Mafanikio ya binadamu yeyote hutegemea namma anavyotumia maarifa katika kuyaendea yale anayoyaamini na kuyatamani. Wakati maarifa ni zao la teknolojia iliyopo, maono hutokana na mitazamo na uelekeo wa fikra za Imani za dini, falsafa na itikadi. Ndio kusema teknolojia na maono ndio msingi wa mafanikio ya binadamu.
Kwa kuwa binadamu haishi pekee, bali ndani ya jamii, fikra za kiitikadi ndio huwa miongozo ya taratibu za maisha ya watu katika tofauti zao.
Katika jamii zinazotawaliwa na mawazo ya walio wengi, watu huongozwa na itikadi kupitia vyama vya kisiasa. Kwa njia ya Chaguzi huru, watu hupata fursa ya kuchagua fikra wanazoziona zinawafaa zaidi. Kila chama cha kisiasa huwa na fikra na mitazamo tofauti. Lengo ni kuweka mazingira huru zaidi katika kuchagua Miongozo na Uongozi Ili kufikia malengo ya matamanio na matarajio kama jamii.
Jukumu kubwa la itikadi hizi za kisiasa ni kuratibu maono ya jamii. Vilevile kuratibu upatikanaji na kusimamia matumizi sahihi ya teknolojia, fursa na rasilimali za jamii kupitia Ilani za Chaguzi.
Hata hivyo, Ili teknolojia iweze kuleta matokeo chanya kwa jamii husika, mambo makuu manne sharti yazingatiwe katika taratibu za kila siku kwenye jamii.
Jambo la kwanza ni tamko la kimamlaka linalobainisha aina ya mabadiliko, kiwango cha mabadiliko, walengwa wa mabadiliko, muda wa kuyafikia pamoja na mipango na rasilimali za utekelezaji. Kwa maneno mengine ni uwepo wa Sera za mabadiliko.
Jambo la pili ni kuwepo kwa hamasa kwa jamii juu ya mabadiliko na mipango ya mabadiliko hayo. Lengo ni kutengeneza utayari wa jamii kwa nia ya kupata ushirikiano.
Jambo la tatu ni uwezeshaji wa kimfumo na kitaasisi kujenga mazingira wezeshi ya utekelezaji mipango ya sera.
Jambo la nne ni kuwepo kwa ushirikishaji jamii katika utekelezaji wa mipango ya mabadiliko iliyoainishwa ndani ya sera.
Tanzania kama jamii tulipitia mabadiliko ya sera za kiuchumi miaka ya 80 na 90.
Mabadiliko hayo yalikuwa kuachana na sera za uchumi wa kijamaa kuelekea uchumi wa soko huria. Katika mabadiliko hayo shughuli za kibiashara kama mabenki na makampuni ya umma yalibinafsishwa ili kuingiza mitaji na teknolojia.
Kukua kwa sekta ya fedha kama benki ya kijamii SACCOS kulileta fursa mpya na nafuu ya upatikanaji mitaji kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ambao masharti ya mabenki yaliwaweka kando.
Mabadiliko haya yalileta hamasa kwa vijana kuachana na shughuli za kilimo cha kujikimu na kuhamia mijini kujikita na shughuli za biashara ndogondogo.
Kufuatia hamasa hiyo, serikali ya awamu ya tatu ilianzisha MKURABITA, mfumo wa kuwatambua rasmi wafanyabiashara hao wadogo wadogo.
Mfumo huu ulishika Kasi kipindi cha awamu ya nne ya uongozi (2005 - 2015). Kupitia MKURABITA wakala wa usajili makampuni na biashara BRELA pamoja na wakala wa hakimiliki Tanzania COSOTA zilianzishwa. Taasisi hizi za kimfumo zinatoa hati za umiliki kisheria. Hati hizo ziliwawezesha wafanyabiashara hawa kuingia mikataba ya kibiashara na kufanya shughuli zao chini ya ulinzi wa kisheria.
Kufuatia hatua hii, mafanikio makubwa yameonekana katika sekta ya Sanaa hasa filamu, muziki na matangazo. Wasanii vijana wameweza kupiga hatua kubwa katika sanaa na uchumi kitaifa na kimataifa ambapo wanamuziki na wasanii vijana wameweza kupiga hatua kubwa kiuchumi kutokana na uwepo wa hati miliki pamoja na mitandao ya kijamii.
Kukamilika kwa shughuli za urasmishaji sekta ya biashara nchini kumetoa fursa kwa serikali ya awamu ya sita (2021+) chini ya Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluh Hassan, kuanza fursa mpya katika sekta ya kilimo. Kupitia ajenda 1030, shughuli za kilimo zimefungamanishwa na shughuli za biashara na Kuondoa mazoea ya kilimo cha kubahatisha.
Kupitia mpango wa "Kilimo ni Biashara" serikali imeimarisha taasisi za utafiti wa mbegu nchini kuweza kufanya utafiti wa mbegu kulingana na soko. Serikali kupitia bajeti ya mwaka 2022/2023 imeweka ruzuku ya mbolea Ili kushusha bei na kuwezesha upatikanaji wa mbolea kwa gharama nafuu.
Serikali pia imeanzisha mpango wa kusajili wakulima wote nchini. Lengo ni kuweza kuwa na takwimu halisi kwa lengo la kuweza kupanga kwa uhakika mipango na bajeti ya kilimo nchini. Lakini pia kuweza kufanya ufuatiliaji wa maendeleo na changamoto kwa nia ya kuzitatua.
Pia serikali kwa kushirikisha sekta binafsi kama taasisi za fedha na makampuni ya biashara za mazao, wameanzisha mpango wa vitalu kwa ajili ya kuwezesha "kilimo ni biashara" hususani kwa vijana. Lengo ni kuhamasisha nguvu kazi ya vijana kujikita zaidi katika shughuli zenye tija Ili kuinua hali zao kiuchumi sambamba na uchumi wa taifa.
USHAURI:
Kwa kuwa serikali imeamua kuwekeza teknolojia katika kilimo kwa ajili ya kutengeneza fursa za ajira na kuboresha hali za watanzania wengi, nashauri mambo yafuatayo yaendelee kufanyika.
Kuimarisha mfumo wa umwagiliaji kwa kuweka ruzuku kwenye vifaa vya umwagiliaji pamoja na uchimbaji visima. Lengo ni kuwezesha wakulima wengi wa hali ya chini kuweza kumudu teknolojia hii.
Pili ni kwa fursa za kilimo biashara. Nashauri kuwepo utaratibu wa kielektroniki wa kushirikisha walengwa wa miradi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi. Katika utaratibu huo, ianzishwe tovuti ya kilimo ni biashara ambayo itakuwa na taarifa mbalimbali za miradi ilipo pamoja na masharti yake. Mfumo pia uwe na dirisha la usajili Ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi Ili kuweza kuwa mmoja wa washiriki.
Hali hii itasaidia Kupunguza vitendo vya rushwa na upendeleo katika kugawa fursa hizi kwa walengwa.
Mwisho, Serikali kwa kushirikiana na taasisi za fedha kuwa na program za mashamba vitalu kwa ajili ya kuendesha kilimo biashara kila Kijiji kwa ajili ya kutoa mikopo ya kilimo hususani kwa vijana wanaoingia katika soko la ajira. Lengo ikiwa ni kupanua wigo wa ajira zenye tija na kuimarisha sekta ya kilimo nchini.

Upvote
0