Mfanyabiashara na Mwekezaji wa Mbeya Joseph Mbilinyi asaini Mkataba wa kusimamia Masuala ya Logistics za kampuni ya Wachina

Mfanyabiashara na Mwekezaji wa Mbeya Joseph Mbilinyi asaini Mkataba wa kusimamia Masuala ya Logistics za kampuni ya Wachina

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Joseph_O._Mbilinyi_on_Instagram:_“MFANYABIASHARA_wa_MBEYA_leo_nimesaini_MKATABA_na_kampuni_moj...jpg


Hii ndio Taarifa ambayo Mwekezaji Mzalendo Ndugu Mbilinyi ameisambaza kwa vyombo vya habari vya ndani na Nje ya Nchi , wakati akitia Saini Mkataba huo wa kusimamia masuala ya Logistics mbele ya jopo la Wanasheria wake wa Kimataifa na washauri wake wa masuala ya biashara Mjini Iringa

Sugu amesema kwamba ameingia kandarasi hiyo ya mwaka mmoja yenye kipengere cha kuongezwa ikiwa kila upande utaona umuhimu wa kufanya hivyo .

Ni wazi sasa kwamba milango ya uwekezaji iliyoharibiwa kwa miaka 6 inaanza kufunguka na kurudi upya .
 
Mijitu ya ccm yenyewe inaiba hela kisha inaficha hela nje ya nchi badala ya kuwekeza kama Sugu

Sugu moto chini
Hata mimi niko njiani kuingiza nchini dollars million hamsini awamu ya kwanza kusikilizia. Wakinishawish kuna mazingira mazuri ya uwwkezaji na haki za binadamu naongeza zingine 200million dollars halafu baadaye naongeza
 
Hata mimi niko njiani kuingiza nchini dollars million hamsini awamu ya kwanza kusikilizia. Wakinishawish kuna mazingira mazuri ya uwwkezaji na haki za binadamu naongeza zingine 200million dollars halafu baadaye naongeza
karibu sana mkuu
 
Sugu angeendelea kuwa mbunge asingepata akili ya kuwekeza fedha alizopata kama kiinua mgongo. Tena ameamua tayari kesha chelewa.

Tanzania kila baada ya miaka mitano, tunatengeneza ma milionea wapya 400 ambao ni wabunge. Badala ya pesa waloyoipata wawekeze kufungua ajira mpya, wanaenda kuhonga wajumbe ili warudi bungeni.

Kukomesha tabia hizi, katiba mpya iweke vigezo vifuatavyo:-

1. Mbunge aruhusiwe kugombea kwa vipindi viwili tu. Akimaliza afanye kazi nyingine.

2. Kwa anayetaka kuendelea, tuweke kigezo cha awe ameajiri watu wasiopungua 500 na wawe wanalipa P.A.Y.E. Hii itasaidia kuongeza uwekezaji.

3. Kwa shughuli za shamba, uvuvi na ufugaji, tuweke sharti la mfano mtu awe analima heka kuanzia 1,000

4. Wasafirisha mazao mfano mtu akiweza kupata soko nje ya nchi, anachukua mazao na anayaprocess na kusafirisha, huyo pia awe na sifa za kuongeza toka 10yrs na kuendelea.

Hapa tutakuwa tumelazimisha badala pesa kuhongwa wajumbe, itumike kufanya uwekezaji.

Sugu hongera sana
 
Back
Top Bottom