Jabali Jiwwe
Member
- Jul 28, 2022
- 7
- 8
MFUMO WA AJIRA NCHINI UBADILISHWE
Wakati ni sasa wa serikali pamoja na sekta binafsi kuja na mbinu au mkakati mpya wa ajira na kuajiri nchini.
Sote tunajua hivi sasa kuna malalamiko mengi kwa wananchi walio wengi kukosa ajira pamoja na kwamba elimu na sifa zote za kuweza kuitumikia nchi yao kupitia sifa za kielimu wanazo.
Sote ni mashahidi kuwa hivi sasa ukosefu wa ajira nchini ni bomu linalosubiriwa kulipuka, tunaweza kuona kwa sasa kuwa nchi yetu ipo na amani ya kutosha, huku viongozi wetu wakidhani wameweza sana kutuliza nchi iko salama lakin binafsi kwa maoni yangu naona kuna bomu litalipuka miaka ya mbele wala sio mbali litakalosababishwa na ukosefu wa ajira kwa walio wengi
Ni kawaida sana kwa sasa kusikia kiongozi akijinadi na kuwashauri vijana wajiari na akapongezwa na yeye binafsi kuona kama ameongea pointi kubwa sana ili hali akijua yeye kujiari alishindwa akaomba ridhaa kwa chama au kampuni au serikali ikamuajiri na wengi ya viongozi kinara wa kauli hii ni wanasiasa ambao wao walishindwa kujiajiri wakaomba ridhaa au wakaomba wananchi ajira kwa mana ya wabunge au madiwani
Mambo yote haya yamesababishwa na MFUMO MZIMA WA AJIRA HAPA NCHINI.
Kwanini nasema hivo?
Nimejaribu kufanya tafiti mimi mwenyewe bonafsi na nimegundua mfumo wa ajira tulio nao sasa unatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa na ya haraka kunusuru bomu litakalolipuka katika kipindi cha miaka kumi ijayo!
Nina mapendekezo kadhaa ya nini kifanyike katika mifumo yetu ya ajira kwa watanzania
(i) Serikali iandae sera na sheria mpya za kuongoza mfumo mzima wa wafanyakazi waliopo katika utumishi kwa serikali na binafsi, kivipi? Kwanza kubadili mda wa watumishi kustaafu kutoka miaka 60 iwe miaka 48
Hii itasaidia kuweza vijana wengi walio mtaani kuajiriwa kuchukua nafasi za hawa watakaostaafu kwa kila mwaka. Kwa sasa ukiangalia ni watumishi wengi sana wenye umri huo walio kazini ambao wengi wao walishalitumikia taifa kwa kazi zao, hii itafanya kuajiri watumishi wapya 35000 kwa kila mwaka, katika nyanja mbalimbali katika utumishi wa umma ikiwa ni serikalini na sekta binafsi.
Hii itaongeza ufanisi mkubwa katika utumishi hasa ukizingatia katika sheria ya sasa mtu mwenye miaka 45 haruhusiwi kuomba nafasi za ajira katika nyanja mbali mbali.
Kwa kigezo cha ufanisi, au umri umeenda, sasa waliopo kazini wenye umri huo iweje wawe na ufanisi kwanini wasi staafu kabisa ili vijana walio mtaani na wana sifa wasiajiajiriwe
Nadhani serikali ije na mpango huu mathubuti ili vijana wapate nafasi ya kulitumikia taifa lao
Pili kila mwaka serikali itakuwa inaokoa mabilion ya pesa, hii ni katika wale wanaostaafu kikawaida wanakuwa wanalipwa hela nyingi kuliko atakayeajiriwa kwa ajira mpya hii ni katika nyanja nyingi na muda huo serikali itaokoa kiwango fulani cha pesa cha mafao ya wastaafu hasa kutokana muda wa kustaafu kupungua kutoka miaka 60 mpka miaka 48 hasa ukizingatia idadi ya miaka kazini inaongeza kiasi kikubwa cha pensheni.
(ii) Serikali iweke watu wenye sifa (ufanisi)
Ripoti ya CAG kipindi cha Profesa Musa Asad alisema katika maofsi mengi ya uma nchi hakuna ufanisi, watu wameajiriwa wasio na sifa. Serikali inayo haja ya kuchunguza hili na kuajiri vijana walio mtaan wenye sifa na ufanisi mkubwa, wenye kiu ya kulitumikia taifa, hii itapunguza sana malalamiko na itawachukua vijana wengi waliomaliza vyuo na wapo mtaani bila ajira
(iii) Vyuo vithibitiwe kuanzisha kozi kiholela
Kwa sasa vyuo vingi, vyuo vya kati na elimu ya juu vimekuwa na utaratibu usio mzuri hasa huu wa kuanzisha kozi mpya kila mwaka ili viweze kudahili wanafunzi wengi, hali hii inafanya kuwa na utiriri wa kozi ambao katika mfumo wa ajira hazitambuliki, Seririkali inapotoa nafasi ya ajira, hutoa pia sifa za waombaji sasa kuna baadhi ya kozi hazitambuliki ingawa kazi hizo zaweza kuwa zinamfaa mtu huyo au mwombaji huyo hivo kufanya baadhi vijana kukosa sifa na kufanya vijana wengi kubaki mtaani na kuongeza idadi ya wasio na kazi mtaani.
Kwa hiyo mfumo wetu ajira uendane na mahitaji ya nchi na kozi zinazotolewa vyuo vikuu
Mfano wote ni mashahidi kwa sasa tunaambiwa walimu wa masomo ya arts ni wengi sana nchini, ni jukumu la vyuo vinavyotoa kozi hizo kuacha kutoa kwa miaka kadhaa ili kuepuka ukosefu wa ajira katika wale wanafunzi watakosoma ikiwa tayari mahitaji yake katika nchi hayapo, hii itapunguza lundo la wanafunzi au vijana wanakosa ajira na lawama kupelekwa kwa serikali. Katika hili pia vyuo viangalie sera ya na mipango ya serikali kwa muda muafaka, vyuo navyo vinakariri sera zilizopita kuliko kuangalia mahitaji ya jamii na maendeleo ya nchi kwenye sera na mipango, mfano juzi tumeona ajira kadhaa za afya zimekosa watu walioomba wenye sifa, hii ni habari mbaya sana kwa vyuo kwani vimeshindwa kutoa wataalamu katika maeneo hayo kwa kung'ang'ana na kozi ambazo serikali imeajiri watu wengi. Hili nalo katika mfumo mzima wa ajira linatia dosari ya kufanya vijana wengi wabaki mtaani kwa kusoma vitu vilivyo nje ya sera na mipango ya serikali.
(iv) Vijana wapewe vipao mbele katika nafasi za kisiasa.
Hii inaweza kusaidia kupunguza malalamiko ya vijana wengi ambao hawana ajira,
Serikali kupitia ofsi ya msajili wa vyama anaweza kuweka sheria kabisa kuwa katika kugombea kuwe na uwiano wa vijana watakaopewa nafasi ndani ya vyama hivyo, hii itasaidia vijana kuwa na sauti kikatiba ya kuweza kuamua mambo mbali mbali ya ki nchi.
Haya ni maoni yangu juu ya mfumo mzima wa ajira katika nchi yetu yatakayopunguz idadi kubwa ya vijana mtaani wenye sifa ya kuajiriwa na hatimaye wakaitumikie nchi yao.

Upvote
2