"Mficha Uchi hazai". Nimeamua kuja kupasua jipu

"Mficha Uchi hazai". Nimeamua kuja kupasua jipu

Sheria ya China inamruhusu mwanamke kumwua mme msaliti endapo tu atakuwa na ushahidi wa kutosha dhidi yake, kwa hiyo mbongo hawezi kuoa mchina.
 
nimekuwa msomaji mzuri sana wa JF hasa nikivutiwa na watu kadhaa wa humu ndani kama akina Sky Eclat , GuDume , Nucky Thompson , Salary Slip, Da'Vinci e.t.c hawa ni watu ambao nimekuwa kwa ukaribu sana nawasoma threads zao sababu ya mambo kadhaa kadhaa. hasa GuDume the great entertainer na mwelimishaji pamoja na Da'vinci kwa makala zake kadhaa.

mwenzenu nimekuja nahitaji mwenzi. nyie wazoefu humu ndani mnisaidie mwanamke ambaye ana jiheshimu mzuri na serious ambaye nitaweza kudate na kuoana naye. kuna watu kadhaa wanasema wameshawahi pata wanawake wa kuoa humu.nami ngependa nifanikiwe.
1. mke awe mzuri rangi yoyote ila asijichubue
2. elimu kuanzia kidato cha sita/diploma na kuendelea
3. awe na tabia nzuri na figure nzuri pia
4. awe na mapenzi ya dhati aliye serious kuolewa na si mdangaji
5. kama ana mtoto anihakikishie kuwa hana mahusiano na baba wa huyo mtoto tena na si zaidi ya mtoto mmoja
6. kazi si lazima awe nayo kama anayo its ok lakini awe tayari kufanya kazi au biashara ikiwa tutakubaliana ili asikae tu nyumbani.
7. awe tayari nipafahamu anapoish naye apafaham ninapoishi
8. awe mstaarabu na ningependa dini awe muislamu
9. awe tayari kujifunza kwangu nami kunifunza ili tuweze ku copy.
10. tukishaanza kuwa karibu baadaye tutumiane picha na kufahamiana

mimi nina miaka 27. nilikuwa masomoni china nimerudi mwaka sasa na nimeajiriwa kampuni flani. si tajiri lakini ninajimudu na naweza kummudu mtu mwingine. naishi dar es salaam ubungo. natumia pombe kiasi si sana. ni maji ya kunde kimo cha wastani na uzito kiasi si sana. naweza zungumza lugha tatu. kiswahili,kiingereza na kichina kiasi. kwa wale walio serious please tuwasiliane. nasisitiza kuwa kigezo cha uzuri na umbo pia vipo na ni muhimu maana sitak mtu wa kumchezea tu.

NB: NImewashirikisha JF sababu naamini mtu ambaye tutakutana kwa jambo hili humu atakuwa serious na mwenye nia hasa. nimechoka kukosa mtu wa kuishi naye na kupanga mipango pamoja.
Huitaji kujieleza sana weka picha tu inatosha.watakuja wenyewe
 
Acha uvivu ingia mitaani ujitafutie mwenyewe
Tena hamba sehem yenye watoto wazuri kama mitaa ya Mbagala. Tofauti inaweza kuwa ni exposure na vigezo vya elimu lakini kwa wife materials,Mbagala kutamu kuliko maeneo ya kujirusha kama Sinza,Tabata na Kinondoni au maeneo ya kishua kama Masaki,O'bay,Mbezi Beach na Mbweni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We unaona ni kazi sana?tunatofautiana uelewa na akili.malezi na pia exposure.ni vitu vidogo sana. Ila nmeshangaa wwe umeona ni kitu kikubwa...

Aisee...mgeni kajua kutag na wenyeji hawawezi mpka sasa. Kweli China kuna maendeleo ya tknolojia ya mitambo na U SPY.
 
Everyone has their choice.just respect mine. Heshima ni kitu cha bure sana kwa wanawake wenye ufaham.wewe watumie hao uliowataja kwa nini unipangie maisha mama?

Umeshindwa kumwambia Mama/Baba, Shangazi/Mjomba, Dada/Kaka hata shekh wakutafutie mchumba mpaka uje utafute kwenye mtandao!!

Eti "tukishazoeana kidogo ndio tutatumiana picha"
Lol 'insecured'

Sent from Jamii Forums using siemens kidole juu.
 
Everyone has their choice.just respect mine. Heshima ni kitu cha bure sana kwa wanawake wenye ufaham.wewe watumie hao uliowataja kwa nini unipangie maisha mama?
Nani kakupangia maisha?
do i know you?? hell no,
that was an advice and nothing more you can take it or leave it.... Maneno yangu sio sheria.

Heshima??? dude, you have issues.

Sent from Jamii Forums using siemens kidole juu.
 
Back
Top Bottom