Mfanyabiashara wa huduma za kifedha apotea katika mazingira ya kutatanisha Arusha. Mke wake asimulia kilichotokea

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Mfanyabiashara wa huduma za kifedha (wakala), Davis Mandari (48), mzaliwa wa Kilimanjaro na mkazi wa Kwa Mrefu, jijini Arusha, ameripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Inadaiwa kuwa kabla ya kutoweka, alituma ujumbe mfupi kwa mke wake akidai kuwa amechukuliwa na jeshi la polisi.

Mke wa Davis, Marcy Mandari, amesema kuwa mume wake alitoweka mnamo Machi 9, 2025. Kulingana na maelezo yake, siku hiyo Davis aliaga anakwenda kanisani, lakini akiwa njiani, alimtumia ujumbe mfupi wa simu (SMS) akisema kuwa ameshikiliwa na polisi.

Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Hata hivyo, baada ya kupokea ujumbe huo, Marcy alijaribu kumpigia simu mumewe lakini haikupokewa. Tangu siku hiyo, simu ya Davis imeendelea kuwa kimya.

Marcy amesema amefanya jitihada kubwa kumtafuta mume wake kwa kutembelea vituo vya polisi, hospitali na mochwari mbalimbali jijini Arusha, lakini hajafanikiwa kumpata.

Ameeleza kusikitishwa na tukio hilo akisema kuwa mume wake hakuwa mtu wa makundi, mgomvi, wala hakuwa na uhusiano wowote wa kisiasa, hivyo anashindwa kuelewa alipo.

Pia Soma: PreGE2025 - Familia ya Daniel Nyamhanga yamuomba Rais Samia kuwasaidia kupata, wasema ushahidi upo akichukuliwa na watu wasiojulikana

Ameiomba serikali na jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina ili mumewe apatikane, kwani familia yao inamtegemea, hasa watoto wao watatu ambao wote bado wanasoma.

Source: Jambo TV
 
Mungu amsaidie apatikane. Hata kama kuna kosa alifanya haihalalishi yeye kutekwa au kupotezwa. Jeshi la polisi pia lijitokeze baada ya kutajwa.
 
Siku nikisikia mtoto mmoja tu wa kiongozi mashuhuri katekwa na asitafutwe kabisa mnijulishe

Mi naona nchi yangu ni kama inawatu maalumu na wasio maalumu
 
Hali inatisha mno, utekaji umeshamiri kwa kasi, hakuna amani tena ndani ya nchi hii.

Jah tusaidie.
 
Huyu mama mbona anaongea kama hana ofu yoyote, anaongea kwa vituo, anyway ni mawazo yangu.
 
Body language ya mke wa aliyepotea inatia Shaka kidogo.
Ingawa Haimaanishi police wasifanye jitihada za kumtafuta huyo mtu.
 
Bahati mbaya polisi wamejichanganya na wahalifu kwenye haya matukio ya utekaji. Kwa hiyo inatuwia vigumu baadhi yetu kufahamu ni nani hasa waliomteka.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Wakuu,

Mfanyabiashara wa huduma za kifedha (wakala), Davis Mandari (48), mzaliwa wa Kilimanjaro na mkazi wa Kwa Mrefu, jijini Arusha, ameripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Inadaiwa kuwa kabla ya kutoweka, alituma ujumbe mfupi kwa mke wake akidai kuwa amechukuliwa na jeshi la polisi.

Mke wa Davis, Marcy Mandari, amesema kuwa mume wake alitoweka mnamo Machi 9, 2025. Kulingana na maelezo yake, siku hiyo Davis aliaga anakwenda kanisani, lakini akiwa njiani, alimtumia ujumbe mfupi wa simu (SMS) akisema kuwa ameshikiliwa na polisi.

Hata hivyo, baada ya kupokea ujumbe huo, Marcy alijaribu kumpigia simu mumewe lakini haikupokewa. Tangu siku hiyo, simu ya Davis imeendelea kuwa kimya.

Marcy amesema amefanya jitihada kubwa kumtafuta mume wake kwa kutembelea vituo vya polisi, hospitali na mochwari mbalimbali jijini Arusha, lakini hajafanikiwa kumpata.

Ameeleza kusikitishwa na tukio hilo akisema kuwa mume wake hakuwa mtu wa makundi, mgomvi, wala hakuwa na uhusiano wowote wa kisiasa, hivyo anashindwa kuelewa alipo.

Ameiomba serikali na jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina ili mumewe apatikane, kwani familia yao inamtegemea, hasa watoto wao watatu ambao wote bado wanasoma.

Source: Jambo TV
Makonda ameshapita naye huyo
 
Back
Top Bottom