SoC02 Mfumo bora utakaoisaidia jamii hasa kwenye suala la Ajira

SoC02 Mfumo bora utakaoisaidia jamii hasa kwenye suala la Ajira

Stories of Change - 2022 Competition

East

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2022
Posts
603
Reaction score
1,722
UTANGULIZI
Teknolojia ni moja ya tawi ambalo hutumia njia za kiufundi au kisayansi kutatua changamoto zituzungukazo katika mazingira yetu. Sekta ya sayansi na teknolojia imeleta mapinduzi makubwa sana ambayo imechochea sekta nyingine kukua, kwa mfamo uchuni na kilimo. Mifumo mbalimbali imeweza gunduliwa, mifumo hiyo ni Kama vile mifumo endeshi (Android, window, Linux na IOS) na programu ndogo ndogo pamoja na mitandao ya kijamii. Tukiangazia moja kwa moja katika mfumo bora wenye tija katika jamii, kifupi mfumo huu utaangazia changamoto tuzipatazo za kila siku hasa kwenye masuala ya ajira, biashara na kilimo. Tumeona na tunazidia kuona jinsi gani jamii inavyohangaika kwa kukosa mfumo bora utakao warahisishia kujua ni nini cha kufanya kwa mda huo.

Mifumo mingi iliyopo imetusaidia kwa kuwa weka watu katika Kijiji kimoja kupita mtandao , uwepo wa mitandao ya kijamii umewakutanisha watu katika kutatua changamoto zao na kuchochea mae deleo. Pia, umeweza kuona mifumo mbambali yenye kazi tofauti tofauti kama biashara, afya, kilimo na ajira. Lakini uwepo wa mifumo hio imeweza kukumbana na changamoto za kiteknolojia hasa upande wa ulinzi (udukuzi), upotoshaji wa taarifa za mhusika, wizi na utapeli. Kupitia mfumo huu utaweza kumrahisishia mtumiaji na kujenga uaminifu kwani suala la uhakiki wa data ni moja ya sifa kuu katika mfumo huu, wasiwasi wa mhusika utajuwa ni mdogo ukilinganisha na uaminifu.

Sifa za mfumo huu
Mfumo huu utaweza kusaidia jamii na lengo lake kuu ni kusogeza fursa kwa jamii, watu wataweza kusambazi kazi zao na fursa nyingine kupitia kazi au fursa hizo muhitaji ataweza julishwa mapema na kazi ikishapata mhusika basi wengine watataarifiwa kwa njia ya ujumbe. Na fursa hizo zitapatikana mda wowote kulingana na uhitaji wa mhusika au jamii. Sifa hizo ni Kama ifuatavyo :

1. Mfumo uwe na uwezo wa kutoa taarifa au ujumbe kwa mhusika muda wowote. Sifa hii ifanye kazi kwenye aina zote za simu na talakishi na ujumbe umfikia mtu kwa nama yeyote hata Kama hana kifurushi cha data.

2. Utambuzi wa mahali ni muhimu, hii ni kwa ajili ya kutambua sehemu alipo mhusika na kazi au fursa aitakayo. Kwa mfano kama mhusika kachagua kilimo au biashara basi akiwa eneo hilo mifumo utamjulisha haraka bila kuchelewa.

3. Mfumo utapaswa uunganishwe na mamlaka husika ili uweze kutatiliwa kuepusha uhalifu, baadhi ya uharifu huo unaweza kuwa kutoa taarifa za uongo, matumizi mabaya ya vifaa na hata kuiba taarifa za mtu mwingine turejee Cyber Crime Act 2015.

4. Mfumo uwe na utaratibu maalumu kwa ajili ya usajili wa mhusika katika mfumo huu kuepusha taarifa za uongo (akaunti moja kwa kila mtu).

5. Takwimu za uhitaji wa fursa au kazi ni mhimu ili mhitaji aweze kupanga bajeti na ni kipi afanye kuisaidia jamii. Kwa mfano mkoa x idadi kubwa ya watu wanna hitaji mahindi , hivyo mfanyabiashara itameaidia kupeleka kiwango husika bila kupata hasara.

6. Upande wa tenda au kazi mfumo unapaswa umuwezeshe mtoa tena au kazi kufatilia kazi yake inayofanywa na mfanya tenda au kazi hatua kwa hatua ili kujenga uaminifu.

Matokeo au matarajio ya mfumo huu kwa jamii.
Kwa mfumo huu tutegemee mafanikio mazuri kwa mtu mmoja mmoja na hata jamii nzima. Yafuatayo ni matokeo ambayo tunaweza kupata :

1. Kupunguza wimbi la utegemezi wa ajira. Mfumo utamsaidia mtu kutambua fursa na kazi zimzungukazo kutegemea na eneo husika.

2. Kuibua fursa ndogo ndogo, kwa mfano mtu kachugua kazi ya kufua au kumwagilia bustani hivyo akiwa katika harakati zake na akapita eneo ambalo kuna mtu anauhitaji wa mtu wa kufua au kumwagilia bustani basi mfumo utamtaarifu iwe kwa ujumbe wa kawaida au kutumia mtandao.

3. Itakuza pato la mtu mmoja mmoja kwani fursa zitakuwa nyingi kuliko kawaida. Kupitia kazi ndogo ndogo zituzungukazo mtumiaji ataweza kujipatia walau kiasi fulani cha pesa kupitia kazi atakayoipata kwenye mfumo huu.

4. Kupunguza kwa changamoto kama vile wizi, utapeli na taarifa za uongo kwani taasisi kama TCRA zitahusika.

5. Kuhamasisha watu kutafuta fursa na kujiajiri kupitia takwimu wazipatazo kwenye mfumo huu. Mahitaji ya wahusika yataweza kuoneshwa kwenye mfumo huu. Itachochea bidii na kujituma kupitia mfumo huu kupitia fursa zinazomfikia na kuziona.

6. Kupata taarifa sahihi na kwa wakati sahihi bila hofu, uwepo wa sifa ya ukusanyaji wa taarifa za eneo na mahitaji yake , itamsaidia mtumiaji kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi.

Changamoto za mfumo huu
Katika maisha hakuna kitu kikamilifu penye faida na kasoro zipo, moja ya changamoto katika mfumo huu ni ngumu kufuatilia namna kazi inavyoenda kwa mtu mwenye simu ya batani kwani suala la kufatilia mahali ni ngumu Sana. Mfumo utahitaji mtaji ili uweze kukamulika na kufanya kazi kama unavyotakiwa mda wote.

Itahitaji elimu kidogo ili kuelewa namna au jinsi ya kutumia mfumo huu ipasavyo bila kuvunja sheria. Pia suala la uaminifu kwa mara ya kwanza , ijapokuwa mfumo utakuwa na taarifa sahihi uaminufu wa mtu kwa mtu bado ni changamoto kubwa sana.

Hitimisho
Kulingana na changamoto tuzipatazo miongoni mwetu, kupitia mfumo huu utaweza kurahisisha maisha yetu hasa upande wa uchumi, biashara na hata kilimo. Jamii itaweza kushirikiana kwa namna tofauti tofauti kuhakikisha shughuli za kijamii, kiuchumi na hata kibiashara zinaenda vixuri. Kupitia uwepo wa data za kweli mhusika atakuwa na imani na kile anachokifanya na kutarajia matokeo chanya.
 
Upvote 129
IDEAS ZA KUTOKA KIMAISHA KWA MTAJI MDOGO

1.Nunua pikipiki ya Dhamana ukaanza biashara ya Boda boda.
2.Fungua saluni
3.Mradi wa tofali za kuchoma
3.Fuga kuku
4.Somea ujuzi wowote
5.Mradi wa kushona nguo
6.kijiwe cha kuchomelea
7.kijiwe cha milango na madirisha ya aluminum
8.Mgahawa Mdogo
9.Kijjwe cha kahawa
10.Mashine ya kupukuchua mazao mfano mahindi, mpunga, mtama, karanga, nk
11.Mashine ya kukata nyasi, kupalilia
12.Kuuza mbuzi, kuku,
13.Biashara ya mazao.
14.kukodi bus, daladala na kuzisimamia upate cha juu
15.Kutengeneza sabuni, sanitizer, handwash,
16.Kutengeneza unga wa lishe
17.Kilimo cha umwagailiaji water pump, mbegu, madawa
18.Jiko la supu
19.kutengeneza mkaa mbadala
20.Kuuza chips
21.Kukaanga kuku
22.Kutengeneza vitafunio
23.Kuzalisha ethanol
24.kufuga poko mbuzi katoliki
25.Kufungua kilabu cha pombe za kienyeji
26.Kufungua vijiwe vya Kukusanya ubuyu maporini yakitimia magunia unaleta mjini
27.Kuuza juice
28.Kuuza juice ya miwa
29.Kijiwe cha kukaanga samaki jioni
30.Shughuli za upambaji kumbi
31.Kusambaza bidhaa majumbani
32.Kusambaza bidhaa basic needs kwenye maduka ya vijijini yaani unanua mjini unasambaza kwa oda viduka vya vijijini.
33.Kuzunguka minadani kuuza nguo za mitumba, vyombo, nk
34.Kufungua tuition center
35.Kufungua grocery
36.Kuwa wakala wa bidhaa za viwandani
37.kijiwe cha kukusanya taka za plastic, chuma,oil chafu na tairi chakavu.
38.Kufungua genge la kuuza basic home need
39.Kufungua ofisi ya kupiga nguo pasi.
40.Ofisi ya kutengeneza viatu na mabegi
41.Kutengeneza vyombo vya kupikia mfano, majiko, ndoo, sufuria, mifuniko, vikaangio, nk
42.Saluni ya kutengeneza kucha za wanawake
43......Jengea vyumba vitatu wazazi wako nyumba ya Bati upate baraka
44..Nunua shamba
45.Nunua ng'ombe wadogo watano kwa laki na nusu anza ufugaji.
Au nunua mbuzi anza kufuga
46.Fungua kijiwe cha kuonyesha mpira
47.duka la nguo za kupoint classic za mitumba piga pasi tundika kwenye enga
48..Ofisi za baiskeli za kukodi hapo unapata baiskeli nane
49..Duka la spea za pikipiki na baiskeli
50.Duka la dawa na vipodozi
51..ofisi ya kuchaji simu kwa sola vijijini
52..ofisi ya uwakala wa kutuma na kutoa pesa
53.. Bustani za kuzalisha miche ya miti na matunda
54... Ufugaji nyuki na kuuza asali
55.. Kuzalisha unga wa muhogo
56..Direct sale yaani door to door delivery hapa unakuwa na torori na speaker unapita KILA nyumba unauza bidhaa na kuchukua oda ya nini wanataka Ili kesho uwaletee.
57.Utengenezaji pellets chakula cha mifugo,samaki.
58..unga wa lishe
59..mikeka
60.bidhaa za mianzi.
61.wine,
62.usafi wa majumbani
63.kuuza uji wa ulezi,mchele
64.utengenezaji mbolea za mboji na za maji.
65.utengenezaji wa vigae vya cement na vya udongo.
66.kupanda miti kwa ajili ya nguzo na mirunda
67.utengenezaji wa ndala
68.utengenezaji viatu
69.Upondaji kokoto
70.ufundi simu na radio
71
 
Sinah maana nchi niliopo tunadepend kwa developed countries
Sawa.
Hii itasaidia mtu kujua au kupata kazi ndogo ndogo ndani ya eneo husika na hata nje ya eneo. Kuna kazi nyingi tu kwenye jamii zetu ambazo muda mwingine wa naitaji kuisaidiwa. Utapataje mtu? Utajuaje Kuna kazi mahali fulani?.
Kwa kutengeneza kitu kama nilichotoa kitakuwa na uwezo wa kumjulisha mtu kuhusu kazi anayotaka mfano mtu anatafuta kazi za kufua, kumwagilia bustani na hata mafundi. Hivyo atapata taarifa kwa kujulishwa kuwa kazi anayotaka imepatikana.
Pia kuwepo kwa sifa ya kutambua kazi zilizopo itasaidia kwa wale wanaotaka kazi yoyote (itakuwa inafanya kazi kama wi-fi au bluetooth).
Nimeeleweka hii I naweza kuwa kama tovuti, apps au program ya kompyuta nalo litushinde wakati watu wapo IT, co/outer science hadi wahandisi WA kompyuta.
 
IDEAS ZA KUTOKA KIMAISHA KWA MTAJI MDOGO

1.Nunua pikipiki ya Dhamana ukaanza biashara ya Boda boda.
2.Fungua saluni
3.Mradi wa tofali za kuchoma
3.Fuga kuku
4.Somea ujuzi wowote
5.Mradi wa kushona nguo
6.kijiwe cha kuchomelea
7.kijiwe cha milango na madirisha ya aluminum
8.Mgahawa Mdogo
9.Kijjwe cha kahawa
10.Mashine ya kupukuchua mazao mfano mahindi, mpunga, mtama, karanga, nk
11.Mashine ya kukata nyasi, kupalilia
12.Kuuza mbuzi, kuku,
13.Biashara ya mazao.
14.kukodi bus, daladala na kuzisimamia upate cha juu
15.Kutengeneza sabuni, sanitizer, handwash,
16.Kutengeneza unga wa lishe
17.Kilimo cha umwagailiaji water pump, mbegu, madawa
18.Jiko la supu
19.kutengeneza mkaa mbadala
20.Kuuza chips
21.Kukaanga kuku
22.Kutengeneza vitafunio
23.Kuzalisha ethanol
24.kufuga poko mbuzi katoliki
25.Kufungua kilabu cha pombe za kienyeji
26.Kufungua vijiwe vya Kukusanya ubuyu maporini yakitimia magunia unaleta mjini
27.Kuuza juice
28.Kuuza juice ya miwa
29.Kijiwe cha kukaanga samaki jioni
30.Shughuli za upambaji kumbi
31.Kusambaza bidhaa majumbani
32.Kusambaza bidhaa basic needs kwenye maduka ya vijijini yaani unanua mjini unasambaza kwa oda viduka vya vijijini.
33.Kuzunguka minadani kuuza nguo za mitumba, vyombo, nk
34.Kufungua tuition center
35.Kufungua grocery
36.Kuwa wakala wa bidhaa za viwandani
37.kijiwe cha kukusanya taka za plastic, chuma,oil chafu na tairi chakavu.
38.Kufungua genge la kuuza basic home need
39.Kufungua ofisi ya kupiga nguo pasi.
40.Ofisi ya kutengeneza viatu na mabegi
41.Kutengeneza vyombo vya kupikia mfano, majiko, ndoo, sufuria, mifuniko, vikaangio, nk
42.Saluni ya kutengeneza kucha za wanawake
43......Jengea vyumba vitatu wazazi wako nyumba ya Bati upate baraka
44..Nunua shamba
45.Nunua ng'ombe wadogo watano kwa laki na nusu anza ufugaji.
Au nunua mbuzi anza kufuga
46.Fungua kijiwe cha kuonyesha mpira
47.duka la nguo za kupoint classic za mitumba piga pasi tundika kwenye enga
48..Ofisi za baiskeli za kukodi hapo unapata baiskeli nane
49..Duka la spea za pikipiki na baiskeli
50.Duka la dawa na vipodozi
51..ofisi ya kuchaji simu kwa sola vijijini
52..ofisi ya uwakala wa kutuma na kutoa pesa
53.. Bustani za kuzalisha miche ya miti na matunda
54... Ufugaji nyuki na kuuza asali
55.. Kuzalisha unga wa muhogo
56..Direct sale yaani door to door delivery hapa unakuwa na torori na speaker unapita KILA nyumba unauza bidhaa na kuchukua oda ya nini wanataka Ili kesho uwaletee.
57.Utengenezaji pellets chakula cha mifugo,samaki.
58..unga wa lishe
59..mikeka
60.bidhaa za mianzi.
61.wine,
62.usafi wa majumbani
63.kuuza uji wa ulezi,mchele
64.utengenezaji mbolea za mboji na za maji.
65.utengenezaji wa vigae vya cement na vya udongo.
66.kupanda miti kwa ajili ya nguzo na mirunda
67.utengenezaji wa ndala
68.utengenezaji viatu
69.Upondaji kokoto
70.ufundi simu na radio
71
tutajuaje kama unafanya kitu fulani ndani ya jamii kama sio uanze kuzunguka kutangaza? mfano Hao Hao wenye ujuzi kama mafundi vibarua wanapataje
Vipi kuhusu wale ambao Hawa a ujuzi wowote wenyewe ni kazi kazi? Si itawasaidia kupata taarifa na kazi nyingi kwa uharaka.
Kifupi mimi nimejikita kwenye Kupunguza wimbi la ukosefu WA ajira. Kuna watu wamesoma hadi elimu ya juu ila wanafanya kazi ndogo ndogo.
Unaweza pata ajira ukatoka kimaisha na kinyume chake.
Nimeeleweka
 
Hata kikubwa kilianza na kidogo kidogo,
 
Karubuni katika mada hii
 
Ni kweli ajira ni changamoto kubwa

Nakukaribisha pia kusoma makala yangu na kutoa mawazo yako.

[emoji116]

Na

na

Asante
Sawa
 
Back
Top Bottom