Mfumo jike katika familia ni ushetani

Mfumo jike katika familia ni ushetani

ARGAN MARA

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2016
Posts
1,020
Reaction score
2,716
Tangu dhambi ilipoingizwa na mwanamke duniani, Mungu aliamuru mfume dume ktk familia. Soma { Mwa 3:16 akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako na kuzaa kwako kwa uchungu utazaa watoto na tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala}

Siungi mkono wanaume kuwatesa na kuwanyanyasa wake zao, maana hiyo siyo maana ya kutawala. Lakini naitaji wanawake wajue kuwa wao wanapaswa kuwa chini ya mamlaka ya waume zao.

Cheo Cha mke, fedha, umaarufu, vipaji, karama, nk; havimfanyi mke kuwa mtawala wa familia.

Ukweli ni kuwa mwanamke wa kisasa anaweza kuwa na elimu kubwa, fedha, cheo, maarufu, star ,kuliko mume wake. Lakini hayo bado hayampi mke mamlaka ya kumtawala mume na familia.

Wanawake wapumbavu pekee wanaharibu sana familia na kukataa mamlaka ya waume zao, Ukweli ni kuwa mke asiyetaka kuwa chini ya mamlaka ya mume wake kwa sababu yoyote ile, lazima ataishia kuwa msimbe.Kwa sababu anakiuka kwa makusudi utaratibu wa Mungu aliyouweka kuhusu familia.

Wale wanawake vichwa ngumu mnaodai haki sawa, mna upako wa kisimbe na mtaishia kuwa wasimbe waelevu. Mke wa mtu ukitaka ndoa yako idumu fuata agizo alilolisema Mungu, hata kama una elimu zaidi, cheo, fedha, karama, vipaji kuliko mume wako.

Mwenyezi Mungu ajasema wanawake waache utii na kuwa na viburi kwa waume zao, kisa wana vitu hivyo kuliko waume zao. Ukikaidi haya lazima ndoa yako itakuwa ya hovyo na itavunjika tu.
 
Kwanza hili neno msimbe ni kiswalihi fasaha au ni moja ya neno la kikabila

Msimbe maana yake ni mwanamke alieolewa kisha akaachika na hili neno mm nimekuja kulijua usukumani .

Ktk jamii ya kitanzania wanawake wa kisukuma wale waliopo ndani ya mila na destuli binafsi naona wanaonewa sana au kunyanyasika.

Mwanamke wa kisukuma anaenda kusenya kuni,(kukata kuni ) tololi zima na sio moja ni zaidi ya mawili, wanaswaga ng'ombe kurudisha kuni kutoka msituni mwanamke wa kisukuma haruhusiwi kuhoji matumizi yeyote ya mali nyumbani kama mahindi,mpunga, ng'ombe nk. Mwanamke wa kisukuma hauruhusiwi kuleta pingamizi mumeo anapotaka kuongeza mke wa pili .

Kuna ile wanaita chagulaga yaani unawakuta mabinti wa kisukuma wengii wanatoka eidha ngomani au wengine wanatoka kusindikiza harusi sasa wakati wanarudi wanume wa kisukuma husimama njiani na kuanza kuwatongoza, sasa hapo unaweza kuta mtu ktk hilo kundi yupo dada yake nae anatongozwa na mwanaume mwingine au unaweza ukawa unatongoza umesimama na mwanamke pembeni mkeo anapita anakuona na hafanyi chochote hii ni moja kati ya mila ya kisukuma japo kwa sasa imepotea sana ila huko kwingineko bado inaendelea, nyumbani kukiwa na mtoto wa kiume wa miaka 10, hapo anakuwa amekabidhiwa nyumba hata uje kuazima panga lazma umwambie yeye na ikitokea haujamkuta unaambiwa na akina mama mwenyewe hayupo.

Mwanamke wa kisukuma anachomiliki nyumbani ni kuku na maziwa ya ng'ombe lkn hao kuku anaowamiliki akija hawara wa mumewe anakamatiwa na kupewa bila mwanamke kupewa taarifa, nakumbuka nilikuwa na mwanamke mmoja rafiki sanaa kumbe mumewe hajui kusoma sasa yule jamaa ana mwanamke mwingine hukoo kitaaa yule mwanamke wapembeni hajui kama jamaa hajui kusoma akamtumia sms ya kumwambia aende ujumbe ule akausoma mke itabidi tu amwambie mwanmke wako anakuita huko nenda aisee nilishangaa sana kiufupi kuna wanawake wa kisukuma wanateseka sanaaaa
 
Ukweli 100% hili ni andiko bora la mwezi, mama watoto nilimpiga chini kama utani alivyoanza kuota mapembe nikachukua chombo nyingine yenye heshima mpaka inaniamkia. Wanaume tunataka UTII peke yake.
 
Mfumo ni aina ya mfumo wanaotaka uwe njia ya kuingiza mambo ya kisengelemaa mamaaae zao
 
Kwanza hili neno msimbe ni kiswalihi fasaha au ni moja ya neno la kikabila

Msimbe maana yake ni mwanamke alieolewa kisha akaachika na hili neno mm nimekuja kulijua usukumani .

Ktk jamii ya kitanzania wanawake wa kisukuma wale waliopo ndani ya mila na destuli binafsi naona wanaonewa sana au kunyanyasika.

Mwanamke wa kisukuma anaenda kusenya kuni,(kukata kuni ) tololi zima na sio moja ni zaidi ya mawili, wanaswaga ng'ombe kurudisha kuni kutoka msituni mwanamke wa kisukuma haruhusiwi kuhoji matumizi yeyote ya mali nyumbani kama mahindi,mpunga, ng'ombe nk. Mwanamke wa kisukuma hauruhusiwi kuleta pingamizi mumeo anapotaka kuongeza mke wa pili .

Kuna ile wanaita chagulaga yaani unawakuta mabinti wa kisukuma wengii wanatoka eidha ngomani au wengine wanatoka kusindikiza harusi sasa wakati wanarudi wanume wa kisukuma husimama njiani na kuanza kuwatongoza, sasa hapo unaweza kuta mtu ktk hilo kundi yupo dada yake nae anatongozwa na mwanaume mwingine au unaweza ukawa unatongoza umesimama na mwanamke pembeni mkeo anapita anakuona na hafanyi chochote hii ni moja kati ya mila ya kisukuma japo kwa sasa imepotea sana ila huko kwingineko bado inaendelea, nyumbani kukiwa na mtoto wa kiume wa miaka 10, hapo anakuwa amekabidhiwa nyumba hata uje kuazima panga lazma umwambie yeye na ikitokea haujamkuta unaambiwa na akina mama mwenyewe hayupo.

Mwanamke wa kisukuma anachomiliki nyumbani ni kuku na maziwa ya ng'ombe lkn hao kuku anaowamiliki akija hawara wa mumewe anakamatiwa na kupewa bila mwanamke kupewa taarifa, nakumbuka nilikuwa na mwanamke mmoja rafiki sanaa kumbe mumewe hajui kusoma sasa yule jamaa ana mwanamke mwingine hukoo kitaaa yule mwanamke wapembeni hajui kama jamaa hajui kusoma akamtumia sms ya kumwambia aende ujumbe ule akausoma mke itabidi tu amwambie mwanmke wako anakuita huko nenda aisee nilishangaa sana kiufupi kuna wanawake wa kisukuma wanateseka sanaaaa
umeongea vema na sample ya mfano wako ni nzuri,lakin tujiulize kitu kimoja.Ukijaribu kulinganisha jamii hiyo ya kisukuma na zile nyingine zisizo na mfumo dume wapi kuna afadhali katika ndoa zao?
 
Back
Top Bottom