Mfanyakazi usithubutu kuacha kazi kwa kushawishiwa kwa njia yoyote ile

Mfanyakazi usithubutu kuacha kazi kwa kushawishiwa kwa njia yoyote ile

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
4,580
Reaction score
7,943
Habari wanajukwaa!

Uzi huu ni maalumu kwa ajili ya waajiriwa wa serikali na wale wa sekta binafsi. Pia unawahusu wale watakaoajiriwa siku za machoni.

Kuna upuuzi siku hizi unasambazwa sana na watu mbalimbali unaohusu kupondea ajira(kuajiriwa) na kutukuza kujiajiri.

Katika haya maisha kila mtu ana mpango kazi wake kichwani wa kumwezesha kufika mahali pale anapopahitaji, ili kufika mahali unapopalenga unahitaji ushauri kwa sehemu ndogo sana.

Kwanini niseme ushauri unahitajika kwa sehemu ndogo sana?

1. Wewe ndiwe mwenye picha halisi ya kule uendako na utakako

2. Watu wengi hawawezi kubeba mzigo wa mwingine kama mzigo wao. Watu wamejawa wivu (hasa ngozi nyeusi)

3. Watu wanaishi kwa maigizo, mfano humu ndani mtu utakuta amekosa ajira na sasa anasajili line kwa mwezi anaingiza laki mbili tu ila ukiomba ushauri yeye atajiintroduce kama mmiliki wa kampuni na hana mpango wa kuajiriwa tena maishani mwake.

Unaweza kujiajiri ukiwa mwajiriwa na kuzikabili changamoto nyingi kwa urahisi zaidi ya yule asiyeajiriwa. Kivipi?
(A) Ni rahisi kupata mtaji
(B) Ni rahisi kukuza mtaji wako pindi unapoona biashara yako ina soko zuri
(C) Unaweza kuwageuza wafanyakazi wenzako kuwa kama soko la awali huku ukisoma somo la biashara kwa vitendo

Note:
Usiache kazi mpaka pale utakapoona biashara yako inaweza kuendelea kukuingizia fedha hata kama unaumwa ,hapa namanisha mpaka pale itakapojiendesha yenyewe. Uwe jela, uwe umelazwa n.k system iwe inaoperate, kinyume na hapo usithubutu.

Pia napenda kusema kuwa mafanikio ni pale moyo wa mtu unaporidhika na vile alivyo na si kumiliki magorofa au kampuni. Mwingine hata kuwa mpika chai wa waziri kwake ni mafanikio hivyo acha kumbughudhi ili ajione mnyonge aache kazi.
 
Niko kwenye ajira mwaka wa pili huu.Nimeanza Kutrade Forex mwezi September.

Kwa mpunga naopiga next month naandika resignation letter. Kwanini, kwa sababu mshahara wangu wa mwezi naweza kuupata ndani ya week moja soko likikubali.

Kuajiriwa ni utumwa, ukweli utabaki milele Uoga wako Umasikini wako
 
Kuna watu wameibuka siku hizi, wanajiita Inspirational speakers, hawa wanakula sana hela za vijana kwa semina za ujanja ujanja wakihamasisha vijana wajiajiri wakati wao wameajiriwa.
Namkumbuka marehemu Seth (Bikra wa kisukuma) apumzike kwa amani.....
Alikua anapinga sana kuajiriwa, anatoa shule bila ada namna ya kujiajiri, ila hadi anafariki alikua kaajiriwa Efm radio
 
Acha upumbavu wewe...
Niko kwenye ajira PSRS (Utumishi Portal System Admin) mwaka wa pili huu.
Nimeanza Kutrade Forex mwezi September.
Kwa mpunga naopiga next month naandika resignation letter. Kwanini, kwa sababu mshahara wangu wa mwezi naweza kuupata ndani ya week moja soko likikubali.
Kuajiriwa ni utumwa, ukweli utabaki milele
Uoga wako Umasikini wako (Bila shaka wewe ni Mwalimu wa secondary)
Kujitangaza kazi unayofanya ni dalili kwamba una dream ya kupata hio kazi.

Keep on dreaming
 
Acha upumbavu wewe...
Niko kwenye ajira PSRS (Utumishi Portal System Admin) mwaka wa pili huu.
Nimeanza Kutrade Forex mwezi September.
Kwa mpunga naopiga next month naandika resignation letter. Kwanini, kwa sababu mshahara wangu wa mwezi naweza kuupata ndani ya week moja soko likikubali.
Kuajiriwa ni utumwa, ukweli utabaki milele
Uoga wako Umasikini wako (Bila shaka wewe ni Mwalimu wa secondary)
Sasa wote tutaacha kazi tuje forex???
Wengine wakafuge, wengine muende forex, wengine wakalime, wengine tubaki kuhudumia umma....
 
Acha upumbavu wewe...
Niko kwenye ajira PSRS (Utumishi Portal System Admin) mwaka wa pili huu.
Nimeanza Kutrade Forex mwezi September.
Kwa mpunga naopiga next month naandika resignation letter. Kwanini, kwa sababu mshahara wangu wa mwezi naweza kuupata ndani ya week moja soko likikubali.
Kuajiriwa ni utumwa, ukweli utabaki milele
Uoga wako Umasikini wako (Bila shaka wewe ni Mwalimu wa secondary)
Jamaa muongo sana tena hapo ulipo ni hauna kazi yoyote na hyo forex unaiota ndotoni
 
Jamaa muongo sana tena hapo ulipo ni hauna kazi yoyote na hyo forex unaiota ndotoni

Tazama wewe mtumwa wa ajira.
Leo Jpili nimeingiza Mshahara wa walimu wanne wa secondary.
Angalia Profit hapo juu kabisa change into TZS.
Uoga wako umasikini wako.
cc: Evelyn Salt, Dreka

upload_2017-11-26_23-42-6.png
 
Acha upumbavu wewe...
Niko kwenye ajira mwaka wa pili huu.
Nimeanza Kutrade Forex mwezi September.
Kwa mpunga naopiga next month naandika resignation letter. Kwanini, kwa sababu mshahara wangu wa mwezi naweza kuupata ndani ya week moja soko likikubali.
Kuajiriwa ni utumwa, ukweli utabaki milele
Uoga wako Umasikini wako (Bila shaka wewe ni Mwalimu wa secondary)
Daaaah we jamaa si juzi tu ulikua unalilia mshahara leo hii ushakua tajiri wa forex unawaambia wenzio waache kazi?
Ama kweli maisha bila unafiki hayaendi
e4558cdaecb9ff64737d9dbf5e972330.jpg
944704163041c8a1e080fba5c6f2fe69.jpg
 
Back
Top Bottom