KERO Mfumo wa ESS hautambui changamoto za kiutumishi katika ombi la uhamisho

KERO Mfumo wa ESS hautambui changamoto za kiutumishi katika ombi la uhamisho

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

jiwe angavu

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Posts
22,569
Reaction score
43,614
Tangu kuletwa kwa mfumo huu umekua kikwazo na kero zaidi kwa watumishi kuomba uhamisho.

Mfumo huu umetumiwa kuminya haki ya uhamisho kwa watumishi waumma.

Mbaya zaidi mfumo hautambui changamoto za watumishi katika kuomba uhamisho mfano,ugonjwa,mazingira hatarishi au ndoa.

Hali hii inapelekea watumishi wanaoomba uhamisho kukata tamaa na kukosa hama sa ya utendaji kazi.

OMBI:mfumo utambue mahitaji na changamoto hizo za watumishi wanao omba uhamisho.
 
Wakizingua unazingua pia. Mtu aruhusiwe aende atakako kulingana na sababu zake. Baada ya hapo mapengo yatazibwa kwa kuelekeza wafanyakazi wapya katika maeneo yenye uhaba kama yatakuwepo.
 
Hivi kwa nini huu mfumo hauna loan take over? huwezi kuuza deni lako hata kwa bank nyingine na ukitaka kutop up ndo kifo chako!😄 milion 35. Unalipa mil 70 .
 
Tangu kuletwa kwa mfumo huu umekua kikwazo na kero zaidi kwa watumishi kuomba uhamisho.

Mfumo huu umetumiwa kuminya haki ya uhamisho kwa watumishi waumma.

Mbaya zaidi mfumo hautambui changamoto za watumishi katika kuomba uhamisho mfano,ugonjwa,mazingira hatarishi au ndoa.

Hali hii inapelekea watumishi wanaoomba uhamisho kukata tamaa na kukosa hama sa ya utendaji kazi.

OMBI:mfumo utambue mahitaji na changamoto hizo za watumishi wanao omba uhamisho.
Mkuu ukitaka ufate utalatibu aisee utasota sana. Soma tena sentence hiyo
 
Huu mfumo ungewekwa kipengele cha uhamisho kwa watu wenye case maalum, hii ingesaidia watu wenye changamoto kubwa labda kama za kiafya na matatizo mengine ya kijamii ili waweze kuhama, kitu cha msingi katika uhamisho huu ni strong supportive documents. Hii ingesaidia sana maana huu utaratibu wa kufosi hadi mtu afikishe miaka mitatu na changamoto kibao za Vacancy not budgeted si sawa na sababu zisizokuwa na tija ili kuminya uhamisho kwa watumishi.

Pia, hata watu wanaoomba kuhama kwa kufuata taratibu maalum wangewekewa kipengele Cha kukata rufaa maana case za kukataliwa uhamisho zimekuwa nyingi mno licha ya watu kuwa na sababu strong. Mbona mambo mengine yana dirisha la rufaa endapo muhusika hajaridhishwa na matokeo..? Tunaona Bodi ya mikopo ya wanafunzi wanafanya hivyo. Uhamisho ni jambo sensitive kwa mtumishi na ni sehemu inayoamua muelekea wa maisha ya mtumishi husika kwanini wao wanachukulia poa. Si sawa Mnaumiza familia za watu
 
Huu mfumo umejaa mapungufu mwanzo mwisho. Mazuri yake ni ya kutafuta kwa tochi.
 
Back
Top Bottom