Haya sasa hili sakata limechukua new twist...
Waziri afurahia polisi kuwakamata maafisa wa TRA
Na Lilian Lugakingira, Bukoba.
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki amelipongeza Jeshi la Polisi mkoani Kagera kufanikiwa kuwakamata maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wanaodaiwa kusababisha kifo cha mfanyabiashara wa mjini Kayanga wilayani Karagwe, Amri Amir (54).
Maafisa hao wawili, mmoja akitokea jijini Mwanza Kitengo cha Kuchunguza Wakwepa Kodi na mwingine wilaya ya Karagwe walikamatwa kufuatia kifo cha mfanyabiashara huyo ili waisaide polisi.
Balozi Kagasheki alisema anatambua kwamba lazima serikali ikusanye kodi kutoka kwa wafanyabiashara, lakini sio kuitafuta kwa kutumia vitisho kama walivyofanya maafisa hao, na kudai kuwa wakazi wa Kagera wamechoshwa na vitendo wanavyofanyiwa na watu hao.
Alisema hata kabla ya tukio hilo amekuwa akipokea malalamika kutoka kwa wananchi kuhusiana na tabia ya maafisa wa kitengo hicho mkoani hapa ya kuwatisha wananchi.
Balozi Kagasheki alidai kuwa amepata taarifa kwamba maafisa hao walimfuata mfanyabiashara huyo na kumtishia hivyo kuanguka na kufariki kisha wakaingia kwenye gari lao na kutoroka kisha kukamatwa na polisi katika eneo la Buseresere wilayani Chato wakielekea Mwanza.
Alisema, taarifa za uchunguzi zilizotolewa na wataalam marehemu alikufa baada ya kupasuka mishipa kichwani na kusababisha damu kuingia katika ubongo.
Alimshukuru Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Henry Salewi ambaye baada ya kupokea taarifa kuwa watu hao wamekimbia na gari alipiga simu na kufunga mipaka yote ya kutoka mkoani hapa na kisha kupiga simu kwa Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza ili kama wangekuwa tayari wamekwishaingia Mwanza wakamatwe na kurudishwa Kagera.
Balozi Kagasheki alisema maafisa wa TRA hawazuiliwi kutafuta kodi kwa wananchi
bali njia wanazozitumia sio nzuri.
Kwa upande wake, Kamanda Salewi alikiri kushikiliwa kwa watu hao na kuwa wanaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo lililotokea Oktoba 23, mwaka huu eneo la Kayanga, wilayani Karagwe.