Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato (TRA) wamethibitisha kuwa tatizo lililotokea kwenye mfumo wa kielektroniki wa utoaji risiti (EFD) kwa siku kadhaa zilizopita limetatuliwa sasa. Hivyo asitokee mfanyabiashara atakayekataa kutoa risiti za kielektroniki kwa kisingizio cha kuwa mfumo hauko sawa kama ilivyokuwa hapo awali. Hima Watanzania tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi yetu.
UKIUZA TOA RISITI, UKINUNUA DAI RISITI.
UKIUZA TOA RISITI, UKINUNUA DAI RISITI.