Mfumo wa elimu wa Nchi ya Ufini unavyolifanya Taifa hilo kuwa bora katika elimu Duniani; Tanzania inajifunza nini?

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,628
Reaction score
6,411
Nchi ya Ufini (Finland) ni Nchi mojawapo kati ya Nchi zilizopo upande wa Kaskazini wa Ulaya inapakana na Sweden Norway na Russia.

Nchi hii ina ukubwa wa kilomita a mraba 338,455 km². Inakadiriwa uwa na idadi ya watu milioni tano na laki tano (5.5 mill). Mji wake Mkuu unaitwa Finish

Nchi inafanya vizuri sana kwenye masuala ya elimu Duniani kwa mfano kulingana na US. Global investors mwaka 2020 katika orodha yake Nchi kumi ambazo watu wake wameelimika sana Nchi ya Ufini (Finland) ilishika nafasi ya nane huku asilimia 43.60 ya watu wake walihesabika kuwa wasomi pia, Nchi hii ikionekana kuwa na bunge bora sana Duniani linalozingatia demokrasia, haki za kiraia na uhuru wa kujieleza. Kigezo kilichotumika kupima Nchi zilizoelimika ni kile kilichotafsiruwa na Nchi za Ulaya (OECD) ambacho kina zifasiri nchi zilizoelimika zaidi Duniani kuwa ni zile zenye asilimia kubwa a watu wenye umri wa miaka 25mpaka 64 ambao wamehitimu elimu ya vyuo vikuu katika muundo wa miaka miwili mpaka minne au mafunzo ya ufundi.

Kwa nini Nchi ya Ufini inafanya vizuri katika suala la elimu Duniani? Swali hili limenifanya kupitia maandiko mbalimbali yanayouelezea mfumo wa elimu wa Ufini ulivyo na nimeweza kubaini masuala yafuatayo ambayo angalau Nchi yetu Tanzania kupitia wizara ya elimu sayansi na teknolojia ikiyatupia jicho na kuyatilia uzito tunaweza tumepata matunda "returns " ya elimu ya mtu binafsi na za jamii jambo ambalo litaifanya jamii pana ya Watanzania kuwa bora na iliyostarabika maradufu. Masuala hayo nia;

1. Mtaala wa elimu katika Nchi ya Ufini huukiliwa na Walimu. Walimu katika nchi ya Ufini wa nguvu kubwa katika kuutawala mtaala wa elimu. Siyo rahisi kwa wanasiasa kuchopeka lolote wanaloliona linafaa kwa maslahi yao kwenye mtaala wa elimu.

2. Elimu katika Nchi ya Ufini hutolewa ila malipo. Katika Nchi hii Wazazi jukumu lako ni kuhakikisha watoto wao wanakwenda shuleni suala la chakula na vitabu hutolewa bure shuleni.

3. Wanafunzi wanapokuwa shuleni kupata muda wa kushiriki katika michezo mingi na ya aina tofautitofauti. Shule za Ufini huandaliwa katika hali ya kuwa a mazingira yanayoruhusu michezo mbalimbali kufanyika.

4. Wazazi/ walezi wa Wanafunzi hawachangishwi mchango wowote ule. Shule zote kuwekewa miundombinu katika hali ya usawa haya yote hufanyika kutokana a kodi wanazolipa Wananchi wa Ufini. Mfumo wa kodi wa ufini ni rafiki jambo linalowafanya wananchi kupenda kulipa kodi badala ya kukimbia kulipa kodi.

5. Matokeo ya mitihani ya ndani ya shule huwa hayatangazwi au kulinganishwa kati ya shule na shule, Shule hujipima zenyewe kwa zenyewe.

6. Walimu katika Nchi ya Ufini ni wasomi. Siyo jambo la ajabu kwa Profesa Profesa katika Nchi ya Ufini kufundisha katika madaraja ya elimu ya msingi. Walimu wengi Ufini wana shahada za uzamili na uzamivu.

7. Mfumo wa uchaguzi wa fani ya ualimu katika Nchi ya Ufini unamtaka mtu kuchagua kama chagua la kwanza " first option" na siyo ilimradi.

8. Fani ya ualimu inaheshimiwa na Wazazi pamoja na jamii kwa ujumla. Walimu katika Nchi ya Ufini wanaheshimika kama wanavyoheshimika madaktari, wanasheria na wahandisi.

9. Hakuna mtoto anayeachwa kuwa mjinga. Serikali ya Ufini huhakikisha inazusaidia familia masikini na zenye watoto wadogo kwakuwapatia vyakula na mavazi ili kuhakikisha watoto hao wanapata elimu.

10. Shule husisitiza stadi za msingi za umahiri na umilisi wa kila somo. Wanafunzi hawaandaliwi kushindana, yaani kundi la wanaoweza na wasioweza " winners and loosers" ila wanaandaliwa wote kuweza.

11. Watoto wadogo wa madarasa ya awali na msingi kuachiwa uhuru wa kutosha kufanya mambo yao ya utoto. Ni mara chache sana kwa watoto wa Ufini walio chini ya umri wa miaka kumi 12 kupewa kazi za nyumbani (home-work).

13.Watu wa Ufini huamini "kidogo ni kingi". Wanafunzi wa Ufini kwa kiasi kikubwa hufundishwa utafuta utatuzi wa changamoto katika maisha halisi badala ya kukasirishwa nukuu nyingi za masomo.


​
 
Sasa nchi ya watu 5.5m unalinganishaje na nchi yenye watu takribani 58m? Wasomi wetu sometimes mnajidhalilisha.
Unajidhalilisha sana kwa kufikiri taratibu mbona hujiulizi kwa nini Israel ni Nchi ya jangwa na hawalii lii njaa?..unapata fundisho gani?
 
Mfumo wa Elimu ya Tanzania ni wa Kumfanya Msomi ajikite sana katika Kufaulu with the dinstiction ( A au B+ ) na Kupata Cheti cha Kitaaluma ili akija nacho Mitaani aje Kuwaringishia Wasiosoma na Wamuogope wakati yeye Mwenyewe Kichwani na katika Application ya kile alichosoma Shuleni au Chuoni hawezi Kukitafsiri kwa Maendeleo yake na ya Taifa.
 
Hili ni tatizo ndiyo maana kuna haja ya kujifunza kutoka kwa wenzetu.
 
Ongezea na tuna rasilimali kibao
USA ina raia zaidi ya 200M+ na sisi tuna 60M mbona wametuzidi sana ...kama unaangalia kigezo cha idadi ya watu kufanya nchi yao kua bora?
 
Mji mkuu wake ni HELISINK
 
Kile kidhungu cha Prof. Ndalichako kili niacha hoi. Waziri wa Elimu Tz.
 
Mpaka leo najiuliza kwanini mfumo wa elimu wa tanzania bado haujaboreshwa huwa napata majibu mengi ambayo sio vyema kuyaandika hapa.

Mfumo wa elimu ndio nguzo kuu ya maendeleo kwa taifa husika hivyo ni kitengo kinachotakiwa kuboreshwa kila baada ya muda na kuangaliwa kwa makini sana ili mfumo uweze kuffit mahitaji ya taifa na wananchi.
Kitu ambacho Tanzania imeshindwa kufanya.

Kama Tanzania ikiweza kushirikiana na kujifunza mazuri kutoka katika mataifa mengine basi tunaweza kutoka hapa tulipo na kupiga hatua kubwa.
Sio kwenye mfumo wa elimu tu bali kuna mifumo na vitu vingi vinavyotakiwa kuboreshwa au kubadirishwa,
Ni muda wa kuanza kuondoa vyote vya zamani na kuboresha au kubadirisha ili tuweze kukimbia na kasi ya dunia kwenye technology, elimu na uchumi.
 
Kaa kwa kutulia, unazungumzia Ufini au Israel?
Kwani nimeandika ili kujilinganisha?..
Mifano ya Ufini na huo wa Israeli niliokupa kutokana na swali lako ni ili tuangalie cha kujifunza au fundisho na siyo kujilinganisha.
Kumbuka kujifunza jambo siyo suala la kulingana.
Karibu tena.
 
Kwani nimeandika ili kujilinganisha?..
Mifano ya Ufini na huo wa Israeli niliokupa kutokana na swali lako ni ili tuangalie cha kujifunza au fundisho na siyo kujilinganisha.
Kumbuka kujifunza jambo siyo suala la kulingana.
Karibu tena.
Tunapata funzo gani na demographic dividend tofauti kwa Ufini na TZ?
 
Tunapata funzo gani na demographic dividend tofauti kwa Ufini na TZ?
Hatuangalii population hapa ila tunachokiangalia ni je hiyo population regardless ni kubwa au ndogo inafanya nini na inakifanya namna gani?
Unataka kujenga hoja mufilisi kuwa hatuwezi kujifunza kutoka kwenye eneo lenye idadi ndogo ya watu kuliko yetu jambo ambalo sidha kama akili yako inaliafiki.
 
Demographic dividend vs Population SI kitu kimoja ndugu. Tulia kwanza naona umeshaanza kupanik.
 
Kwa akili hizi za viongozi wa AFRIKA za kuwaaminisha wananchi wake kuwa ni "wanyonge" hatuna la kujifunza zaidi ya ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…