KERO Mfumo wa Ajira Portal hautambui mabadiliko ya elimu, huwezi kuomba tofauti na Elimu uliyojaza awali

KERO Mfumo wa Ajira Portal hautambui mabadiliko ya elimu, huwezi kuomba tofauti na Elimu uliyojaza awali

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mfumo wa Ajira Portal wa Secretariat ya Ajira ambao unapatikana katika tovuti ya Public Service Recruitment Secretariat | PSRS una changamoto kadhaa ambazo zimekuwa kikwazo kwa sisi Watumiaji wengi.

Mfumo huo hauruhusu kwa Watu wenye level ya elimu zaidi ya moja kujisajili na kuomba ajira katika nafasi tofauti na zile ambazo walijiandikisha mwanzo wakati wanajiunga kwenye mfumo.

Mfano ukiwa na Digrii au Diploma ukijisajili kwa moja kati ya hizo inamaanisha huwezi kuomba kazi kwa kutumia nafasi nyingine ya elimu hata kama umebadilisha vyeti kwenye mfumo.

Mfano ukijiandikisha Diploma kisha baadaye ukapata Digrii, mfumo hautatambua hayo mabadiliko kwa kuwa ile namba ya NIDA iliyotumika awali ilisoma wewe ni mtu wa Diploma, hivyo huwezi kuomba nafasi ya Digrii.

Hivyohivyo ukijiandikisha kuwa wewe una Digrii, zikitokea nafasi za Diploma, mfumo haukuruhusu kuomba kwa kuwa tayari namba yako ya NIDA inasoma wewe umesajiliwa katika qualification nyingine.

Tunaomba TAMISEMI washughulikie changamoto hii kwa kuwa imekuwa kikwao kwa watu wengi.
 
Huo mfumo ndo mzuri ili kila mtu apate kulingana na kiwango chake cha elimu kilipoishia
Kama una diploma upate kazi za diploma bila mtu mwenye diploma na degree kuongeza idadi ya waombaji
Kama una degree omba za degree tu

Washikilie hapo hapo
 
Umejaribu kuedit taarifa zako za elimu?
 
Huo mfumo ndo mzuri ili kila mtu apate kulingana na kiwango chake cha elimu kilipoishia
Kama una diploma upate kazi za diploma bila mtu mwenye diploma na degree kuongeza idadi ya waombaji
Kama una degree omba za degree tu

Washikilie hapo hapo
Naunga mkono hojaa.
 
Sasa si una degree ? Ulienda kusoma ya nn kama unataka kufanya kaz ya diploma
 
Zamani ilikua inawezekana, unaomba kwa qualifications zote ulizonazo. Ila nafikiri walipofanya tathimini zao wakaona haifai na ndiyo wakaja na mfumo ambao unatia Pingu au kitanzi.

Ila nachojua mpaka sasa ukiongeza qualifications Kutoka chini kwenda juu kwa maana ya dip ukaweka bachelor kwenye fani Ile Ile basi mfumo utajiahulisha na kusoma bachelor badala ya dip. Kisichowezekana ni kujishusha.
 
Mfumo wa Ajira Portal wa Secretariat ya Ajira ambao unapatikana katika tovuti ya Public Service Recruitment Secretariat | PSRS una changamoto kadhaa ambazo zimekuwa kikwazo kwa sisi Watumiaji wengi.

Mfumo huo hauruhusu kwa Watu wenye level ya elimu zaidi ya moja kujisajili na kuomba ajira katika nafasi tofauti na zile ambazo walijiandikisha mwanzo wakati wanajiunga kwenye mfumo.

Mfano ukiwa na Digrii au Diploma ukijisajili kwa moja kati ya hizo inamaanisha huwezi kuomba kazi kwa kutumia nafasi nyingine ya elimu hata kama umebadilisha vyeti kwenye mfumo.

Mfano ukijiandikisha Diploma kisha baadaye ukapata Digrii, mfumo hautatambua hayo mabadiliko kwa kuwa ile namba ya NIDA iliyotumika awali ilisoma wewe ni mtu wa Diploma, hivyo huwezi kuomba nafasi ya Digrii.

Hivyohivyo ukijiandikisha kuwa wewe una Digrii, zikitokea nafasi za Diploma, mfumo haukuruhusu kuomba kwa kuwa tayari namba yako ya NIDA inasoma wewe umesajiliwa katika qualification nyingine.

Tunaomba TAMISEMI washughulikie changamoto hii kwa kuwa imekuwa kikwao kwa watu wengi.
"Swala la mtu mwenye cheti cha diploma na degree kukataliwa kuomba kazi za diploma limepingwa vikali. Ukishapata degree, wewe unahesabika kama mwenye sifa za degree, hata kama ulipitia diploma. Hivyo, ukiomba kazi ya diploma, huwezi kupewa kipaumbele kwa sababu ni kutokuwa sawa kumshindanisha mtu mwenye degree na mwenye diploma kisa tu wote wana vyeti.

Kama kazi imetangazwa kwa wale wenye diploma, na waombaji walioishia diploma wapo, kwa nini tujaze nafasi kwa mtu aliyefikia kiwango cha degree? Kazi nyingi za degree ni za kiutawala (managerial), ilhali za diploma ni za utendaji wa moja kwa moja. Ukipeleka mtu mwenye degree kwenye kazi ya diploma, tayari mawazoni mwake anajiandaa kuonesha vyeti vya degree ili apandishwe cheo au atoke kwenye nafasi hiyo.

Ushauri wangu ni huu: Kama una vyeti vyote viwili (diploma na degree) na unataka kuomba kazi za diploma kwa sababu umeona pengo fulani, basi usiweke cheti cha degree kwenye mfumo. Hii itakupa nafasi bora ya kushindana kwenye nafasi za diploma."
 
Back
Top Bottom