Mfanyabiashara akisema umfuate DM kwenda kujua bei huwa unaenda?

Mfanyabiashara akisema umfuate DM kwenda kujua bei huwa unaenda?

tucker carlson

Senior Member
Joined
Oct 5, 2025
Posts
182
Reaction score
759
Hivi nyie wafanyabiashara huko DM kunakuwaga na viyoyozi?

Mimi huwa nikiona 'DM for price' siendi DM maana nahisi mfanyabiashara anataka kutazama profile yangu nimevaa nini, nina followers wangapi, au nina muonekano gani ili anipangie bei kulingana na muonekano wangu.

Lakini pia nikiingia DM nikamuuliza muuzaji bei, halafu akanitajia bei iliyozidi bajeti yangu mara tatu, inanipa
Inabidi nianze kujieleza, kuomba msamaha, au kumwacha kwenye 'Read', jambo ambalo linajisikia vibaya.

Nyie wenzangu mnaendaga DM kuulizia bei?
 
Back
Top Bottom