elle ruth
New Member
- Oct 17, 2017
- 1
- 1
MFAWIDHI
Ilikuwa Usiku wa saa nane wenye giza pasi na mwanga wa mwezi, mvua za upepo mkali zilifanikiwa kuvuja mpaka ndani. Hali iliyomuamsha binti mrembo mweusi macho yake meupe makubwa ya mviringo na shingo yake ndefu kama twiga hakika alipendeza sana machoni. Radi zilimulika ndani ya dirisha dogo lenye nondo chakavu chuma za bawaba zilipiga kelele dhaifu sauti iliyosababishwa na bundi alietua dirishani hapo akitafuta mawindo alilia kwa sauti “hu - huu- huuu” Hali iliyomfanya Maya kuogopa sana kwakua bundi hakua ndege mwenye sifa nzuri kwenye desturi za kiafrika. Katika sintofahamu hio simu yake ndogo ya tufe zilizochakaa iliita na kumshtua kidogo aliitazama kwa muda kisha akasogea na kuona jina Joyce, binti huyo alikua ni rafiki yake wa muda mrefu aliekua mwaka wa tatu wa masomo chuoni.
“Haloo” ilisikika upande wa pili “Nihadithie ule ubuyu basi shogaa kama bado hujalala, mimi sina hata lepe la usingizi nimeachwa tena moyo unauma mno shoo” alisikika Joyce “pole shoo nani tena kakuacha raundi hii na wewe umezidi kuwa pendapenda, huku kunaogopesha mno natamani tuongee hadi pakuche” Maya alijibu “Nani mwingine zaidi ya Derick shogaa kanambia tena anataka nimpe muda” alijibu Joyce kisha simu ikakatika. “ngoja nijiunge haraka nimpigie Maya maana huu usiku sijui utaishaje mwenzenu” alijisemea huku akimpigia tena Maya bila mafanikio. “sasa mimi nifanye nini na madakika yote haya ngoja nijaribu kumpigia D tena” alipiga na kupiga mara ya tano simu ilipokelewa na sauti nzuri ya mwanamke ikasikika “Halo! Joyce pumzika mama, mimi na mume wangu na watoto tumepumzika pia ni usiku sana kipenzi” mkewe Derick aliongea kisha akakata simu kabla hata Joyce hajajibu chochote.
Joyce alikaa chini na kunyoosha miguu kwa mshtuko ni kama alipigwa na shoti alisikia baridi mwili mzima. mwanaume aliyekua wakipendana na kuahidiana maisha ameoa? mbona hakusema? ataambia nini familia yake? Alikumbuka watu walivyoleta masufuria, maturubali na viti kwa ajili ya sherehe ya mahari aibu ataipeleka wapi? simu ile ilizidi kumchanganya kabisa aliingia whatsapp na kwenda kwenye ukurasa aliokuwa akichat na Derick asione picha kwenye wasifu wake, alishtuka kidogo lakini alipojaribu kutuma ujumbe haukupokelewa akajua ameshasitishwa mawasiliano naye. Akaingia kwenye grupu la chuo la whatsapp na kuona ujumbe kwamba matokeo yametoka, kwa haraka akaingia kwenye account yake ili kujihakikishia alijikuta ana supplimentary tatu na somo moja amebeba, yani kushindwa kufuzu. Aliyatazama yale matokeo kwa muda mrefu asiamini hadi usingizi ulipompitia.
Upande wa pili Maya aliamka na kujiandaa haraka na kwenda kuripoti halmashauri ambapo ndipo angeelekezwa mipango yote ya kupangiwa kituo cha kazi. “umepangiwa kituo gani binti?” aliuliza mwanaume mmoja alieitwa Mzee Kazi, mzee huyo alifanya kazi kwa kitambo kirefu nae alikaribia kustaafu ofisini hapo huku akimuangalia kuanzia miguuni, kwenye maungo yake hadi kwenye sura yake ya kuvutia “nimepangiwa shule ya msingi Kasheshe” alijibu Maya. “ mh utaweza kweli wewe yale mazingira ya kijijini? na ulivyo binti mzuri kule si utapotea kabisa wewe? embu ukimaliza kujaza hizi fomu unione!” mwanaume yule aliongea huku akimpa simu yake aandike namba zake. aliazimia kukutana na babu yule baada ya muda wa kazi ili waweze kuongea labda anaweza kusaidika.
Alipofika kwenye nyumba ya kufikia wageni alimkuta Mzee Kazi amekaa na bia zake mbili za safari alimwelekeza Maya akae huku akimuita mhudumu. “agiza utakachotaka, unatumia pombe?” aliuliza Mzee Kazi. “hapana sijawai” alijibu Maya. “jaribu leo mimi nipo apa usijali ntakulinda” aliongeza Mzee Kazi “asante nitakunywa tu soda baba” basi mhudumu alimletea Maya soda nao walipiga stori kadhaa kuhusu mkoa anaotokea, biashara na watu wake. “mimi ninao uwezo na madaraka ya kukupeleka popote unapotaka,nikipiga simu moja tu! unaonaje tukichukua chumba tukapumzike?” alimuangalia machoni na kumshika kiunoni “unakiuno kizuri sana Maya” alimtoa mikono huku akamwambia “baba kama masharti ya msaada wako ndio hayo, hilo suala mimi sitaweza, nashukuru kwa pendekezo lakini Mungu atanisaidia tu nitaweza kuishi Kasheshe” baada ya muda kidogo Maya aliomba kwenda maliwato nae Mzee Kazi alimpisha huku akitingisha kichwa akimwangalia kwa matamanio.
Ghafla zilisikika kelele nyingi za watu “ameua! ameua!” zilizomwamsha Maya huku kichwa kikiwa kinamuuma kweli kweli kuangalia pembeni alilala Mzee Kazi akiwa mtupu. Kwenye meza aliona vidonge vya bluu (viagra) sigara, msokoto wa bagi na bia mbili! bila hata dakika moja kupita alisikia mlango ukigongwa, alivoangalia ndani ya shuka naye alikua mtupu. katika taharuki ile alisikia kitasa kikipekenywa na funguo na kisha kufunguka. watu wengi walijazana nje ya mlango na kuchungulia dirishani.
Askari mmoja alielekea alipolala Mzee Kazi na kumwamsha bila mafanikio ndipo akamgeukia Maya na kumwambia “binti jiandae uvae unahitajika kituoni ili kutoa maelezo” matukio yote hayo yalikua kama ndoto masikioni kwa Maya. alipokua akitoka kwenye chumba cha kupumzikia wageni huku akisindikizwa na askari aliona mke wa mzee Kazi akilia huku akibembelezwa na yule mhudumu aliempokea jana jioni, alimnyooshea Maya kidole na kumshutumu. “wewe ni malaya na muuwaji! mme wangu jamani mimi mme wangu umeondoka jamani, hawa watumishi wa ajira mpya wameniulia mume wangu”. Walipofika kituoni Maya alihitajika kutoa maelezo ya kilichotokea aliulizwa na afande “Enhee binti unaitwa nani? unatokea wapi? mihadarati tulioikuta chumbani ni ya nani? na imekuaje mzee yule akashikwa na umauti akiwa na wewe faragha?” huku akibubujikwa na machozi hajui pa kuanzia alisema kwa kigugumizi “ umauti? mihadarati?” akavuta pumzi na kuendelea “mimi! mimi nlienda uwani nilivyorudi nilikaa na kumalizia kinywaji changu, sijui kingine kilichotokea hadi nilipoamka leo baada ya kusikia kelele kutokea dirisha la chumba nilichokuwepo.” “binti nimekuuliza unaitwa nani? na unatokea wapi na kwanini msichana mdogo hivyo unavuta bangi?” askari alisisitiza “ni muuwaji huyo, nionesheni alipo muuwaji wa baba watoto wangu nimuuwe kwa mikono yangu mimi mwenyewe”. Alisikika mke wa Mzee Kazi kutokea nje ya kituo cha polisi.
simu ndogo ya nokia tochi iliyokuwa mezani iliita kwa sauti, askari aliiangalia kisha akamwangalia Maya na kuashiria anaweza kupokea “haloo! Maya? Maya rafiki angu afadhali nimekupata natamani ata nijiue maisha yangu hayana thamani tena. Derick ameoa jamani, Derick ana watoto watatu na mke jamani watu wanapika pilau apa nje nashindwa kuwaambia mhusika hatofika simu zangu hapokei wala meseji hajibu nimechanganyikiwa mimi” Joyce aliongea kwa haraka bila kumpa Maya nafasi ya kuongea. Maya alimjibu kwa sauti iliyochanganyika na kilio “ukidhania kwako kunaungua rafiki yangu kwa wenzio kunateketea, naomba Mama yangu asiambiwe kuhusu hili nitakalokueleza”

Upvote
1