Inawezekana Lengo lake ni kukufikishia ujumbe kuwa anazipenda tabia za rafiki yako ili nawe nawe ubadilike na kuwa na tabia kama hizo. Tatizo linakuja kwamba hakufikiria madhara ya kukufikishia ujumbe kwa njia ya kumsifia rafiki yako. Inaonekana anakupenda ila upeo wake wa jinsi ya kukufikishia ujumbe ni mdogo.
Jaribu kumfanya hivyo anavyopenda (kama inawezekana, maana kwenye mapenzi hutakiwi kuiga/kujilazimisha tabia ambazo huziwezi/huzipendi) kisha uone kama atafurahia na kuanza kukusifia.
Ukiona hakuna mabadiliko, na masifa bado yanamwagwa kwa rafiki yako, chapa lapa.