Mfumo wa EFD sasa uko shwari

Benmpo

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2015
Posts
450
Reaction score
423
Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato (TRA) wamethibitisha kuwa tatizo lililotokea kwenye mfumo wa kielektroniki wa utoaji risiti (EFD) kwa siku kadhaa zilizopita limetatuliwa sasa. Hivyo asitokee mfanyabiashara atakayekataa kutoa risiti za kielektroniki kwa kisingizio cha kuwa mfumo hauko sawa kama ilivyokuwa hapo awali. Hima Watanzania tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi yetu.

UKIUZA TOA RISITI, UKINUNUA DAI RISITI.
 
Hili tangazo lako linatuhusu nin sis wakulima?au mmeishiwa posho hvyo mmeambiwa mtuhamasishe sie wakulima?Kulipa kodi ni jambo jema lakini matumizi ya hovyo yasiyomsaidia mlipa kodi,ulipaji unakua wa mtutu wa bunduki.
 
Labda sema kwamba huna elimu ya kodi. Nani kasema kuwa mkulima hapaswi kulipa kodi? Maendeleo yetu yanatuhitaji sote mimi na wewe
 
Kwetu ripoti bado haziendi, TRA wanafanya uzembe mkubwa sana halafu hawako wazi.
 
Bado zinasumbua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…