wanalindwa sana (tena hata kabla ya vita dhidi ya ugaidi)?

Unaweza kuniambia sababu ya JFK kuuawa? Sababu ya John Hinckley Jr kujaribu kumuua Reagan? Sababu ya kuuawa kwa Olof Palme? Na wengine wengi
 
Abdul Karim Qassim nae akauawa mwaka 1963.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…