Mpishimzoefu
New Member
- May 27, 2024
- 1
- 0
Watumishi wa Umma wamekuwa wakipitia changamoto za kifedha kwasababu ya kukosa kipato Cha ziada,Iwapo mifuko hii itaunganishwa changamoto hii inaweza kupungua.
Kwanza nianze na kueleza maana ya mifuko hii
1. NSSF Ni mfuko wa hifadhi ya jamii ambao unamsaidia mfanyakazi wa Umma au Taasisi binafsi kwa kumuwekea Hakiba yake ya badae
2. UTT AMIS Huu ni mifuko wa pamoja wa uwekezaji, ambao mwekezaji anaweka fedha zake na anapata faida
Umuhimu wa kuunganisha hii mifuko nikama ifuatavyo
Kwakuwa Nssf wanapokea michango ya wanachama na kutumia fedha zao bila riba au gawio,na kuzitumia hizo fedha kufanya miradi mbalimbali. ambayo inailetea faida Serikali ambapo wanachama hawapati ongezeko kutokana na fedha zao
kuzalishwa
Huku wao wakikabiliwa na Upungufu wa kipato,Kuunganishwa kwa mifuko hii kutawaidia watumi wa Umma Kuongeza kipato.
lLakini pia kupunguza Umaskini miongoni mwao, hasa tukizingatia Ufanisi wa mfuko wa UTT AMIS ambao Mtumishi wa Umma anaweza Kuchagua aina ya uwekezaji anaotaka kuufanya
kulingana na mfuko husika. Mfano Kuna mifuko inayotoa gawio na ile ya kukuza mtaji kwa uwekezaji wa muda mrefu na muda mfupi.
Sehemu pekee ya kupata hizo fedha kwaajiri ya uwekezaji huo ni Nssf Kwa maana kwamba dhana ya kuunganisha mifuko hii sio kumfanya Mtumishi atumie fedha zake za baadae, Ila
kufanya fedha yake anayokatwa imletee faida ambayo itamsaidia kufanya maendeleo yake mengine.
Pia tukumbukuke kuwa fedha za watumishi zinazowekwa kwenye mfuko wa Nssf ndizo hutumiwa na serikali Kama chanzo Cha mikopo hivyo Serikali hutumia pesa hizo bila wahusika kupata riba
Mfuko wa Hati Fungani
Huu mfuko unaweza kuwafaa Sana watumishi wa Umma, na kuwakomboa na mzigo wa Mikopo umiza na madeni. Mf,wakiweza kuunganishwa namfuko huu wanaweza kunufaika na gawio la kila mwezi ambapo kiwango Cha kuanza nachoni Tsh 10,000,000
Hivyo Serikali inaweza kuanzia hapo,Kwakuwaingiza Moja kwa Moja watumishi watakokuwa wametimiza kiasi hicho kwenye mfuko wa Nssf na kuwawekezea fedha hizo kwenye mfuko wa Hati Fungani wa Utt amis.
Lakini kuwaruhusi tu kuchukua faida ya kila mwezi Wala sio ule mtaji uliyowekezwa.
Na baadae kuwapa fursa zaidi kulingana na kiwango Cha fedha zao zoitakavyokuwa zinaongezeka kwenye mfuko wa Nssf
Kama vile kuwaunganisha kwenye mfuko wa Wekeza maisha ambao una faida zaidi kuliko huo nilioutaja hapo Juu.

Upvote
6