Mfumo mbovu wa N-Card Stendi ya Magufuli

Mfumo mbovu wa N-Card Stendi ya Magufuli

ismail hassan

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2017
Posts
696
Reaction score
1,629
Kufuatilia taarifa ya juzi halmashauri ya wilaya Ubungo ilipotangaza kuwa tiketi za kuingilia getini zilipwe kwa mfumo wa N card kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli kilitekeleza agizo.

Cha kushangaza mifumo waliyo iweka inatia sana ukakasi, kama ifuatavyo.

1. Dirisha la utoaji wa kadi ni moja kiasi kwamba asubuhi kunakuwa na mlundikano wa watu wengi sana.

2. Wizi kutokea, kutokana na mlundikano wa watu kwenye dirisha, watu hupoteza mali zao bimaana wezi nao hujiunga kwenye huduma ya kujifanya wanataka N card mwishowe kuibia watu mana ni mlundikano na akikuibia huwezi kumuona.

3. Vurugu kubwa kwa wanachi, mfano ni leo asubuhi watu walileta fujo mpaka wakataka kuvunja vile vimilango vya kuingilia, unakuta mtu amekata tiketi na basi linaondoka saa 12:00 lakini getini kuingia ni changamoto, hii inasababisha vurugu.

4. Sehemu chache za kuingilia, baada ya kupata N card sehemu za kuingilia ni chache na katika chache hizo utakuta kuna vimilango vingine vimekosa wahudumu na kusababisha vurugu.

5. Baadhi ya mabasi kutoingia kituoni, kuna baadhi ya mabasi hayaingii kituoni tangu juzi, nadhani hii huduma mbovu ndo imesababisha hili, serikali haioni kuwa inapoteza kodi kwa haya mabasi yanayochukuwa abiria nje ya kituo kikuu? Wafanyaje sasa?

Ushauri kwa Serikali
Huduma ya kutumia N card ni nzuri mana itaongeza kodi na kutosababisha upotevu na ubadhilifu wa makusanyo, maana inaeleweka njia ya zamani upigaji ulikuwa ni mwingi sana.

Serikali iboreshe mifumo ya utoaji huduma na ihakikishe kuwa kunakuwa na mazingira salama kwa wasafiri, madirisha ya utoaji wa kadi yawe mengi, elimu pia kwa wananchi itumike kwamba ukioata kadi unaweza weka vocha na kuepuka kupanga foleni ili kupata N card kila siku.
 
Kwan wenyewe hawakujua kwamba dirisha Moja litaleta msongamano wa watu!?

Tatizo hii nchi Siasa nyingi mno.
 
Na hapo bado umeme hujakatika, mtapenda[emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom