Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 20,137
- 26,189
Hatimaye mfalme wa taarabu Alhaji Mzee Yusuph ametangaza rasmi ujio wake kwa mara nyingine kwenye muziki wa taarabu.
Kwa kifupi tangu mfalme akae nje ya muziki wa taarabu , muziki wa taarabu ulikosa radha kabisa maana waimbaji waliobaki wanapiga piga kelele tu cha maana wanachokiimba hakuna.
Tumemiss kusikia ngoma kali za kipindi kile kama vile Wasiwasi Wako ndio maradhi yako,My Valentine, mpenzi chocolate, VIP, Wagombano ndio wapatanao , Two in One nk.
Mzee Yusuph alifanikiwa kuibua vipaji kadhaa cya wasanii wanaofanya vizuri kwenye muziki wa taarabu kama vile Abuubakar Sudi (Prince Amigo) ,Mohammed Ally (mtoto pori), Isha Ramadhani (Isha Mashauzi), Fatma Mahmoud (Fatma Nyoro), Rahma Machupa (Messi) ,Mwasiti Kitoronto nk.
Kwa sasa wasanii walioibuliwa na mzee Yusuph wanafanya vizuri kwenye bendi zao mpya wanazofanya kazi, mfano Fatma Nyoro ni msanii tegemezi wa Yah TMK , Rahma Machupa na Mohammed Ally na Mwasiti Kitoronto ni wasanii tegemezi wa Nakshi Nakshi Modern taarabu chini ya father Mauji na Chidy boy.
Mashabiki tunamsubiri kwa hamu mfalme aturudishe kundini mashabiki zake tulioacha kusikiliza taarabu tangu yeye ajiweke kando na muziki huo.
Na kwa hakika jamaa atapigahela sana .