Mfanyabiashara afa akihojiwa na TRA

Mfanyabiashara afa akihojiwa na TRA

Haya sasa hili sakata limechukua new twist...

Waziri afurahia polisi kuwakamata maafisa wa TRA
Na Lilian Lugakingira, Bukoba.

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki amelipongeza Jeshi la Polisi mkoani Kagera kufanikiwa kuwakamata maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wanaodaiwa kusababisha kifo cha mfanyabiashara wa mjini Kayanga wilayani Karagwe, Amri Amir (54).

Maafisa hao wawili, mmoja akitokea jijini Mwanza Kitengo cha Kuchunguza Wakwepa Kodi na mwingine wilaya ya Karagwe walikamatwa kufuatia kifo cha mfanyabiashara huyo ili waisaide polisi.

Balozi Kagasheki alisema anatambua kwamba lazima serikali ikusanye kodi kutoka kwa wafanyabiashara, lakini sio kuitafuta kwa kutumia vitisho kama walivyofanya maafisa hao, na kudai kuwa wakazi wa Kagera wamechoshwa na vitendo wanavyofanyiwa na watu hao.

Alisema hata kabla ya tukio hilo amekuwa akipokea malalamika kutoka kwa wananchi kuhusiana na tabia ya maafisa wa kitengo hicho mkoani hapa ya kuwatisha wananchi.

Balozi Kagasheki alidai kuwa amepata taarifa kwamba maafisa hao walimfuata mfanyabiashara huyo na kumtishia hivyo kuanguka na kufariki kisha wakaingia kwenye gari lao na kutoroka kisha kukamatwa na polisi katika eneo la Buseresere wilayani Chato wakielekea Mwanza.

Alisema, taarifa za uchunguzi zilizotolewa na wataalam marehemu alikufa baada ya kupasuka mishipa kichwani na kusababisha damu kuingia katika ubongo.

Alimshukuru Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Henry Salewi ambaye baada ya kupokea taarifa kuwa watu hao wamekimbia na gari alipiga simu na kufunga mipaka yote ya kutoka mkoani hapa na kisha kupiga simu kwa Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza ili kama wangekuwa tayari wamekwishaingia Mwanza wakamatwe na kurudishwa Kagera.

Balozi Kagasheki alisema maafisa wa TRA hawazuiliwi kutafuta kodi kwa wananchi

bali njia wanazozitumia sio nzuri.

Kwa upande wake, Kamanda Salewi alikiri kushikiliwa kwa watu hao na kuwa wanaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo lililotokea Oktoba 23, mwaka huu eneo la Kayanga, wilayani Karagwe.

Masatu,
Watu hawa wa sisiemu yako wanacheza double standard. Na hasa huyu fisadi mdogo Kagasheki.
Hivi unamjua Kagasheki wewe? Huyu ni msema hovyo kwa kila kitu kinachowagusa watu hata kama kisheria kiko sawa. Ni huyu huyu amekuwa aki support biashara ya pikipiki Bukoba kwa kudandia hoja za kafu, ambayo kisheria haipo badala yake inatakiwa irekebishwe sheria na hajafanya chochote mbali na hizi kele zisizo na sababu anazotaka kuaminisha watu kwamba, his on their side .
Hawa mabwana wa TRA kwanza they are pumba**'s. wao walikuwa kazini na hawakuwa na kosa lolote. Nini kiliwakimbiza? Mi nadhani si ajabu kwa ule mshituko wa kuona mtu akifa mbele yao nao wangeanguka wakafa kama wangekuwa na presha pia.
Hata haya mambo yanayozungumzwa hapa kuwa alitishiwa ni ujinga mtupu kwa sababu hakuna aliyekuwapo. Wao watu wa TRA mara zote huwa wanakwambia ukweli jinsi sheria ya kodi inavyokutaka ulipe kiasi ulicholimbikiza na fine yake, regardless ni kubwa kiasi gani. Basi!. Kilichobaki ni wewe kusuka ama kunyoa.
Hizi sheria za kodi zilishasemwa siku nyingi na watu wamezipigia kelele si leo wala jana wala juzi. Kila siku watu wamesema jinsi sheria hizi zilivyo kandamizi maana hazina transparency.
Walipa kodi wa Tanzania wanategemea huruma ya tax officers katika kuwa taxed. Na Tax structure ya kitanzania iko negotiable kwa maana inampa mteja ( yaani mlipa kodi) uwanja wa ku negotiate na wakubwa wa kodi maana watu hawajui walipe nini na nini waache. Ukienda kulipa huyu anakwambia lipa hizi. Na mwaka kesho mwingine anakwambia mwaka jana ulilipa kidogo inatakiwa uongeze hizi... na baada ya miaka miwili mwingine anakwambia mwaka juzi na mwaka jana ulilipa kidogo inabidi uongeze hivi. Na ujinga huu unaendelea hivi kila leo kiasi cha kusababisha rushwa kwa ma tax officers.
Haya serikali inajua na Kagasheki na mafisadi wenzake wanajua na hawataki kubadilisha sheria maana wanadai kwa njia hiyo eti watajisifu jinsi walivyokusanya kodi kubwa. Ujinga mkubwa huu mwingine kwa watanzania. Shame on them.
Kibaya zaidi wanayo sera ya kutolipisha hao wajinga na wezi wenzao wanaowaita makada na wafadhili wa sisiemu. Hiyo sera si rasmi hivyo kwa bahati mbaya anaponaswa huyo mwizi mwenzao bila wao kujua. Haya ndiyo malipo. Na nawambia wako wengi wanaokutana na haya na hawajaandikwa magazetini maana wengine walipata hata strokes na wameugua na kufa bila ripoti.
Nawambia ndugu zangu, Mungu yuko kazini ku eliminate wote wanaotuibia na wataondoka mmoja mmoja hadi waishe. Hakuna atakayesalia nakwambia. Pressure zitawamaliza. Rudisheni pesa za watanzania, ili mpone.
Wito wangu kwa wakuu kama Masatu na wengine mnaoishutumu TRA kwa nini msiilaumu serikali hii ya wezi ambayo imekumbatia sheria mbovu za kodi ikiwa inaelewa kuwa ni mbovu? Kwani ni lazima niende kwa waziri wa pesa au kwa boss wa TRA au hata kwa JK ili nipate favour ya kulipa kodi inayopaswa kulipa? Kwa nini watu wasilipe kodi kama inavyotakiwa? Na kwa nini kodi ziwe ambazo sio affordable?
Nawambia ukweli katika dunia hii hakuna anayependa kulipa kodi kirahisi huku akijua pesa yake inakwenda kutumika ovyo. Tena inapotakiwa imsaidie inaonekana eti serikali inam favour kwa kumpa maendeleo. Usipo weka vitisho hakuna atakayelipa hata mmoja!!!!
Nyie Kagasheki acha ubabaishaji kwa kuwa aliyekufa ni shabiki wa sisiemu. Wako wengi wanaopata same fate hao mbona hamsemi? Badili hizi sheria. Na Hao waliobaki kwa kampuni ya huyu marehemu walipe kodi kwa kuonyesha hesabu sahihi. Na walipe hakuna msamaha kwa wasiolipa kodi wakati walio na tubiashara tudogo wanalipishwa kwa lazima.
Wale tax officers walikuwa kazini lakini kwa kitendo chao cha kijinga washughulikiwe kisheria.
BTW si ni Rais Kikwete mwenyewe aliyetoa wito kwa TRA kukusanya kodi bila huruma kwa wale wasiolipa? Na hiyo huruma anayotaka kutwambia Kagasheki ni ipi? Je anapingana na boss wake? Shame upon them!😱
 
Masatu,
Watu hawa wa sisiemu yako wanacheza double standard. Na hasa huyu fisadi mdogo Kagasheki.
Hivi unamjua Kagasheki wewe?

Acha kupayuka kama mnywa chimpumu nani kakwambia kuwa nina own CCM?

Rudisheni pesa za watanzania, ili mpone.
Wito wangu kwa wakuu kama Masatu na wengine mnaoishutumu TRA kwa nini msiilaumu serikali hii ya wezi ambayo imekumbatia sheria mbovu za kodi ikiwa inaelewa kuwa ni mbovu?

Nionyeshe nilipowalaumu TRA
 
RIP Amir.
Mimi nadhani kilichomshtuwa si kwamba anadaiwa kodi..Bali ni kitendo cha yeye kama mweka hazina wa ccm na kada maarufu kuulizwa mambo ya kodi.
Hapo naona ninaweza kukubaliana na wale wanasema kuwa ni possible maafisa hao walitumwa kwasababu ya vita ya ndani kwa ndani humo ccm.
Pia kitendo cha kukimbia badala ya ku perform huduma ya kwanza ni kosa kubwa....Wanaweza kusema walitumwa na nani....Kwani si kawaida kwa watu kama hao wa ccm kufuatiliwa kwa style hiyo.
 
Back
Top Bottom