KERO Mfuko wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10% katika Wilaya ya Rungwe si rafiki

KERO Mfuko wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10% katika Wilaya ya Rungwe si rafiki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mfuko wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10% katika Wilaya ya Rungwe si rafiki na unatia wasiwasi kutokana na changamoto tunazokutana nazo katika kufuatilia fedha zetu.

Tulifanya maombi ya mkopo wa 10% na tukafuata taratibu zote zilizowekwa. Kikundi chetu kilipitishwa baada ya kuthibitishwa kuwa kimekidhi vigezo, na hata tuliitwa kwenye semina na kuhudhuria.

Baadaye tulitumwa ujumbe kwenye simu tukielekezwa kwenda benki kuchukua bank statement ili kuthibitisha kama fedha zimeingizwa kwenye akaunti. Tulipofika benki, tukaambiwa fedha hizo bado hazijawekwa kwenye akaunti.

Tuliporejea Halmashauri, tuliambiwa kuwa fedha tayari zimeruhusiwa na kuingizwa kwenye akaunti za vikundi. Hali hii imetufanya tuendelee kuhangaika kati ya benki na Halmashauri, huku kila upande ukituelekeza kwa mwingine na bila kupata majibu sahihi.

Tunaomba wahusika kutoa ufafanuzi wa wazi kuhusu fedha hizi na kuhakikisha vikundi vilivyokidhi vigezo vinapata mikopo yao kwa wakati.
 
Back
Top Bottom