Habari wanajukwaa!
Uzi huu ni maalumu kwa ajili ya waajiriwa wa serikali na wale wa sekta binafsi. Pia unawahusu wale watakaoajiriwa siku za machoni.
Kuna upuuzi siku hizi unasambazwa sana na watu mbalimbali unaohusu kupondea ajira(kuajiriwa) na kutukuza kujiajiri.
Katika haya maisha kila mtu ana mpango kazi wake kichwani wa kumwezesha kufika mahali pale anapopahitaji, ili kufika mahali unapopalenga unahitaji ushauri kwa sehemu ndogo sana.
Kwanini niseme ushauri unahitajika kwa sehemu ndogo sana?
1. Wewe ndiwe mwenye picha halisi ya kule uendako na utakako
2. Watu wengi hawawezi kubeba mzigo wa mwingine kama mzigo wao. Watu wamejawa wivu (hasa ngozi nyeusi)
3. Watu wanaishi kwa maigizo, mfano humu ndani mtu utakuta amekosa ajira na sasa anasajili line kwa mwezi anaingiza laki mbili tu ila ukiomba ushauri yeye atajiintroduce kama mmiliki wa kampuni na hana mpango wa kuajiriwa tena maishani mwake.
Unaweza kujiajiri ukiwa mwajiriwa na kuzikabili changamoto nyingi kwa urahisi zaidi ya yule asiyeajiriwa. Kivipi?
(A) Ni rahisi kupata mtaji
(B) Ni rahisi kukuza mtaji wako pindi unapoona biashara yako ina soko zuri
(C) Unaweza kuwageuza wafanyakazi wenzako kuwa kama soko la awali huku ukisoma somo la biashara kwa vitendo
Note:
Usiache kazi mpaka pale utakapoona biashara yako inaweza kuendelea kukuingizia fedha hata kama unaumwa ,hapa namanisha mpaka pale itakapojiendesha yenyewe. Uwe jela, uwe umelazwa n.k system iwe inaoperate, kinyume na hapo usithubutu.
Pia napenda kusema kuwa mafanikio ni pale moyo wa mtu unaporidhika na vile alivyo na si kumiliki magorofa au kampuni. Mwingine hata kuwa mpika chai wa waziri kwake ni mafanikio hivyo acha kumbughudhi ili ajione mnyonge aache kazi.