Mfanyabiashara Boaz amepotea anatafutwa na ndugu zake

Mfanyabiashara Boaz amepotea anatafutwa na ndugu zake

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Wakuu matukio ya watu kuendelea kupotea yanazidi kuendelea

Mfanyabiashara wa Spea maeneo ya Tabata Dampo Dar es salaam aitwae Boaz Nyimbo anatafutwa na Ndugu, Jamaa na Marafiki baada ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Jumamosi tarehe 4 January 2025.


Ndugu wa karibu wameeleza kuwa siku ya Jumamosi Boaz alitoka kwenda kazini na baadae jioni alitoka kwenda kuangalia mpira wa Yanga na kurejea nyumbani ambako hakukaa sana akamuaga Mkewe kwamba anatoka mara moja atarejea lakini hakurudi nyumbani wala kujulikana alipo hadi leo na simu zake hazipatikani.

“Tunamtafuta ndugu yetu Boaz Nyimbo ambaye hajaonekana toka Jumamosi 4/1/2025, mara ya mwisho alionekana maeneo ya Tabata, tumemtafuta Hospitali na Vituo vya Polisi bila mafanikio, tunaomba kwa atakayemuona atoe taarifa polisi ama apige simu zifuatazo 0741816232 ama 0755399039, tunashukuru kwa ushirikiano” - imeeleza taarifa ya Familia.
Screenshot 2025-01-11 204934.png


Screenshot 2025-01-11 204631.png

 
Tuishi vizur na watu,sahv sio lazima mpaka umtukane chura kiziwi hata jirani anaweza kukupoteza au mkeo
 
Back
Top Bottom