Thailand
JF-Expert Member
- Nov 15, 2019
- 275
- 795
Tuanze kwa kusema nini maana ya mfumo wa elimu.
Mfumo rasmi wa Elimu kwa Tanzania, ni njia kuu ya kutoa huduma za masomo ya elimu kuanzia elimu ya awali hadi Chuo Kikuu. Mfumo wa elimu kwa Tanzania upo katika form ya 2-7-4-6-3+
✓Miaka 2 elimu ya vidudu/cheke-chea hutolewa kwa wanafunzi wenye umri kati ya miaka 5–6 (miaka 2), lakini hii watoto sehemu kubwa wanaanza wakiwa na umri wa miaka 3, ili kuwa na mazoea ya shule.
✓Miaka 7 elimu ya msingi ambayo hutolewa kwa watoto walio na umri wa miaka 7–13 (Darasa la I-VII)
✓Miaka 4 elimu ya sekondari hutolewa kati ya umri wa miaka 14–17 (Fomu 1-4)
✓Miaka 2 elimu ya juu ya sekondari hutolewa kati ya umri wa miaka18–19(Fom 5na6)
✓Miaka 3 au zaidi elimu ya Chuo Kikuu.
Ukiangalia vizuri mfumo wetu wa elimu wa 2+7+4+2+3 unampasa mwanafunzi wa kitanzania kukaa darasani kwa muda au zaidi ya miaka 18 akiwa anasoma ili apate degree yake ya kwanza.
Hii ni ajabu! Fikiria mtoto kama ameanza shule na miaka 7 itabidi akae darasani hadi miaka 25 atakapokuwa amemaliza degree yake ya kwanza alafu aje kupambana kwenye soko la ajira ambapo sasa tuna muingiliano katika soko la ajira kwa Afrika Mashariki.
Tuangalie kwa majirani zetu Kenya ambao ndo wapinzani wetu wakuu kwenye soko la ajira. Mfumo wao wa elimu uko hivi 8-4-4 jumla unakuta mtoto anakaa miaka 16 au 17 kupata elimu yake ya degree then anakuja bongo kuchukua ajira na fursa za mbongo huyo atakekuwa bado mwaka mmoja kuhitimisha masomo yake. Wasomi wa kenya wana cover fursa za ajira za Afrika Mashariki kutokana na sera ya kufungua mipaka na kuondoa vizuizi kwa wananchi lakini ni ngumu kwa mtanzania kupenya kwenye soko la ajira nje ya mipaka ya Tanzania hususani Kenya.
Hivyo watanzania lazima tuone ni kwa namna gani tunaweza kuenda kasi na mabadiliko ya dunia hasa kwanza kwa kubadili mfumo na mtaala wa elimu yetu ili uwe wezeshi kwa vijana wengi kupata elimu mahususi yenye kuwajengea uthubutu na kujiamini.
Mfumo wa elimu pendekezwa unaoweza kutuvusha watanzania ni wakupunguza muda wa watoto kuwa shule ili waje wawai fursa za ajira zilizopo ndani ya soko la Afrika Mashariki.
MFUMO WA ELIMU NI WA 7-2-2-3 badala ya ule wa zamani wa 7-4-2-3.
Ukiangalia vizuri mfumo wa elimu pendekezwa unaoweza kutuvusha utampunguzia mtoto wa kitanzania miaka 2 ya kukaa darasani, yaani 7+2+2+3=14 badala ya ule wa zamani wenye miaka mingi ya kusoma yaani 7+4+2+3=16.
Kwenye huu mfumo wa elimu pendekezwa Elimu ya msingi itakua miaka 7 kama awali na miaka 2 ya Elimu sekondari O level, miaka 2 ya Elimu sekondari A level na miaka 3 ya Elimu ya chuo kikuu.
Faida ya mfumo wetu wa elimu pendekezwa:
✓ ukizingatia data za kupungua kwa makadirio ya umri wa kuishi mtanzania, mfumo huu wa elimu pendekezwa utasadia mtoto kutokaa shuleni, hivyo yeye mwenyewe anaweza kuinjoi ajira yake kwa muda mrefu kabla hajafa. Hata pia wazazi wataona mafanikio ya vijana wao mapema wakiwa wamemaliza elimu ya degree.
✓ watanzania kuwahi kushika ajira na fursa zinazotuzunguka katika soko la Afrika Mashariki.
Mtaala wa elimu (mpangilio wa masomo na nini cha kufudishwa) ndani ya mfumo huu mpya wa elimu utakuwa kama ufatavyo:
1. Kuanzia darasa la kwanza hadi la 2
Masomo; KUSOMA, KUANDIKA, NA KUHESABU kwa lugha kuu mbili English na kiswahili.
2. Darasa la 3 hadi 5, masomo yatakuwa MATHEMATICS, SCIENCE, URAIA, ENGLISH NA KISWAHILI.
3. Darasa la 6 hadi la 7, masomo hapa yatakuwa mengi kidogo na mwanafunzi kupitia haya masomo ndo yatatoa mwelekeo wa mtoto aende kusoma either sayansi, biashara au Arts katika masomo yake ya sekondari. Masomo katika hatua hii yatakuwa ni, MATHEMATICS, PHYSICS, CHEMISTRY, BIOLOGY, ECONOMICS ( hili somo nalo inabidi lianze mapema kutokana na umuhimu wake katika kuleta maendeleo katika taifa letu) HISTORY, GEOGRAPHY, URAIA NA UZALENDO, KISWAHILI, ENGLISH NA UJASIRIAMALI.
Hayo ndo yatakuwa masomo ya elimu ya msingi kiasi kwamba hata mtoto asipoendelea na masomo ya sekondari atakuwa na faida ya kufahamu mambo mengi ya muhimu.
Kwa sababu elimu ya sekondari itaitaji mtoto kuchaguliwa wenda kusoma Sayansi au biashara au Arts hivyo rekodi za ufaulu wa mtoto zitarekodiwa kuanzia darasa la kwanza hadi la 7. Mtoto wa ufaulu mkubwa na Mwenye ufaulu wa kuanzia C marks 60 kwenye kila somo lake la Sayansi atachaguliwa kujiunga na shule Ya Sayansi, chini ya hapo kulingana na ufaulu wake anaweza kuchaguliwa kusoma either biashara au Arts. Hili halitaingiliwa na wazazi maana unakuta muda mwingine mtoto anauwezo mkubwa kwenye masomo ya biashara au Arts lakini mzazi anamlazimisha kusoma Sayansi.
ELIMU YA SEKONDARI
4. Kuanzia kidato cha 1 hadi cha 2, mtoto atachaguliwa kusoma either biashara, Sayansi au Arts.
Masomo kwa mtoto atakechaguliwa kusoma SAYANSI yatakuwa; MATHEMATICS, PHYSICS, CHEMISTRY, BIOLOGY, COMPUTER, GEOGRAPHY, URAIA, KISWAHILI, ENGLISH NA UJASIRIAMALI.
Kwa mtoto atakechaguliwa kusoma Arts kidato cha 1 na 2 masomo yake yatakuwa;
HISTORY, GEOGRAPHY, URAIA, COMPUTER, KISWAHILI, ENGLISH, CHINESE, FRENCH, ECONOMICS NA UJASIRIAMALI.
Kwa mtoto atakechaguliwa kusoma Biashara masomo yake yatakuwa; ECONOMICS, ACCOUNTANCY, COMMERCE, COMPUTER, KISWAHILI, ENGLISH, MATHEMATICS, URAIA, NA GEOGRAPHY.
Baada ya miaka hiyo miwili ya mtoto kusoma kidato cha 1 na 2, mtoto atafanya mtihani wa taifa Necta na atakechaguliwa baada ya kufaulu mitihani yake atajiunga na Elimu ya Advance form 3 na form 4, na atachaguliwa kusoma tahasusi comb aliyofaulu vizuri.
ELIMU Ya SEKONDARI ADVANCE
Form 3 hadi 4, wanasayansi watakao faulu watakaochaguliwa kusoma tahasusi comb mojawapo kati ya hizi: PCM, PCB, CBG, CBN, CBA, PMCo(physics, mathematics, computer) PBPE(Physics, biology, physical education)
Wanabiashara wataoka chaguliwa kusoma advance watapashwa kusoma comb zifuatazo, EGM, ECA, EMA( Economics, mathematics na accountancy) EACo(economics, accountancy na computer)
Kwa comb za Arts masoma yatakuwa kama ifuatavyo; HGE, HKL, HGL, HGK, KLF, LFChinese.
Masomo ya ziada kwenye mtaala yatakuwa ni STADI ZA KAZI, MUZIKI, SANAA NA UTAMADUNI.
Watanzania tusapoti mabadiliko Ya mfumo wetu wa elimu wa kisasa ili kuwezesha vijana wetu kuziwahi fursa za ajira na ujasiriamali katika ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Upvote
1