Mfumo wa gpa kutumika kuchakata matokeo ya kidato cha nne 2014 na kidato cha sita 2015

NZELLA

Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
37
Reaction score
4
Baraza la mitihani la Tanzania NECTA linatarajia kuanza kutumia mfumo mpya wa upangaji matokeo ya mitihani ya mwisho yaani FE kuanzia mitihani itakayofanyika NOVEMBER,2014 na kidato cha sita MAY,2015.
Kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa BMT CA itachangia alama 30 na FE alama 70.Source barua ya tarehe 3.3.2014 iliyotumwa shuleni kwangu
 
Elimu ya Tanzania mmh haya.....

salaam aleykum!!
vyuo vingi hutumia utaratibu huu kutoa nafasi ya effort ya mwanafunzi katika continuous assessment (CA) kujidhihirisha katika matokeo yake ya kumpatia cheti. mtihani wa mwisho sio jibu pekee la kuonyesha umahili wa mwanafunzi ambayo ni system tuliyoirithi kwa waingereza.

tatizo linakuja kwenye mbinu na authenticity ya namna continous assessment inapatikana kutoka shule kadhaa ambazo zimezagaa na zina circumstances tofauti. hata kuna vyuo ambavyo baadhi ya walimu walitumia CA kuwapa ufaulu mzuri baadhi ya wanafunzi wa aina yao ili wabakie kama tutorial assistants (TAs)
 
Mie nadhani ni mfumo mzima wa elimu unatakiwa kutengenezwa, sio kudeal na matokeo kuridhisha watu... mfumo ndio tatizo na walimu waangaliwe sio kuleta CA au division 5, 6....
 
Mashaka yangu ni hapo kwenye C.A maana shule zinaendeshwa kibiashara zaidi kuvutia wazazi hivyo kutakuwa na uchakachuaji tu.
 
Tunaomba mtuwekee hizo GPA zitakavyochakatwa ili tuchangie vizuri maana hilo tangazo bado hatujaliona
 
salaam aleykum!!
vyuo vingi hutumia utaratibu huu kutoa nafasi ya effort ya mwanafunzi katika continuous assessment (CA) kujidhihirisha katika matokeo yake ya kumpatia cheti. mtihani wa mwisho sio jibu pekee la kuonyesha umahili wa mwanafunzi ambayo ni system tuliyoirithi kwa waingereza.

tatizo linakuja kwenye mbinu na authenticity ya namna continous assessment inapatikana kutoka shule kadhaa ambazo zimezagaa na zina circumstances tofauti. hata kuna vyuo ambavyo baadhi ya walimu walitumia CA kuwapa ufaulu mzuri baadhi ya wanafunzi wa aina yao ili wabakie kama tutorial assistants (TAs)

Maelezo mazuri sana. Asante. Tatizo langu siku zote ni kushindwa kuelewa ni kwa nini Wizara, na BMT, kuleta mabadiliko mazito kama haya kwa kushitukiza. To me, it amounts to changing goal posts between the Match na double standards za hali ya juu! Kwa nini Tangazo hili lisitolewe leo kwa ajili ya Graduants wa Mwaka 2017 ili wote wajiandae? Tunaongelea Wanafunzi walioko Kidato cha Nne ambao, kwa Shule zilizo seriious kama Seminaries, wamekwisha kamilisha Syllabus na sasa hivi wako kwenye final touches. Tabia hii ya kuleta mabadiliko ya ghafla inakatisha tamaa kabisa kwenye suala la Elimu kwenye Nchi hii!:frusty:
 
Wakuu hii thread imenichanganya sitaki kuamini kuwa hii wizara ya Elimu na Baraza la Mitihani wamekuwa ni sikio la kufa kiasi hicho waweze kuthubutu kutumia mfumo mpya wa upangaji wa matokeo wakati wanafunzi wenyewe wameshamaliza mitihani ya Kidato cha Sita kwa wale wanaochukua masomo ya arts. Mwezi Novemba walitangaza madaraja mapya sasa kabla hata ya kuyatumia iweje waje na mfumo wa GPA wakati wanatangaza hayo ya Novemba walisema yalipangwa kwa kuzingatia maoni ya wadau ambapo utafiti ulifanyika kwa kutumia madodoso? Sasa je kuna utafiti gani mwingine umefanyika. Wizara ya elimu na NECTA waache kabisa kufanya usanii kwenye upangaji wa madaraja wanafanya kiini macho kubadili mara kwa mara ili watudanganye kuwa elimu imepanda. Ama kweli hii BRN inaimaliza kabisa elimu yetu ambayo kwa sasa iko ICU!!!!!
 
Baraza la mitihani la Tanzania NECTA linatarajia kuanza kutumia mfumo mpya wa upangaji matokeo ya mitihani ya mwisho yaani FE kuanzia mitihani itakayofanyika NOVEMBER,2014 na kidato cha sita MAY,2015.
Kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa BMT CA itachangia alama 30 na FE alama 70.Source barua ya tarehe 3.3.2014 iliyotumwa shuleni kwangu
wana CA..??
 
Ha ha ha hahaha!!!! kama habari ndiyo hiyo basi elimu kwishey, kila kukicha ni kupanga alama tu badaala ya kuangalia namna ya kuboresha miundombinu shuleni. Mmmmmh, mpaka kawambwa amalize muda wake wa uwaziri 2015 atakuwa ameifanyia KWELI sana elimu yetu kama alivyofanyia KWELI shirika la reli.
Baraza la mitihani la Tanzania NECTA linatarajia kuanza kutumia mfumo mpya wa upangaji matokeo ya mitihani ya mwisho yaani FE kuanzia mitihani itakayofanyika NOVEMBER,2014 na kidato cha sita MAY,2015.
Kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa BMT CA itachangia alama 30 na FE alama 70.Source barua ya tarehe 3.3.2014 iliyotumwa shuleni kwangu
 
Wakuu hii thread imenichanganya sitaki kuamini kuwa hii wizara ya Elimu na Baraza la Mitihani wamekuwa ni sikio la kufa kiasi hicho waweze kuthubutu kutumia mfumo mpya wa upangaji wa matokeo wakati wanafunzi wenyewe wameshamaliza mitihani ya Kidato cha Sita kwa wale wanaochukua masomo ya arts. Mwezi Novemba walitangaza madaraja mapya sasa kabla hata ya kuyatumia iweje waje na mfumo wa GPA wakati wanatangaza hayo ya Novemba walisema yalipangwa kwa kuzingatia maoni ya wadau ambapo utafiti ulifanyika kwa kutumia madodoso? Sasa je kuna utafiti gani mwingine umefanyika. Wizara ya elimu na NECTA waache kabisa kufanya usanii kwenye upangaji wa madaraja wanafanya kiini macho kubadili mara kwa mara ili watudanganye kuwa elimu imepanda. Ama kweli hii BRN inaimaliza kabisa elimu yetu ambayo kwa sasa iko ICU!!!!!

Soma vizuri ni Form Six wa 2015 na Form Four watakao fanya mtihani mwaka huu November.
 
Mkuu nimeona kuwa mfumo huo utaanza kwa form VI 2015 lakini bado hoja zangu kuhusu dosari ya mfumo uliotangazwa na katibu Mkuu Novemba 2013 ambao ulitokana na maoni ya wadau sijazielewa. Kwa nini mabadiliko kila kukicha?
Soma vizuri ni Form Six wa 2015 na Form Four watakao fanya mtihani mwaka huu November.
 
kwa private candidates itakuwaje kuhusu ca?

ni kwamba kwa kuwa kumekuwepo na malalamiko mengi khsu ca kwa pc necta pia imetoa mwongozo kuwa watahiniwa wa kujitegemea yaan pc watafanya paper mbili ile ya school cand.ambayo itatumika km ca na ile ya kwake itakayotumika km final exam(fe) REJEA RATIBA YA NECTA F.4 MWAKA 2014
GPA HIZO NITAZIWEKA WAZ KESHO MUNGU AKIPENDA!
 
Tz bwana, kila wakiamka wanakuja na kitu kingine. Haya bwana, tupelekeni tu mnavyotaka!!!!!!

Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Tutashukuru sana ukituwekea hizo taarifa kwa undani. Yaani kama NECTA wameweka paper ya pili kwa pc eti iwe ni GPA basi hapo inaonesha kuwa uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana. Tangu lini mtihani wa taifa ukawa ndiyo ca?

NECTA imekaa kisiasa zaidi kuliko kitaalamu na ndiyo maana wameanzisha grade E halafu wanasema iko sawa na F lakini inawanyanyua watu kupata div I-III lakini anayepata E zote anaambiwa amefeli.

You can only find this in Tanzania
 
Maelezo mazuri sana. Asante. Tatizo langu siku zote ni kushindwa kuelewa ni kwa nini Wizara, na BMT, kuleta mabadiliko mazito kama haya kwa kushitukiza. To me, it amounts to changing goal posts between the Match na double standards za hali ya juu! Kwa nini Tangazo hili lisitolewe leo kwa ajili ya Graduants wa Mwaka 2017 ili wote wajiandae? Tunaongelea Wanafunzi walioko Kidato cha Nne ambao, kwa Shule zilizo seriious kama Seminaries, wamekwisha kamilisha Syllabus na sasa hivi wako kwenye final touches. Tabia hii ya kuleta mabadiliko ya ghafla inakatisha tamaa kabisa kwenye suala la Elimu kwenye Nchi hii!:frusty:

Mkuu hilo linakera, linakera, linakera sana - mie liliweza kuniathiri nikiwa chuoni. tumepiga miaka mitatu mfumo wa final Exam (100%) ukitumika ili tupimwe baada ya muda huo. mwaka huohuo wa 3 utawala ukakurupuka na kusema CA miaka 3 ni 75% na final 25%!!!! - watu tulikuwa tuna maintain CA ya kutufanya tu survive tukisubiri tutie gia kubwa final exam ambayo ilizoeleka kuwa 100%. Kwa kweli amri hiyo ilitupa majanga makubwa kwa vyet vyetu.

Kwa kweli walipaswa wayatoe mabadiliko hayo kuwahusu wapya wanaoingia ili waende na mabadiliko hayo hadi wanapomaliza.
 
Kwa kweli hawa NECTA ni watu wa ajabu sana yaani wao wakikurupuka tu wanatbadilisha viwango vya ufaulu.
why, kwanini whyyyyy?
 
Tz bwana, kila wakiamka wanakuja na kitu kingine. Haya bwana, tupelekeni tu mnavyotaka!!!!!!

Sent from my iPhone using JamiiForums app
Mkuu kweli hapa ni kupelekana tu yaani Kidato cha sita 2014 watatumia mfumo mpya halafu 2015 mfumo mwingine tofauti kama ilivyooneshwa kwenye mwongozo wa NECTA NECTA imetoa mwongozo wa matumizi ya viwango vya Ufaulu (Aprili 2014) ambao umesambwazwa katika shule zote ze sekondari kupitia kwa Maafisa Elimu wa Mikoa. Kwa mujibu wa mwongozo huo Madaraja ya ufaulu kwa Kidato cha Sita 2014 yatapangwa kwa kutumia mfumo uliooneshwa kwenye ukurasa wa 8 wa mwongozo huo ambao ni:

Div I pointi 3-7
Div II pointi 8-9
Div III Pointi 10-13
Div IV awe na D mbili au C moja
Div 0 aliyepata chini ya D mbili.

Kwa mujibu wa mwongozo huo masomo yatakayohesabika kwenye kupanga pointi ni yale tu yaliyoko kwenye tahasusi yaani combination. Kwa maneno mengine suala la kupata cheti kwa mgongo wa Bible Knowledge au Islamic Knowledge litakuwa halipo tena.

Kuanzia Kidato cha Nne 2014 na Kidato cha Tano Sita 2015 mfumo wa GPA utatumia. Kwa maelezo Zaidi soma kurasa wa 8 na 9 na pia unaweza kukipata kijitabu hicho toka shule yoyote ya sekondari au kwenye ofisi za elimu za mkoa na wilaya.
 
Back
Top Bottom