Mfumo mpya wa iphone utazuia wezi wa simu kuuza vioo, betri na kamera za iphone

Mfumo mpya wa iphone utazuia wezi wa simu kuuza vioo, betri na kamera za iphone

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274
Mwaka huu Apple imebadilisha utaratibu wake wa kurekebisha simu na vifaa vya kutumia simu. Wiki hii katika mfumo mpya wa iOS 18 wakaguzi na mafundi wa simu wamegundua Apple imeweka mfumo mpya wa kuzuia wezi kuuza display, betri na kamera za simu ambazo zimeibiwa.


Mfumo mpya wa iOS 18 umeweka mfumo wa Activation Lock katika parts za iPhone. Mfumo huu utazuia betri, display na kamera kuuzuwa kwa sababu iOS 18 inafunga na kutambua serial numbers za kila part ya simu na kuziunganisha na Apple ID.

Mwizi akiiba simu ambayo ina Apple ID, simu hiyo haitaweza kutumika wala kuuzwa spare zake.

Ukichukua display ya simu ambayo imewashwa Activation Lock hautaweza kuchuka kamera yake, display au betri na kuiweka kwenye simu nyingine. Utapewa ujumbe kuwa simu hiyo imewekwa spare (display, betri au kamera) ya simu nyingine ambayo imeripotiwa kuwa imeibiwa. Ujumbe huo utakuomba uweke details za Apple ID ambayo inamiliki spare hiyo ili kuifungua simu na kuweza kuitumia.

Apple imetoa RC (Release Candidate) kwa developers ikiwa na mfumo huu na Apple imeelezea lengo lake ni kuzuia mafundi kutumia spare za iPhone ambazo zimeibiwa.

Tayari mfumo huu umefanyiwa majaribio na wataalam na kuonyesha ni kweli unafanya kazi

Snapinsta.app_459668437_849089910649835_1894579827983820965_n_1080.jpg
Snapinsta.app_459624261_849089907316502_363612148869958706_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom