Charles Richard Patrick
New Member
- May 18, 2024
- 1
- 0
Mfumo wa Elimu tulionao hapa Afrika hatukuutengeneza sisi wenyewe bali maadui zetu, hivyo kamwe usitegemee adui yako akupe elimu nzuri. Akupe elimu nzuri ili umpindue? Wazungu walipokuja kwa mara ya kwanza hapa Afrika, walitukuta tuna mfumo wa elimu wa ujuzi na badala yake wakauua na kutupa mfumo wa elimu ya nadharia (theory) ili watutengenezee wafanyakazi ambao ni wazuri wa kukumbuka na sio wanaoweza kufikiria! Unakwenda shule kujifunza mambo ya kipuuzi eti 'Homohabilis, photosynthesis, mbwa ana meno mangapi?' Nambie unakusaidia nini huo upuuzi? Wazungu wametupumbaza vya kutosha sana! Ndiyo! Unaamka usiku eti kusoma je ni mto gani mrefu kuliko yote Afrika? Vasco Da Gama alifika rasi ya tumaini jema mwaka gani? Unakumbuka kila kitu! Mwisho wa siku wazungu wanatengeneza nini? Wanatengeneza kontena lenye maarifa yasiyofaa.
Tuko huru mwaka wa ngapi huu hapa nchini? Hivi ulishawahi kuona kuna kinga yoyote imegunduliwa na daktari wetu? Hapana! Madaktari wetu baada ya kuhitimu elimu yao wanachojua tu ni muda gani wa kutoa panadol au jinsi gani apime joto la mwili! Ndiyo! Unaweza kuwaita kama "wagawa panadol"! Na ikumbukwe kuwa kosa sio lao bali mfumo mbovu wa elimu waliyotutengenezea maadui zetu! Wahitimu wetu wakimaliza walichokisomea utaona kuwa hawawezi kugundua chochote! Ndiyo! Jaribu kwenda Ulaya alafu linganisha mtoto wa Ulaya aliyesoma kwa miaka mitatu utaona mjanja na ana akili nyingi kuliko msomi wa chuo kikuu hapa Afrika. Wametudanganya wazungu eti tusome masomo 9 au 10 hivi wewe ni kompyuta? Wazungu watoto wao wanasoma somo moja tu ndiyo maana wanagundua vitu mbalimbali!
Mfano mwengine; tuna maprofesa kutoka shule za misitu ila anachojua profesa huyo ni jinsi gani ya kukata mti na kuhesabu vipande ila hajui thamani ya mti! Baada ya mkakati huu kukamilika wazungu wakaanzisha viwanda! Muajiriwa ni nani? Msomi aliyetoka shule ya kukumbuka ambaye anajua tu wapi pa kuweka tick na jinsi gani aweke tick! Ndiyo maana Afrika haiendelei. Wametudanganya sana wazungu kuwa ni lazima tutumie Kifaransa, Kireno au Kiingereza kufundishia watoto wetu kitu ambacho ni kibaya sana! Huwezi kufanya nchi yako iendelee kwa kutumia lugha ya kigeni. China wanatumia lugha yao kufundishia, Urusi wanatumia lugha yao kufundishia hata Ufaransa pia ila sisi tumedanganywa hatupaswi kutumia lugha yetu kufundishia watoto wetu na ndiyo maana hakuna mtu leo anajua utamaduni wetu baada ya kuhitimu elimu hiyo ya matakataka! Mtu ukionekana unadumisha mila na utamaduni wa Kiafrika basi watu weusi wenzako wanakuita usiyesoma au usiyestaarabika na watu hao hukuona hauna thamani kabisa kisa unadumisha utamaduni wa mababu zako!
Tumedanganywa juu ya historia halisi ya Afrika sana hususani pale wanapotufundisha eti mzungu ndiye amegundua vitu mbalimbali vya Afrika! Hata Mlima Kilimanjaro wametuaminisha kuwa amegundua mzungu! Ukiuliza huyo mzungu alipelekwa na nani huko mlimani utaambiwa Masawe! Sasa kwanini aandikwe mpelekwaji na si mpeleka? Kwani huyo mzungu si aliwakuta wachaga wakikata kuni na kuwinda swala pale? Hata Ziwa Victoria wazungu wametuaminisha kuwa wameigundua wao wakati huyo mzungu aliwakuta Wasukuma wakichota maji na kuogelea pale! Na wazungu wakaenda mbali zaidi wakatuaminisha kuwa tusimchague mgombea wa nafasi ya uongozi ambaye hajui kuongea lugha ya kigeni au asiye na cheti! Unajua kwanini wametuaminisha hivyo? Kwa sababu kwa mfumo mbovu wa elimu waliyotutengenezea ukienda shule tu basi unakuwa umejifunza jinsi gani umuumize wananchi wako na pia wanaamini wanauwezo wa kukuendesha na pia ushakuwa mtumwa wao mzuri!
Ndiyo maana unaona katika nchi 54 za Afrika ukiondoa nchi za waarabu na zile tatu zilizojikomboa hivi karibuni (Mali, Burkina Faso na Niger) unaona hakuna rais wa nchi nyingine anayeweza kuamka na kuikomboa nchi yake pia bara la Afrika kwa ujumla! China walikuwa na mfumo huu mbovu wa elimu kama tulionao leo hapa Afrika na wakaamua kuchoma moto vitabu vyote vya wazungu na kubuni elimu ya ujuzi leo unaweza kuona China wako wapi! Tubadilishe mfumo mbovu wa elimu waliyotutengenezea maadui zetu ndugu zangu! Hata usome miaka elfu moja kwa mfumo huu huwezi kugundua chochote. Ndiyo! Kama mfumo huu wa elimu waliyotutengenezea maadui zetu ungekuwa mzuri basi ungezalisha ajira badala yake mtu unahitimu kama mhandisi wa ujenzi ajabu unaenda kuwa kondakta wa mabasi ya mikoani, hivi hivyo vyeti ulivyovifungia chumbani vina kazi gani? Tulipigwa ndugu zangu! Nina mengi ya kuzungumza na Mh. Rais kuhusiana na ukombozi wa fikra wa watu wetu lakini ndivyo hivyo tena huwa hakuna urahisi!
CHARLES RICHARD
0718492565

Upvote
0