Mfanyakazi yeyote mwenye akili hawezi kuwa na urafiki wenye afya na Mwanasiasa

Mfanyakazi yeyote mwenye akili hawezi kuwa na urafiki wenye afya na Mwanasiasa

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
16,583
Reaction score
42,992
1. Ndie anaeamua ulipwe kiasi gani.

2. Ndie anayebutua mkataba wako wa ajira Kama ilikuwa ya kudumu inakuwa on temporary basis.

3. Ndie anayeweza kuamua uongezwe makato au uongezewe Kodi kwenye mshahara wako.

4. Ndie anayeweza kuamua ulipwe au usilipwe mafao yako. Mfano fao la kujitoa au wale wastaafu wa iliyokuwa Afrika Mashariki.

5. Ndiye anayeamua ufukuzwe kazi ama la.

Haya ndio mahusiano ya wanasiasa na wafanyakazi popote duniani hasa nchi ambazo mifumo yake ya utawala haijakaa vizuri. Hivyo mfanyakazi unapoamua kuwa na mapenzi na mwanasiasa basi ujue na hizi konsekwensesi.
 
Kuna haja ya kuwa makini sana wakati wa kufanya chaguzi jamii itafakari upya namna bora ya kuweka viongozi madarakani.

Hakuna kitu kinacho kera kama kumchagua kiongozi badala ya kutekeleza yale tuliyokusudia anaanza kupabana na wapiga kura kwa kuwatafutia makosa ili kuwakomoa!

Kweli tuliwachagua mtuchape viboko,mtufukuze kazi bila kufuata sheria?

Unajisikiaje unasimama kwenye mkutano na kumsimamisha kazi mtumishi bila kuwa na ushahidi ukimtuhumu na tuhuma hewa?

Kazi kubwa inahitajika kuikomboa nchi kutoka katika fikra kandamizi ni muhimu kuanza na sekta ya sheria hivi majuzi wamepitisha sheria na kuongeza usajili wa wanasheria lakini waheshimiwa hawa wanavyo tekeleza sheria mpya kwa upendeleo na mwendo wa konokono ni mwanzo wa kudunisha haki katika nchi hii izidi kujichimbia shimo.

Nakubaliana nawe kwamba wanasiasa ndiyo kila kitu ni muhimu tukapata dawa ya kudumu dhidi yao.
 
Tatizo lilianzia tangu enzi za awamu ya kwanza ambapo siasa zilipewa kipaumbele kwenye nchi hii. Mwanasiasa hata awe mjinga mjinga anaonekana ana nguvu kuliko hata maprofesa, suluhisho ni kurejesha mchakato wa katiba mpya ambapo zitaundwa taasisi imara ambazo hazitayumbishwa na mwanasiasa yoyote. Wanasiasa wabaki kuhamasisha yale ambayo yameshapitishwa na wataalamu..
 
Halafu tunachagua wabunge ambao hata elimu yao ni ya std 7 tena ya kuchechemea. Mnategemea nini.
 
Back
Top Bottom