DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Baada ya serikali kutangaza nafasi mpya za ajira kwa watumishi wa umma, matumaini yalizuka miongoni mwa maelfu ya vijana nchini. Wengi waliona tangazo hilo kama tiketi ya matumaini mapya baada ya miaka ya kusota bila kazi. Lakini furaha hiyo imegeuka kuwa changamoto kubwa.
Kupitia mfumo wa Ajira Portal, ambao ndiyo njia rasmi ya kuwasilisha maombi, waombaji wengi wamejikuta wakihangaika kuingia bila mafanikio. Wengi wanasema wamekuwa wakipata ujumbe ule ule unaorudiwa kila mara “Log in error.” Baadhi wamejaribu kwa siku kadhaa bila mafanikio, wengine wamekata tamaa kabisa.
Pia Soma: Serikali yatangaza nafasi 41,500 za ajira ikiwemo nafasi 7,000 kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama
Katika utafiti uliofanywa kwa siku tatu, imebainika kuwa malalamiko haya si ya mtu mmoja.
Waombaji kutoka mikoa mbalimbali wamelalamikia ugumu wa kuingia kwenye mfumo, kurasa kuchelewa kupakia, na wakati mwingine tovuti kushindwa kufunguka kabisa.

“Nilijaribu kuingia mara zaidi ya kumi, lakini kila nikijaribu, mfumo unaniambia log in error. Nimebadilisha kifaa, nikaenda kwa jirani, lakini bado. Naomba serikali iangalie hili jambo,” anasema mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.