Ukifuga mbwa akiuma watu njiani unashtakiwa wewe mfugaji.
Sasa ukichagua viongozi wabovu, wezi na wasiojali umma wa watanzania kama inavyoonyesha, utakuwa umeshiriki moja kwa moja kuharibu nchi yako mwenyewe!
Wakiiba hela dawa zikakosekana hospitali watoto wakafa, ni wewe mpiga kura umeua watoto hao. Elimu ikidumaa ni wewe ndio umeidumaza.
Vifo vya kina mama vikiongezeka, wewe ndo umewaua wamama! Dawa zikikosekana hospitali wewe ndo unahusika.
Na siku ya mwisho, damu za wezi hao (maana wewe ndo umewawezesha kuiba na
ulijua ni wezi lakini ukawapa madaraka!) na za wote waliopotea kwa sababu yako zitakuwa mikononi mwako.
Afadhali ungekuwa hujui kuwa ni wezi, ungesamehewa! Lakini tazama unajua kabisa mambo yote yanayoendelea na unataka kukosea tena kwa makusudi! Na utadaiwa mbele ya haki!
Amua sasa kuitendea haki nchi na taifa lako uepuke hukumu!!