Mzee Mwanakijiji,
Mkuu shukran kwa habari hii lakini mjomba vipi wewe na Pinda kuna kitu gani hasa?...
Tatizo langu ni Pinda ni kuwa akiwa ni muwakilishi wa serikali ametoa agizo la kutaka watu wavunje sheria ati kwa sababu "viongozi wote wamechoshwa". Ingekuwa ni kuvunja sheria ndogo tungeweza kuchukulia alipitiwa lakini alipoitisha watu wauawe hapo hapo alivuka mpaka wa uchungu na kuingia uwanja wa kisasi.
Katika uwanja wa kisasi ni wachache sana hupona, kwani kila mwenye uchungu anakuwa na haki ya kisasi, na kila anayesababishiwa kisasi anapewa uchungu!
Hivyo tatizo langu na Pinda ni kuwa hadi leo hii hajatoa kauli au wito wa kutaka watuhumiwa wa mauaji ya Albino wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na kabisa hajakataza watu kujichukulia sheria mkononi.
Hivi kweli wewe huoni uchungu kwa tukio hili isipokuwa kulitumia kama kielelezo cha yatakayofuata if wananchi watamsikiliza Pinda!..
Uchungu wangu mimi unazidi uchungu wa kihisia. Sioni furaha yeyote katika kuangalia picha hiyo bali kitisho ya nini kinawezekana. Hebu fikiria kama huyo mtu hapo angekuwa anadaiwa kuwa ni muuaji wa albino na wananchi wamemkamata na kumpa kibano? Kwa wengine hilo "anastahili" but what if people are wrong!?
Mkuu haya ni mambo yanayotokea kila siku,
Mzee wewe ni mwingine ambaye anarudia hili kwangu kana kwamba mimi sijui kuwa watu wanauliwa kila siku namna hii. Tangu utoto wangu nimekataa hili na believe me nimepata nafasi nyingine za kulipiza kisasi namna hiyo kwa kumuita mtu mwizi.
Siku moja ilikuwa siku kuu moja hivi ya kidini, pale Mwanza karibu na barabara inayokwenda Isamiliko kwenye kona ya "I turn, U turn" kama blocks tatu au nne kutoka shule ya msingi Nyanza kuna duka la Icecream na vikolombwezo vyako (si mbali sana na Ghandhi Hall). Nikiwa nimejipanga foleni kuwanunulia watoto icecream, popcorn n.k nikasikia mtu kasimama nyuma yangu na yeye akijifanya kuagiza vitu kumbe mkono mmoja alikuwa anani pick pocket..
Bahati nzuri ingawa natoka Bush, mimi si wa bush hivyo, nikakishika kile kidole na kukikunja bila kusema kitu, nikatoka foleni. Nimemkamata hivyoo hivyo bwana mdogo huyo.. nikamuuliza "Nikuitie "mwizi"?" Macho yake na uso wake ulivyobadilika hadi leo nakumbuka. Alipiga magoti na marafiki zake wakaja kuniomba nimsamehe. Nilimuachia. Lakini kama ningeamua kumuitia mwizi, ningemuua yule kijana!
Lakini siku moja kule Tanga maeneo ya New Nguvumali, kuna kijana alikamatwa akiiba "kuku" wa afisa mmoja wa Mkoa na akawa anapelekwa kituoni Chumbageni na raia. Alipofika mitaa fulani hivi vijana wakaanza kuzengea kuuliza kwanini mnapeleka polisi mwizi huyo? wakaanza kudonyoa kwa ngumi, mwisho wale wazee waliokuwa wameshikilia walizidiwa nguvu, na yule kijana aliomba hifadhi ya maisha yake kwa wazee wale lakini hawakuweza kumuokoa. Aliuawa kwa kupigwa mawe! Nilikuwa shule ya Msingi hapo na bado nakumbuka hadi eneo lenyewe (Palikuwa na Mwembe na Bomba la Maji!)
NImeyasema hayo kwa sababu sizungumzii kutoka hewani, na ninafahamu watu kujichukulia sheria mikononi hakukuanza leo. Sisemi kwa sababu sina uchungu bali kwa sababu uchungu ukielekezwa vibaya unafikisha kwenye kisasi.
nadhani ingekuwa bora sana kama ungefuatilia kwa undani kisa hiki na ukayatoa majina ya wahusika, ukasisitiza sheria ichukuliwe dhidi ya huyo mzee uloficha jina lake na kikubwa zaidi wale wote waliohusika na kitendo hiki wafikishwe mahakamani (kwa lugha yenu)...
Laiti ningekuwa na uwezo wa kufuatilia vitu hivi vyote. Ndiyo maana tuna Polisi na vyombo vya usalama.
Binafsi, wote waliohusika na kifo cha huyu mwizi wa mbuzi pamoja na wote wale wanaoiba simu na kuuawa, malipo halili na funzi la kusimamisha sheria ni murder one - hukumu yao ni kifo tu..
Hiyo hukumu haitolewi mitaani bali mahakamani tu baada ya ushahidi wote kutolewa na mtu kupewa nafasi ya kujitetea. Nje ya hapo ni kuishi katika utawala wa mwituni.
Kwa nini usifikirie hivi....kuwa huyo mtu ni sawa na Albino anavyouawa kisha hukatwa viungo vyake miguu na mikono wakaondoka navyo!..
Naweza kufikiria hivyo lakini hilo haliondoi uzito wa kile ambacho macho yameona. Mwizi wa Mbuzi anauawa namna hiyo! na watu wanasimama pembeni kuangalia kana kwamba aliyekufa ni nzi!