DOKEZO Mfanyabiashara wa Magari, Gideon Mlokozi Mashankara amepotea

DOKEZO Mfanyabiashara wa Magari, Gideon Mlokozi Mashankara amepotea

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ningekuwa mwanaharakati at risk...

Popote ambapo nakuwepo kwa muda mrefu nahakikisha nina handcuffs - au mnyororo na kufuli lisilokuwa na funguo linalojiloki ukifunga - au lock ya baiskeli.

Wahuni wakija najifunga mguu kwenye kitu kama meza kubwa au nguzo. Kukudhuru watakudhuru tu. Heri washindwe kukubeba wakupigie uwanja wako wa nyumbani kuliko wakakupigie ugenini.
Yote hayo ya nini kujiumiza kwa kutumia lock ya baiskeli. Ungelikuwa wewe ni Mwana harakati ningekwambia nitafute kwa wakati wako ili nikufanyie dawa wahuni wakikutafuta hawakuoni na wewe unawaona na hata majambazi au wahuni wakikujia nyumbani unajikuta umepotea ndani ya nyumba umetoweka hawawezi kukuona na wala kukukamata dawa zipo hizo .
 
Unaweza ukadhani kama taifa tuna janga la utaahira yaani mtu anakamatwa kwa nguvu na watu ambao hata gari haina namba mnaangalia tu vijana wa daisalamu ni sifuri kabisa
 
 
 
Hivi ni kwanini mtu anapochukuliwa na watu msiowajua msifuatilie hilo gari mpk mwisho mjue anapelekwa kituo gani iwe rahisi kufuatilia?
Pia kuna vitu vinashangaza sana. Yaani mfanyabiashara na mwana harakati unakuja kuchukuliwa kama kuku tu. Yaani unashindwa kutafuta mguu wa kuku ufanye kama Zacharia yule mkurya alivyofanya kule mkoani Mara. Unatekwa na kuuawa kipumbavu bila hata kujitetea?

Vijana mkishakuwa na mali na mkishaanza kujiingiza kwenye uanaharakati, hakikisheni mnakuwa na cha moto. Binafsi naanza mchakato wa kumiliki silaha. Iwe kihalali au kihalifu ila ni lazima niwe na cha moto. Upuuzi kama huo sikubali nife kifala.
 
View attachment 3082444

Anaitwa GIDEON MLOKOZI MASHANKARA ana umri wa miaka 30, mkazi wa Tabata Segerea,

Kazi yake ni mfanyabiashara wa kuuza magari lakini pia ni mwanaharakati huru wa mitandaoni,hajulikani alipo siku ya saba leo baada ya kutekwa na kupotezwa.

Alitekwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari wa jeshi la Polisi siku ya Ijumaa ya tarehe 02 August 2024 majira ya Saa 2 :00 usiku.

Akiwa katika ofisi ya magari ya rafiki yake inayojulikana kama RAPHAEL STAR iliyopo maeneo ya Segerea Stand.

Watu hao waliojitambulisha kama askari wa Jeshi la polisi walikuwa watano,walivamia ofisi hiyo wakiwa wamevalia kiraia na kumuweka Chini ya ulinzi.

Ndipo alipowahoji waoneshe vitambulisho lakini wakakaidi na kudai wanampeleka kituo cha polisi Tabata,atajua huko huko.

Walitumia nguvu na kumfunga pingu kisha wakamuingiza kwenye gari walilokuja nalo aina ya Landcruiser hardtop, ikiwa haina namba

Lakini mashuhuda waliokuwa nje ya ofisi wanasema,gari hilo halikuwa na namba kwa nyuma ila kwa mbele liliandikwa "STL" tu.

Gari hilo halikuelekea Kituo cha polisi Tabata kama walivosema bali lilielekea njia ya kwenda kinyerezi.

Familia ilianza juhudi za kumtafuta vituo vyote vya Polisi Jijini Dar es saalam bila mafanikio

Tulianza kituo cha polisi Tabata, tukaambiwa hayupo na hawana taarifa zake,Tukaenda kituo cha polisi cha Staki Shari,Kinyerezi na Buguruni pia hawakuwa na taarifa zake

Kesho yake asubuhi tuliendelea na vituo vingine tulianzia Central, Oysterbay na vituo vyote bila Mafanikio

Tumezunguka Hospitali zote jijini Dar es saalam na vyumba vya kuhifadhia maiti "Mortuary" bila Mafanikio.

Tulifungua taarifa kituo cha Polisi cha Staki Shari na kupewa RB namba STK/RB/6642/024

Baada ya siku ya tano bila Mafanikio tumeenda Central polisi kufungua jalada la Uchunguz,tumeambiwa upelelezi unaendelea.

Kwa niaba ya Familia tunaomba mtu yoyote mwenye taarifa kuhusu ndugu yetu awasiliane na Baba yake GIDEON kwa namba 0786878133 au kwa namba ya rafiki yake ambayo ni 0624497811

Asante sana.
Isije kuwa ni chuki ya kibishara na yaweza kuwa ni wafanyabishara wenzake wanatumia mwanya uanaharakati kutimiza azma yao kwake.
 
Hivi ni kwanini mtu anapochukuliwa na watu msiowajua msifuatilie hilo gari mpk mwisho mjue anapelekwa kituo gani iwe rahisi kufuatilia?
Hofu km kuna jamaa alitekwa enzi za mzee nankuja wazir akaja kusema atakua mtekwaji kaenda kwa mpenzi wake ctegemei mabadikiko yeyyote siku akitekwa mtt wa waziri naona zitaanza kidgo kukaa sawa twende tu
 
Hivi ni kwanini mtu anapochukuliwa na watu msiowajua msifuatilie hilo gari mpk mwisho mjue anapelekwa kituo gani iwe rahisi kufuatilia?
Utafuatiliaje gari halina namba na pia timing hufanyika haraka mno
 
Anaupiga mwingi Eti.

CCM itapiguwa kura na watekaji 2024 na 2025.
 
Hakuna utete wowote endelea kufanya shughuli zako usiingilie yasiyo kuhusu,hautapotea ,utajiongezea kipato ,utaishi kwa raha mustarehe
Kwamba wanaopotezwa wanakuwa wameingilia yasiyowahusu?
 
Kwamba wanaopotezwa wanakuwa wameingilia yasiyowahusu?
Ndg mbona wewe haujapotezwa ,kila mtu afanye kazi zake ,wanasiasa kweli kweli hawapotezwi ndio maana lema,mbowe ,lisu wapo etc
 
lakini pia ni mwanaharakati huru wa mitandaoni,hajulikani alipo siku ya saba leo baada ya kutekwa na kupotezwa.
Mimi mwenye 'D' mbili nishaelewa hapo kwenye mwanaharakati huru wa mitandaoni.....(hakuna uhuru wa kujieleza mitandaoni kwa ajili ya siasa)....mdomo koma
 
Ukishatanguliza uoga basi ujue umeshashindwa.
Inakuwaje watu mliopo mnashindwa hata kuziba barabara kwa kutumia mawe, magari mabovu/mazima, mapikipiki, miti/magogo, mazagazaga n.k. ili wasiondoke?? Mbona mko sharp sana ktk kukimbiza/kufukuzana na kupambana na vibaka; hapo imekuwaje??
Watu watano tu wamefanikiwa kupita na mpendwa wenu huku nyie mnakazania kusoma plate no. eti imendikwa STL tu....
Mkamataji kama hatoi kitambulisho/hajavaa sare na hajafuatana na mwenyeji yeyote e.g. Mtendaji au hata mjumbe; fasta Piga kelele/filimbi, Kusanya Nzi , chukueni Sheria Mkononi chap. Mambo mengine bhana dah!
madini haya mzee
 
Back
Top Bottom