Mfanyabiashara apotea Katoro kwa siku 19, mumewe anamtafuta

Mfanyabiashara apotea Katoro kwa siku 19, mumewe anamtafuta

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Mfanyabiashara wa pembejeo za kilimo na mifugo, Yohana Zakaria, mkazi wa Katoro mkoani Geita, anaendelea kumtafuta mkewe, Tatu Kimori, ambaye alitoweka nyumbani tangu Machi 2 mwaka huu.

Tatu, mwenye umri wa miaka 46, alimuaga mume wake akielekea Sirari Mkoani Mara kwa ajili ya kufuatilia mzigo wa biashara yao, lakini mpaka sasa siku 19 zimepita na hajapatikana.

Zakaria amesema kuwa amefanya juhudi mbalimbali kumtafuta mkewe akishirikiana na ndugu wa Tatu, lakini bado hakuna taarifa yoyote iliyosaidia kumuelekeza alipo.

Hali hii imemuweka katika wasiwasi mkubwa huku akieleza kuwa ameshindwa kupata mafanikio licha ya kutumia njia zote anazoweza.

Mume huyo ameongeza kusema kuwa tayari ameenda kutoa taarifa polisi ambapo alipewa RB namba GER/GD/PE/48/2025, lakini juhudi zake hazijazaa matunda yoyote ya maana.

Tangu kupotea kwa Tatu, Zakaria amekuwa na hofu kubwa kuhusu usalama wa mkewe.

Waandishi wa habari wamefika ofisi ya Polisi Mkoa wa Geita kufahamu hatua zilizochuliwa juu ya tukio hilo, kaimu kamanda wa polisi Geita Adam Maro alishauri waandishi kuwasiliania na Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya na tulivyosiliana na Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mark Njera aliomba atumiwe ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) na alipofahamishwa juu ya tukio hilo alijibu kwa ujumbe mfupi wa simu kuwa hana taarifa hizo.

 
Mama afanye biashara ya kusafiri, wewe baba uko nyumbani, ni hatari kwa usalama wa ndoa.
 
Back
Top Bottom