Mfumo wa demokrasia unafanya nchi ziwe na mikopo mikubwa isiyolipika.

Mfumo wa demokrasia unafanya nchi ziwe na mikopo mikubwa isiyolipika.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Kila siku demokrasia inazidi kujithibitisha kama mfumo wa hovyo sana na haufai kutumika kama mfumo wa utawala.
Zamani nchi zilipoongozwa na wafalme nchi ilikuwa ni mali ya mfalme na vizazi vyake. Nchi ilikuwa kama mali yao binafsi na waliitunza kama mali binafsi.

Wafalme wengi walikuwa makini sana kuhakikisha kuwa mali yao haipotei. Walijitahidi kukopa kwa makini ili wasifilisike na wahakikishe wanarithisha wana wao mali ikiwa vyema. Hata wana wafalme wangeweza kumuua mfalme iwapo wangeona anataka kufuja urithi wao.

Pia kwenye mfumo wa kifalme mfalme hakuwa anawajibika kuwahudumia wananchi wake. Mfalme akiwafanyia kitu watu wake ilikuwa ni hisani tu. Mkimpa mfalme kodi yake ni yake kuitumia atakavyo.

Mfumo huu wa mtu mmoja kumiliki nchi si mzuri na wa kinyonyaji, lakini kwenye suala la kusimamia fedha ulikuwa mzuri kuliko wa kidemokrasia.

Kwenye mfumo wa kidemokrasia rais si mmiliki wa nchi, yeye ni msimamizi tu wa mali. Ni mpitaji tu. Hana uchungu wowote na mali ya nchi(Hana sababu ya kuwa na uchungu). Kuna uwezekano mkubwa madhara ya kukopa na kutapanya mali za umma yasimguse hata kidogo.

Pia serikali za kidemokrasia huwa na maafisa wengi sana ukilinganisha na zile za kifalme. Kuna wabunge, mawaziri, makatibu. . . Vyeo kibao. Wote hawa ni watumia pesa za nchi. Gharama za kulipa maafisa kwenye serikali za kidemokrasia ni kubwa mno.

Kingine ni kuwa kwenye mfumo wa kidemokrasia wananchi hutaka kuhudumiwa na serikali. Wananchi wana sauti juu ya matumizi ya pesa, na mara nyingi wanataka huduma zaidi na zaidi. Pia wana sauti juu ya kodi kiasi gani walipe

Matokeo yake ni kuwa serikali za kidemokrasia zinakuwa na matumizi mengi, zina uongozi usio na uchungu na mali ya umma na wananchi wasiotaka kulipa kodi.

Serikali nyingi za kidemokrasia zinaamua kukopa na kukopa. Serikali hizo zinajaa madeni hadi zinaishia kuanguka. Kila Rais ili abaki madarakani analazimika kukopa ili kuwafurahisha wananchi na maafisa wake. Kwanza mali siyo yake, na pili madeni atakomaa nayo anayekuja. Anayekuja naye amambambikia ajaye. Wakati wa ufalme alikuwa anaweza tokea mfalme mpya akaamua kufunga mkanda kufuta madeni ya baba zake. Rais wa kidemokrasia akisema afunge mkanda kufuta madeni ya watangulizi wake hawezi kaa madarakani hata mwaka. Basi anaamua kuendelea kukopa mambo yaende kipindi chake kama mdhamini kiishe.

Nchi inayoendeshwa kidemokrasia kufilisika sababu ya madeni ni suala la muda tu, halikwepeki.
 
Kama ulivyosema rais ni mpitaji tu, hana hati miliki ya nchi uko sahihi sana kwa mazingira ya sasa ya Tanzania. Samia ni moitaji tu, hana uchungu na rasilimali za Tanganyika, yeye ataziuza atakavyo na atahama nchi kwenda kwao Zanzibar akimaliza musa wake.
 
Shida sio demokrasia,shida ni matumizi ya akili kwa viongozi wengi walio kwenye ofisi za umma.Kila mwaka 500b zinatumika kwenye kununua magari ya kifahari na wakati huo huo hospitals hazina madawa.

Kiasi cha 200b zinatumika kuwalipa Wabunge wa viti maalumu,huu ni upumbavu ambao chanzo chake sio demokrasia,bali kukosa matumizi sahihi ya pesa ya umma.

Huko Ulaya watu walipambamba kuondoa tawala za kifalme,kwa sababu nchi sio mali ya mtu binafsi na ukoo wake.Waafrika ifike muda tukubali maneno ya P.W.Botha kwamba hatuwezi kujitawala na ndio maana hatuwezi panga mambo yasiyo zidi mwaka mmoja.
 
Acha kuhusisha demokrasia na ujinga wa viongozi.
 
Wajinga ndio waliwao.
Ukisikia mtu kavunja sheria ambayo yeye ameitunga ujue maangamizi yanakuja.
Ukisikia mtu kaapa kulinda katiba baadae mtu huyo huyo anakwenda kinyume na katiba lakini hakuna wa kumdhibiti ujue mifuno ipo kimaandishi lakini si kwa vitendo.
Lakini ukisikia mtu anadai kuwa tulikuwa wachanga kujitawala mshutukie,kwani hao watawala walifundishwa na akina nani kujua muda wa kujitawala.
 
Shida sio demokrasia,shida ni matumizi ya akili kwa viongozi wengi walio kwenye ofisi za umma.Kila mwaka 500b zinatumika kwenye kununua magari ya kifahari na wakati huo huo hospitals hazina madawa.

Kiasi cha 200b zinatumika kuwalipa Wabunge wa viti maalumu,huu ni upumbavu ambao chanzo chake sio demokrasia,bali kukosa matumizi sahihi ya pesa ya umma.

Huko Ulaya watu walipambamba kuondoa tawala za kifalme,kwa sababu nchi sio mali ya mtu binafsi na ukoo wake.Waafrika ifike muda tukubali maneno ya P.W.Botha kwamba hatuwezi kujitawala na ndio maana hatuwezi panga mambo yasiyo zidi mwaka mmoja.
Shida ni mfumo wa demokrasia. Kote kwenye demokrasia haya mambo yanatokea. Matumizi ya serikali yanakua kwa kasi. Rais akiwabania maafisa magari ya fahari na wabunge posho kubwa kubwa jua anajihatarisha.
 
Back
Top Bottom