Ni kweli mfuko wa vijana ulio chini ya wizara ya habari vijana utamaduni na michezo unatoa mikopo kwa vijana japo no process ndefu kidogo maana inabidi kwanza muunde kikundi. Usiwe peke yako kisha muwe na usajiri kutoka wilayani kisha ndio mnaandika mradi wa kitu mnachotaka kufanya na kiasi mnachoomba,baada ya hapo sasa ndio mnajaza hiyo fomu ambayo inaviambatanisho vingi kama barua ya mtendaji,nalaka ya usajiri wa kikundi,cv ya kiongozi,na andiko la mradi husika kisha mnapeleka kwa afisa vijana wa wilaya yeye atawapa marks kisha atazipeleka mkoani kisha taifa ambapo kama mkionekana mnasifa. Hela inatumwa kwenye wilaya husika nyie mnaichukua wilayani kupitia tena kwenye saccoss ili kuwabana kwa hiyo marejesho mtafanya kupitia saccoss na ni ndani ya miaka miwili na riba ni asilimia 10