East
JF-Expert Member
- May 9, 2022
- 603
- 1,722
UTANGULIZI
Teknolojia ni moja ya tawi ambalo hutumia njia za kiufundi au kisayansi kutatua changamoto zituzungukazo katika mazingira yetu. Sekta ya sayansi na teknolojia imeleta mapinduzi makubwa sana ambayo imechochea sekta nyingine kukua, kwa mfamo uchuni na kilimo. Mifumo mbalimbali imeweza gunduliwa, mifumo hiyo ni Kama vile mifumo endeshi (Android, window, Linux na IOS) na programu ndogo ndogo pamoja na mitandao ya kijamii. Tukiangazia moja kwa moja katika mfumo bora wenye tija katika jamii, kifupi mfumo huu utaangazia changamoto tuzipatazo za kila siku hasa kwenye masuala ya ajira, biashara na kilimo. Tumeona na tunazidia kuona jinsi gani jamii inavyohangaika kwa kukosa mfumo bora utakao warahisishia kujua ni nini cha kufanya kwa mda huo.
Mifumo mingi iliyopo imetusaidia kwa kuwa weka watu katika Kijiji kimoja kupita mtandao , uwepo wa mitandao ya kijamii umewakutanisha watu katika kutatua changamoto zao na kuchochea mae deleo. Pia, umeweza kuona mifumo mbambali yenye kazi tofauti tofauti kama biashara, afya, kilimo na ajira. Lakini uwepo wa mifumo hio imeweza kukumbana na changamoto za kiteknolojia hasa upande wa ulinzi (udukuzi), upotoshaji wa taarifa za mhusika, wizi na utapeli. Kupitia mfumo huu utaweza kumrahisishia mtumiaji na kujenga uaminifu kwani suala la uhakiki wa data ni moja ya sifa kuu katika mfumo huu, wasiwasi wa mhusika utajuwa ni mdogo ukilinganisha na uaminifu.
Sifa za mfumo huu
Mfumo huu utaweza kusaidia jamii na lengo lake kuu ni kusogeza fursa kwa jamii, watu wataweza kusambazi kazi zao na fursa nyingine kupitia kazi au fursa hizo muhitaji ataweza julishwa mapema na kazi ikishapata mhusika basi wengine watataarifiwa kwa njia ya ujumbe. Na fursa hizo zitapatikana mda wowote kulingana na uhitaji wa mhusika au jamii. Sifa hizo ni Kama ifuatavyo :
1. Mfumo uwe na uwezo wa kutoa taarifa au ujumbe kwa mhusika muda wowote. Sifa hii ifanye kazi kwenye aina zote za simu na talakishi na ujumbe umfikia mtu kwa nama yeyote hata Kama hana kifurushi cha data.
2. Utambuzi wa mahali ni muhimu, hii ni kwa ajili ya kutambua sehemu alipo mhusika na kazi au fursa aitakayo. Kwa mfano kama mhusika kachagua kilimo au biashara basi akiwa eneo hilo mifumo utamjulisha haraka bila kuchelewa.
3. Mfumo utapaswa uunganishwe na mamlaka husika ili uweze kutatiliwa kuepusha uhalifu, baadhi ya uharifu huo unaweza kuwa kutoa taarifa za uongo, matumizi mabaya ya vifaa na hata kuiba taarifa za mtu mwingine turejee Cyber Crime Act 2015.
4. Mfumo uwe na utaratibu maalumu kwa ajili ya usajili wa mhusika katika mfumo huu kuepusha taarifa za uongo (akaunti moja kwa kila mtu).
5. Takwimu za uhitaji wa fursa au kazi ni mhimu ili mhitaji aweze kupanga bajeti na ni kipi afanye kuisaidia jamii. Kwa mfano mkoa x idadi kubwa ya watu wanna hitaji mahindi , hivyo mfanyabiashara itameaidia kupeleka kiwango husika bila kupata hasara.
6. Upande wa tenda au kazi mfumo unapaswa umuwezeshe mtoa tena au kazi kufatilia kazi yake inayofanywa na mfanya tenda au kazi hatua kwa hatua ili kujenga uaminifu.
Matokeo au matarajio ya mfumo huu kwa jamii.
Kwa mfumo huu tutegemee mafanikio mazuri kwa mtu mmoja mmoja na hata jamii nzima. Yafuatayo ni matokeo ambayo tunaweza kupata :
1. Kupunguza wimbi la utegemezi wa ajira. Mfumo utamsaidia mtu kutambua fursa na kazi zimzungukazo kutegemea na eneo husika.
2. Kuibua fursa ndogo ndogo, kwa mfano mtu kachugua kazi ya kufua au kumwagilia bustani hivyo akiwa katika harakati zake na akapita eneo ambalo kuna mtu anauhitaji wa mtu wa kufua au kumwagilia bustani basi mfumo utamtaarifu iwe kwa ujumbe wa kawaida au kutumia mtandao.
3. Itakuza pato la mtu mmoja mmoja kwani fursa zitakuwa nyingi kuliko kawaida. Kupitia kazi ndogo ndogo zituzungukazo mtumiaji ataweza kujipatia walau kiasi fulani cha pesa kupitia kazi atakayoipata kwenye mfumo huu.
4. Kupunguza kwa changamoto kama vile wizi, utapeli na taarifa za uongo kwani taasisi kama TCRA zitahusika.
5. Kuhamasisha watu kutafuta fursa na kujiajiri kupitia takwimu wazipatazo kwenye mfumo huu. Mahitaji ya wahusika yataweza kuoneshwa kwenye mfumo huu. Itachochea bidii na kujituma kupitia mfumo huu kupitia fursa zinazomfikia na kuziona.
6. Kupata taarifa sahihi na kwa wakati sahihi bila hofu, uwepo wa sifa ya ukusanyaji wa taarifa za eneo na mahitaji yake , itamsaidia mtumiaji kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi.
Changamoto za mfumo huu
Katika maisha hakuna kitu kikamilifu penye faida na kasoro zipo, moja ya changamoto katika mfumo huu ni ngumu kufuatilia namna kazi inavyoenda kwa mtu mwenye simu ya batani kwani suala la kufatilia mahali ni ngumu Sana. Mfumo utahitaji mtaji ili uweze kukamulika na kufanya kazi kama unavyotakiwa mda wote.
Itahitaji elimu kidogo ili kuelewa namna au jinsi ya kutumia mfumo huu ipasavyo bila kuvunja sheria. Pia suala la uaminifu kwa mara ya kwanza , ijapokuwa mfumo utakuwa na taarifa sahihi uaminufu wa mtu kwa mtu bado ni changamoto kubwa sana.
Hitimisho
Kulingana na changamoto tuzipatazo miongoni mwetu, kupitia mfumo huu utaweza kurahisisha maisha yetu hasa upande wa uchumi, biashara na hata kilimo. Jamii itaweza kushirikiana kwa namna tofauti tofauti kuhakikisha shughuli za kijamii, kiuchumi na hata kibiashara zinaenda vixuri. Kupitia uwepo wa data za kweli mhusika atakuwa na imani na kile anachokifanya na kutarajia matokeo chanya.

Upvote
129