Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

jimmykb197. Mkuu nifafanulie hapa

4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.
Mwanzo 6 :4
Wana wa Mungu ni wale wacha Mungu wanaotenda mapenzi Ya Mungu katika maisha yao.

Ukisoma Waebrania unaona wazi mwandishi anasema hakuna malaika yeyote ambaye Mungu amemwita mwanaye ila amewafanya malaika kuwa miale ya moto.
Lakini mcha Mungu anaitwa mwana Wa Mungu kwa mujibu wa Biblia. Zaburi 2:7, Matendo 13:33, Waebrania 1:5.

Kwa hiyo kama wana Wa Mungu waliwaona wana wa wanadamu ni wazuri na kujichukulia yeyote na kisha kuzaa nao maana yake walifanya kwa matakwa yao wenyewe na wala si kwa mwongozo Wa Mungu.

Zingatia kwamba mahusiano kati ya wana Wa Mungu na wana wa wanadamu Mungu hakupendezwa nayo na ndiyo maana unaona kizazi hiki cha wanefili kimekuja wakati uovu umezidi sana duniani kiasi kwamba miaka ya mbeleni baada ya haya majitu yaliyotokana na mahusiano yaliyolaaniwa kuzidi katika uovu kuliko hata wazazi wao, Mungu akaamua kuuangamiza ulimwengu wote, ndipo Nuhu na jamaa yake ya karibu sana wakapona maangamizi hayo.

Haya majitu yalikuwa hodari na mashuhuri kwa wakati ule sababu yalikuwa na nguvu, na pia hii ilikuwa ni ishara ya wazi hakikuwa kizazi cha kawaida, mbaya zaidi walitegemea nguvu zao na si kumtegemea Mungu, hivyo walikuwa mbali sana na mapenzi ya Mungu na kuona walijitosheleza sababu ya uwezo waliokuwa nao. Nadhani umepata chochote japo kidogo.
 
naomba kujuzwa kuwa hao Wana Wa Mungu ndio malaika. Ushahidi wowote wa kimaandiko?
Binafsi sijaona sehemu inayo hakikisha kwamba wana Wa Mungu ndiyo malaika, ila ukisoma kisa hiki kupitia kitabu (Biblia ya Roman Catholic) huwa ina maelezo ya ziada kwa chini yanayotoa ufafanuzi zaidi ili kumwelewesha mambo ya ziada msomaji. Hapo ndipo utakuta neno lililoandikwa "Wana wa Mungu au malaika Wa Bwana"
Ila ukisoma katika hali ya ufunuo unaona wazi wana Wa Mungu wakati mwingine ndiyo hao hao wanaitwa mahali pengine malaika Wa Bwana. Kwa sababu hapa wana wa Mungu tafsiri ingine inakuja kuwa ni miungu.

Kwa hiyo kwa ushauri wangu tu jitahidi sana kuushirikisha zaidi ufahamu wako ili upate kuelewa baadhi ya mambo mengine, maana kwa akili tu ya kawaida kuna wakati akili inakataa kabisa kupokea kwa sababu ni mambo yanayohusiana sana na roho.
 
mvua ilinyesha siku 40 tu watu waliteketea ndani ya siku hizo,hizo habari za mwaka umezipata wapi mkuu,kukaa siku 40 bila kula inawezekana hata yesu alifanya hivyo
 
2012
 
mvua ilinyesha siku 40 tu watu waliteketea ndani ya siku hizo,hizo habari za mwaka umezipata wapi mkuu,kukaa siku 40 bila kula inawezekana hata yesu alifanya hivyo
Ni kweli gharika ilikadumu kwa siku 40, lakini maji yalipata nguvu kwa siku 150! Basi soma hiyo Mwanzo sura ya nane yote utapata muda na idadi kamili ambayo maji yalikaa katika uso wa nchi.
 
majini
Halafu msipende kuwafananisha malaika na majini jaman ni viumbe wawili tofauti kabisa jaman majini ni kama sisi tu wanadam baadhi ya sifa zao na zetu zinafanana
hawajaumbwa na udongo inakuaje wawe kama wewe au unamaanisha nini
 
mvua ilinyesha siku 40 tu watu waliteketea ndani ya siku hizo,hizo habari za mwaka umezipata wapi mkuu,kukaa siku 40 bila kula inawezekana hata yesu alifanya hivyo
Ukisoma Mwanzo 7:21-24, utaona hakuna kitu kilichosalia chenye mwili kilichokuwa nje ya safina mkuu. Mungu huwa habahatishi hata
 
Nauliza tu wakati huyo mnefili kajishikiza nuhu akupewa taarifa na Mungu
Mwanzo 8:1-.....
Inasema nuhu alituma njiwa akaangalie Hali ya hewa nje kwanini asingemwambia huyo mnefili aliyejishikiza kwenye hiyo sarina aangalie Hali ya hewa na amjulishe
Na ukisema hakujua kuwa kuna huyo mtu kwanini alichukua njiwa na sio kumuuliza Mungu juu ya Hali ya hewa huko nje au sijakuelewa?
 
Kingine huyo musa alimchoma na mkuki may ambaye ni mkubwaaa kana kwamba musa alionekana kama panzi je kwa skill yako panzi anawezakukuchoma na mkuki ukafa?
Namaanisha kama Mimi mwanadamu nina saizi ya panzi kimwonekano hata mkuki wangu ni sawa nakijiti cha unyasi hakuna ukweli hapo
 
Hapa mwandishi anajitahidi kuelezea namna wale wapelelezi kwa namna walivyoingiwa na hofu na fedheha ndani mwao, ndiyo walivyojiona wao nafsi zao mbele ya yale majitu, hii ilikuwa ni fikra tu ya wale wapelelezi na ndiyo maana baada ya kwenda kutoa taarifa hiyo mbaya kwa wenzo, Mungu aliwakasirikia akawaapia hawataingia katika nchi ile kwa sababu waliwavunja wenzao moyo hata wakamkosea Mungu. Na wale waliowatia moyo wenzao ambao ni Joshua na Kalebu, wao waliingia katika ile nchi na wakamiliki sehemu ya urithi wao
 
Umesoma story ya jamaa jamaa kasema waisrael walikuwa kwenye mahema na wakati huo Huyu ogu akainua mlima kuwaponda bahati mbaya nusu ilimwangukia akaja musa akamchoma alafu anaonyesha Hamas alikuwa mkubwa mno sasa huo mkuki si ungekuwa kama kijiti
 
Mungu alikua na haja gan
 
Ukisoma Mwanzo 7:21-24, utaona hakuna kitu kilichosalia chenye mwili kilichokuwa nje ya safina mkuu. Mungu huwa habahatishi hata
Mkuu soma kitabu cha kumbukumbu na joshua.... Mungu aliapa kuwamaliza wacanaan wote na alisema joshua asiwaonee huruma ila mwisho wa siku mbona Mungu aliwaacha wagibeoni hadi mfalme suleiman alipowaua baadhi yao Mungu alileta ukame mkubwa israel

Mungu ana makusudi na kila jambo huenda alimuacha kwa makusudi yake kama ambavyo aliangusha ukuta wa yeriko ila alimuacha RAHAB pekee
 
Umesoma story ya jamaa jamaa kasema waisrael walikuwa kwenye mahema na wakati huo Huyu ogu akainua mlima kuwaponda bahati mbaya nusu ilimwangukia akaja musa akamchoma alafu anaonyesha Hamas alikuwa mkubwa mno sasa huo mkuki si ungekuwa kama kijiti
Ukisoma vitabu vya wayahudi utakuta mkuki pekee ulikuwa na futi 12 na kilichomuua sio mkuki pekee bali pia vipande vya mawe makubwa vilivyotokana na mlima kupasuka katikati alipokuwa anajaribu kuubeba
 
2Samwali 21:2, Wagibeoni ni kabila inayotokana na Waamori, ambao hapo awali walipaswa na wao wauwawe wote kama wengineo, lakini wao walipoona Waisrael wana nguvu wakaamua kufanya ujanja na hivyo waisrael wakawa apia wagibeoni kwamba hawatawauwa, basi kwa kuwa waliwaapia pasipo kutafuta kusudi la Mungu, Mungu aliwaacha na baadaye wakagundua kumbe hawa walikuwa wenyeji wa nchi ile! Basi wakaamua kuwapa kazi ngumu na kuchanja kuni nk, hivyo wakaachwa hai kwa makubaliano hayo ndiyo maana wakaishi miongoni mwa waisrael.

Kwa kuwa wazee wa kiIsrael waliwaapia wazee wa waamori, Mungu husimamia agano, hivyo Sauli alipowauwa kwa sababu ya faida ya Waisrael Mungu akakumbuka kile kiapo cha miaka hiyo! Ndiyo akaleta adhabu kwa Israeli iliyosababishwa na kosa la mfalme Sauli.

Na kisa cha Rahabu kipo wazi, naye aliapiwa usalama wake na waisrael kwa vile aliwaficha wasionekane na askari wenyeji wa nchi. Nadhani umeelewa
 
Canopy theory is just a conspiracy, no scientific study has ever backed it!
Hakuna maji ya kutosha huko juu kuweza kunyesha na kufunika uso wadunia!
 
Je wewe ni mwana wa Mungu? Na je ukioa wana wa binadamu utazaa wanefili?, au siku hizi duniani tumebaki wana wa Mungu tu? Na je kama tumebaki wana wa Mungu(kwa sifa za wana wa Mungu kibiblia) hukumu ya kazi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…