SoC01 Mfumo bora wa Uongozi unahitajika Afrika

SoC01 Mfumo bora wa Uongozi unahitajika Afrika

Stories of Change - 2021 Competition

Theb

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
3,927
Reaction score
7,276
Habari zenu..?
Andiko hili litatoa mwanga kwa uchache kama sio wingi jinsi gani nchi za bara la Afrika zinavyoweza kuwa na uongozi bora kwa maendeleo ya jamii.

Andiko hili litagawanyika katika sehemu kuu nne. Kwanza, nitatoa maana na mifano iliyoelezewa na wana falsafa katika kuelezea uongozi bora. Pili, nitatoa sifa za uongozi bora. Tatu, kipi kifanyike ili kuwa na viongozi bora. Nne, hapa itakua hitimisho. Nitatoa mawazo au maoni yangu juu ya uongozi bora katika kuyafikia maendeleo bora ya jamii.

Uongozi ni kusimamia, kuweza kutatua au kuzikabili changamoto zinazokusibu na kupata suluhisho hapa ni kwa ngazi ya mtu binafsi. Uongozi katika ngazi ya taifa au jamii, ni hali ya kuweza kusimamia haki, malengo, mawasiliano na kuwezesha jamii kuishi kwa kuelewana na kushirikiana katika kuindeleza jamii.
Mfano wa viongozi walioweza kuwa unganisha watu

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ni mfano wa kiongozi bora aliye weza kuwaunganisha watu wa taifa letu la Tanzania na hata alisaidia nchi zingine katika kupigania uhuru

SIFA ZA KIONGOZI BORA ZILIZO TOLEWA NA MWALIMU NYERERE

1. Kiongozi lazima awe chaguo la watu. Kiongozi anayefaa kwa taifa lolote lazima awe ni chaguo la hao watu wa taifa husika. Ndio maana Mwalimu Nyerere aliruhusu uchaguzi wa kupiga kura japo alikua katika serikali ya kijamaa

2. Kiongozi bora hapaswi kuwa mkabila, mdini wala mkanda.
Kiongozi atakaye watambua watu wa taifa lake kwa ukabila wao huyo hafai.

"nilikutana na mama mmoja akaniambia alikua akifanya kazi jumuiya ya afrika mashariki, na sisi watu wa uganda tulikua tunajuana kwa makabila yetu , watu wa kenya walikua wakijuana kwa makabila yao, huyu mkikuyu, huyu mluhya. Lakini sisi watanzania hatujui makabila ya watu, nikawambia mama ni wakati huo, sasa hivi watanzania wanataka kujua makabila yao, ya nini, mnataka kutambika? Majirani zetu waalikua wanaiga kutoka Tanzania, sasa bila haya na sisi tunataka kuulizana makabila? Mwalimu Nyerere katika hotuba yake ya mkutano mkuu wa CCM 1995".

3.Kiongozi bora lazima awe muadilifu.
Kiongozi aliye bora hapaswi kutotambua misingi ya kuongoza bali anapaswa kuwa bora katika maadili ya uongozi. Hapaswi kuwa mla rushwa mbadhilifu na muongo muongo.

4. Kiongozi bora lazima awe na maono.
Hapa nitaonesha jinsi Mwl Nyerere alivyokuwa na maono na imani katika kutambua maadui wakuu wa taifa letu ambao ni ujinga umasikini na maradhi

"nchi hii ni bado ya wakulima na wafanyakazi, hatuwezi kuwa nchi ya watu wenye kudai na kudai, nawaomba ndugu zangu watanzania hatujalemaa sana, lakini kilema kipo, viongozi wetu wanadai na kudai tuu, watu ni maskini, wachache hao wana nguvu ya kuongoza nchi hii ndio wanaodai tuu'' Nyerere" chanzo bbc.
_109226990_100915131059_julius_nyerere_512x288_nocredit-1.jpg


5. Kiongozi bora lazima awe mwenye subira, mtulivu na mwenye kufuata sheria kulingana na katiba ya nchi.
Hizo ni baadhi ya sifa za kiongozi bora kuingana na mawazo ya Mwl Nyerere.

6. Kiongozi bora hutekeleza mipango na sera za kimaendeleo ya nchi kwa uwazi. Kama kiongozi hata kuwa muwazi katika kutekeleza sera na mipango ya nchi huyo hana sifa ya kuwa kiongozi bora.

Mwl Nyerere alitupatia ufahamu juu ya uongozi bora kama nilivyotoa baadhi ya sifa za kiongozi bora sasa kivipi tutafikia hatua ya kuwa na viongozi bora. Tutalata viongozi bora kwa maendeleo ya taifa letu ikiwa tutakuwa na demokrasia iliyomithilika.

SIFA ZA SERIKALI YA DEMOKRASIA AMBAZO ZILIELEZWA NA MWALIMU JULIUS NYERERE. Hizi ni chachu ya maendeleo katika taifa.

1. Uwepo wa uchaguzi wa huru na wa haki. Ili demokrasia yetu iwe thabiti je tuna uchaguzi wa huru na haki..? Uchaguxi ili uwe wa huru na haki lazima tuwe na tume huru ya uchaguzi. Tume isiyo jengwa na watu wa chama kimoja.

2. Lazima kuwe na mfumo wa vyama vingi na vishiriki katika chaguzi zote nchini. Ili taifa liwe na demokrasia iliyo na faida kwa maendeleo lazima kuwa na vyama vyingi vinavyoshiriki chaguzi na kutupatia viongozi watakao chaguliwa na wananchi kulitia tume huru ya uchaguzi.

3. Lazima serikali iwa husu watu. Lazima serikali ya kidemokrasia iwe inatokana na maamuzi ya wananchi wa taifa letu. Mwl Nyerere anasema "Ili kupata maendeleo ya kweli, watu lazima wahusishwe,

"Ili kupata maendeleo ya kweli, watu lazima wahusishwe1974".
Mwalimu anasiaitiza ilikupata maendeleo ya kweli watu wahusishe kuwa chagua viongozi wao. Je, taifa letu hili hii inatekelezwa kwa ufasaha..?

4. Lazima kuwe na uwazi katika kutekeleza mipango ya serikali.
Mwl Nyerere alisema.
"Hatuwezi kuwa na matumaini ya kutatua matatizo yetu kwa kujifanya kuwa hayapo". Lazima tuwe wawazi ndipo tutayatatua matatizo yetu.

5. Lazima tukosoane maana ndio njia ya kupeana mawazo na fikra tofauti. Hapo napo mwalimu alisema kuhusiana na hili la kukosoana alisema,
"Itakuwa yote ni makosa , na si jambo la muhimu , kuhisi kuwa lazima tusubiri hadi viongozi wafe ndio tuanze kuwakosoa " JK Nyerere.

6. Demokrasia inakua kulingana na nyakati. Hapa ndio maana katika mataifa ya kidemokrasia katiba zinafanyiwa maboreshi ili kuendana na muda na jamii au nyakati husika. Mwalimu alisema,
"Demokrasi sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuiagiza. Demokrasi inapaswa kuendelezwa kulingana na nchi yenyewe ". Juni 1991 mjini Rio De Janeiro, Brazil.

Mwalimu Nyerere aliku kiongozi bora aliekuwa na maono juu ya jamii zetu za Afrika ndio maana tunaona mawazo yake yanaishi.

Hitimisho
Taifa letu linayo kila sababu ya kufuata sifa alizozitoa Mwl Nyerere katika kuelezea kwake kuhusu kiongozi bora na demokrasia pia.

Mwisho kabsa uongozi ndio unaogusa moja kwa moja shughuli za maendeleo ya jamii hivyo haya yaangaliwe kwa umakini.

_109226990_100915131059_julius_nyerere_512x288_nocredit-1.jpg
 
Upvote 3
Msome na hapa wakuu[emoji1317][emoji1303]
 
Mwalimu alikua kiongozi bora tumuige na kujifunza kwake
 
Maendeleo kuyapata ni yule anayewaongoza awe kiongozi bora, na mwajibikaji na mzalendo.
 
Maendeleo kuyapata ni yule anayewaongoza awe kiongozi bora, na mwajibikaji na mzalendo.
Ndio. Viongozi bora watakao kuwa tayari kwa ajili ya kubadilisha mapungufu yoyote yanayoonekana na kukubali mawazo ya wengi na kutambua kipi kifanyike kwa wakati sahihi ni dhahiri atalisaidia taifa kuendelea mkuu usisahau na kura yako[emoji1317][emoji1317][emoji1303]
 
Tuzidi kulisoma andiko letu hili na kura tulipigieni[emoji1317][emoji1317]
 
Kuwa kiongozi bora siyo kigezo.. inahitaji kiongozi aende na wakati, awe mbunifu wa kujenga miundombinu ya kisasa ...
 
Kuwa kiongozi bora siyo kigezo.. inahitaji kiongozi aende na wakati, awe mbunifu wa kujenga miundombinu ya kisasa ...
Hakika kiongozi lazima akubali mabadiliko ya nyakati. Tena yanayoendana na teknolojia inayokua kila wakati. Kuna viongozi wasiotaka mabadiliko hawa hawafai maana future inajengwa na mabadililo yenye ubora. Ukiona kiongozi anakataa uboreshwaji wa mambo ya kimhimili ya utawala muogope au Afrika tunaoviongozi wengi wanao kumbatia udikteta wasiopenda demokrasia ya kweli hawa hawafai.

Usisahau kura yako mdau wangu wa nguvu.
 
[emoji1317][emoji1317][emoji1317]
 
Back
Top Bottom