Pantomath
JF-Expert Member
- Jan 4, 2019
- 842
- 3,449
Nimeamini kuna watu wana kismati tuu. Wakati naanzisha hii biashara nilikaa mwenyewe kwa mda flani ambao nilikua free,
Nikaona mauzo yanaenda poa tuu,
Baada ya majukumu ya kikazi kuanza nikatafuta sista duu haswaa, nikamuweka pale, Mauzo yalashukaa, sio kama hana lugha nzuri, anahudumia vzr na ni mzoefu sana
Kwa ufupi kwake niliweka matarajio makubwa ila mwishowe ni disappointment, Baada ya mda akapata mishe nyingne kwa uzuri wake akasepa na hatimaye hivi karibuni ataolewa na Moja ya wateja wake kipindi yuko hapa kazini.
Sasa sababu ilikua ghafla ikabidi nimchukue mdogo wangu akiwa anasubiri kwenda zake chuo. Huyu hana uzoefu wowote yaani siku nampeleka dukani nampa maelekezo nafanya ile tuu basi ila sikua na imani, kuachana na yote hayo bado ni mtoto.
Kwakua mwanzo biashara haikua ikienda basi nilijiwekea kila mwisho wa week ndio naulizia mauzo. Huyu ndio nikakaa kimya kabisa mpk week ya pili ndio nikauliza kiunyonge. Sikutegemea, alinipa mauzo ambayo sio mimi wala yule tulishawahi fikisha hata kwa mwezi, sikuamini, n
Nikahisi ni upepo tuu wa week mbili, cha kushangaza upepo huo ni miezi bado unaendelea, Week hii nikapata ka likizo nikasema nirudi nikakae mwenyewe,
Nimeishia kula za uso, Hapa nimemwambia kesho rudi golini na Nitakua nakulipa rasmi itakusaidia matumizi chuo, ada mahitaji mengine tuachie sisi au ukikwama niambie.
Mwanzo yeye na wazazi walisema haina haja ya kumlipa yeye anafanyia kazi ya ndani kwahio nikawa nampa tuu kajipesa kwa kushtukiza.
Nimepiga mahesabu kila kile kipo sawa.