Mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote ndiyo utakuwa mkombozi wa afya za Watanzania. Tushauri uundwe vizuri

Mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote ndiyo utakuwa mkombozi wa afya za Watanzania. Tushauri uundwe vizuri

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,119
Reaction score
4,569
Huduma ya afya ni haki ya msingi kwa kila mtanzania. Ni wajibu wa serikali kuweka utaratibu wa kuwezesha kila mtanzania anapata haki hii ya msingi. The Healthcare must be easily accessible and affordable to every tanzanian.

Huko nyuma hadi mwaka 1998 huduma hii ilikuwa inatolewa bure na serikali kupitia bajeti ya serikali. Mwaka 1999 serikali iliweka utaratibu wa wagonjwa kuchangia kiasi kidogo cha gharama ya matibabu yao ie cost sharing. Kiasi hicho cha mgonjwa kuchangia kikawa kinaongezwa kila mwaka hadi kuwa kikubwa sana.

Ikawa tena siyo cost sharing but full cost. Sana sana mchango wa serikali ukabaki ni kulipa tu mishahara ya watoa huduma. Hadi sasa watanzania walio wengi (takribani robo tatu au zaidi) hawana uwezo wa kupata huduma hii. Our health care is no longer affordable to the majority of our people.

Leo hii watu wengi matumbo yao yakijifunga (bowel obstruction) wanakufa kwani gharama ya kuyafungua kwa operesheni ni malaki kama siyo mamillioni ya pesa. Leo hii matibabu ni kwa wale pesa, wale wengine wamebaki wakihangaika kwa miti shamba na tiba mbadala. They have been denied access to our health care.

Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) ulianzishwa kwa ajili ya watumishi wa serikali ili kutatua tatizo hili. Baadaye serikali iliruhusu mtu ye yote kujiunga na mfuko huo. Lakini gharama za kujiunga na mfuko huo imekuwa kubwa sana hususana full bundle ni TSh 1.5 milioni kila mwaka, kitu ambacho watanzania wengi hawawezi.

Matumaini yao yalikuwa kwenye uanzishwaji wa mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote. Walitegemea utakuwa kweli kwa wote lakini gharama ya kujiunga na mfuko huo ilipopendekezwa na serikali kuwa Tsh 350,000 kwa mwaka, matumaini yao yaliyeyuka.

Serikali inabidi ikubali kwamba watanzania wengi (over 70%) ni wanyonge ambao kipato chao kwa siku hakizidi dollar moja ya kimerikani. Na kwamba mfuko huu wa Bima ya Afya kwa Wote ni kwa ajili ya hawa wanyonge. Tungeweza kuuita Mfuko wa ya Afya kwa Wanyonge.

Mapendekezo
1. NHIF: iendelee kwa wale wenye ukwasi wanaohitaji fast track service au private service au VIP service. Mchango wake ubaki huo wa TSh 1.5 millioni kwa mwaka. Watumishi wa umma waendelee na mfuko huu kwa kukatwa mishahara yao na kiasi kinachobaki kwenye hiyo 1.5 milioni kulipwa na serikali kwenye mfuko huo.

Kwa wale VIP iwe TSh 3.0 milioni kwa mwaka. Makampuni binafsi na watu binafsi wenye uwezo washawishiwe kujiunga na mfuko huu.

Wenye bima hii wataweza kutibiwa hata kwenye private hospitals. Hizo bando ndogo ndogo kwenye mfuko huu ziondewe, ibaki full package na vip.

2. Bima ya Afya kwa Wote
Baada ya zoezi la kisasa la sensa kukamilika, sasa tuna takwimu zote zinazohitajika kukokotoa kiasi cha kila familia au kaya tunachotaka wachangie kujiunga na mfuko huu. Tatizo hadi sasa National Beural of Statistics hawajaweka wazi mchakato mzima wa matokeo ya sensa. Hivyo nilizotumia hapa ni maoteo.

- Kwa mjibu wa sera yetu, wazee wa umri wa miaka zaidi ya 60, watoto chini ya miaka 5 na akina mama wenye mimba matibabu yao ni bure.

Serikali iwalipie Sh 30,000 kwa kila mzee, mtoto na mjamzito kwa mwaka kwenye mfuko huu wa bima kwa wote. Hivyo hivyo kwa kila kaya za TASAF. Nimeotea kundi hili litakuwa na watu au kaya million 5. Hivyo kwa mwaka serikali italipa kwenye mfuko huu Sh 30,000 × 5,000,000 = Sh 150 billion. Hili ni jukumu ambalo serikali na tuiombe isilikwepe.

- Kaya za wanyonge kwa maoteo ya sensa ya 2022 ziko 15 millioni ( bado NB haijatoa takwimu yake hadharani). Nimegawa hiyo population ya 61 million kwa 4. Hawa nao walipe Shs 30,000 kwa kila kaya kwa mwaka. Hivyo watalipa kwenye mfuko huu Sh 30,000 × 15,000,000 = Sh 450 billion.

-Hivyo jumla ya Sh 600 billion kwa mwaka zitalipwa kwenye mfuko huu kwa ajili ya matibabu ya magonjwa yo yote watakayopata wanyonge hawa katika hospitali na vituo vyote vya serikali. Bima hii si kwa kupata matibabu kwenye vituo vya binafsi.

Kwa kiasi hiki cha sh 30,000 kwa mwaka, kuna uhakika wa karibu kaya zote kuweza kulipa bima hiyo kwa hiari bila shinikizo wala tozo.

Sh 600 bilioni zitaweza sana kugharimia au kuchangia gharama za dawa, vifaa tiba, vipimo na operesheni zo zote watakazopatiwa kwani kiasi hiki cha pesa ni sawa na takribani theluthi mbili ya bajeti ya wizara ya afya ya mwaka huu wa fedha.

Tusisahau kuwa population kubwa ya Tanzania (90%) ni la vijana na hivyo ni wachache sana (<10%) watakaougua na kuhitaji matibabu. Ndiyo maana hata mlipuko wa ugonjwa wa corona haukutusumbua sana Tanzania maana sisi ni nchi ya young population.

Tuking'ang'ania kuwachangisha malaki ya pesa kila kaya ya hawa wanyonge uwezekano wa kukusanya hata billioni 50 ni mdogo sana uhakika hatutaweza kukusanya zaidi ya sh 10 billion na tatizo la ku deny access to health care to our people because of affordability will continue.

Mfuko huu lazima uwe full package na kusiwe na ubaguzi au unyanyasaji wo wote kwa wale wenye kadi ya mfuko huo kimatibabu.
 
Hongera kwa kutenga muda wako kuandaa bandiko zuri namna hii, ila kuna vitu unachanganya kuhusu idadi ya kaya umetumia idadi ya watu…. kwa vile umesema NBS hawajatoa mchanganuo basi ni maoni yangu kuwa umetumia hizo figure kama mfano tu.

Naunga mkono hoja.
 
Idadi ya watu ni 61 million. Nimekadiria kaya moja kuwa na watu 4 kwa wastani, ndipo nikapata kaya hizo million 15 nilizotumia kwenye ukokotoaji. Natumaini umenielewa.
 
Hivi karibuni, Rais Samia Suluhu alisema serikali itapeleka mswaada wa Bima ya Afya bungeni ili uweze kujadiliwa. Wakati mchakato huo unaendelea Serikali kupitia Wizara ya Afya imependekeza viwango vya kulipia kwenye Bima.

Prof. Makubi amesema uchangiaji unaopendekezwa ni Sh. 340,000 kwa kaya ya watu 6 na Sh. 84,000 kwa mtu mmoja asiye na familia kwa mwaka.Kiwango hiki ukilinganisha na gharama za matibabu ni ndogo na serikali bado itafidia gharama nyingine.

My take: Mapendekezo hayo ya Prof Makubi ya wizara ya afya kama yatakekelezwa na kufanikiwa kwa asilimia 100%, yana maana kwamba wizara ya afya itakuwa inakusanya si chini ya shilingi trillion 5 kila mwaka kwenye mfuko huu kwa ajili ya kununua dawa na vifaa tiba. Hawasemi sasa hivi wanatumia shilingi ngapi kwa manunuzi haya ila tunachojua bajeti nzima ya wizara ya afya kwa sasa kwa mwaka haizidi shillingi trillion moja.
Hebu basi tujaribu kuwapa ushauri wa kisayansi based on facts katika jambo hili mhimu kwa afya za watanzania hasa wale kipato chao hakizdi dola moja au mbili kwa siku ambao ndiyo wengi. Wengi utakuta mtu kipato chake ni shilingi 150,000 kwa mwezi lakini ana mke na watoto wanne wanaomtegemea; hivyo jumla watu watano kila mmoja inakuwa shilingi 30,000 kwa mwezi au buku moja kwa siku.
 
Hii nchi sijui tunaweza kufanya nini kwa uweledi mkubwa. Tuna mipango mizuri sana tatizo lipo kwenye utekelezaji. Yangu macho.
 
Kwanza sijui Kama unafanya kazi sekta ya Afya ( public) au Hakuna.

Nioneshe chochote kizuri ambacho serikali ya Tanzania imewahi kufanikiwa halafu nitasupport hiyo UHC.

Tanzania tayari Kuna iCHF na NHIF nambie zimefikia wapi mpaka tuanze kufikiria UHC.

Nchi hii usitegemee Kama serikali itakuja kulipa mgawo wake kwenye shirika lolote Kama unavyopendekeza.

Mambo yote yanayohusu cost sharing yamekuwa yanapanda gharama kidogo kidogo baada ya Serikali kujitoa. Mifano: Vyuo vya kati, PSSF, NHIF, NSSF, na Sasa matibabu.

Sasa hivi vituo vya Afya vinategemea zaidi makusanyo yao wenyewe ( User fee) na Basket funds ( Wafadhili ).

NHIF inakaribia kufa.

Hicho kinachoitwa UHC lengo lake ni KUKUSANYA pesa ili wanusuru hiyo NHIF.

Na sababu kubwa za kufa huo mfuko Kwanza ni wao wenyewe kulipana POSHO kubwa hatari, kukopeshana, kutengeneza vifurushi vya mtu mmoja mmoja ( hata Kama ukiweka 2M kwa kichwa, akikata mtu anaueumwa tayari ) lazima akufirisi.

Kwahiyo tusubiri vilio na siasa.
 
Nakubaliana na wewe. Sasa unashauri kipi mkuu ili tuondokane na vilio hivyo? Kweli hakuna jinsi ya kukomesha adha, changamoto na vilio hivyo?
 
Nakubaliana na wewe. Sasa unashauri kipi mkuu ili tuondokane na vilio hivyo? Kweli hakuna jinsi ya kukomesha adha, changamoto na vilio hivyo?
Kwanza ni lazima fikra zibadilike.

Mashirika yawe sehemu ya uzalishaji na siyo nafasi za mapumziko kwa wateule wa Wanasiasa.

Mashirika yasipewe ruzuku, uendeshaji uendane na uzalishaji wao.

Mwisho kabisa ni lazima serikali iruhusu watu wafikirie na itafute majibu na solutions kitoka chini.

Pesa zinazokusanywa kwa Jambo fulani zifanye suala Hilo Hilo.
 
Hii nchi sijui tunaweza kufanya nini kwa uweledi mkubwa. Tuna mipango mizuri sana tatizo lipo kwenye utekelezaji. Yangu macho.
Mkuu mipango mizuri kwa mchango wa laki3.5 kwa kaya?
 
Back
Top Bottom