Ndugu wanajamii,
Naitwa Sese, Naandika ujumbe huu nikiwa na maumivu ya moyo na sintofahamu kubwa juu ya hatima ya mtoto mdogo ninayemshughulikia kwa ajili ya mkopo wa elimu ya juu. Katika hatua ya kujaza fomu ya mkopo (HESLB), kwenye kipengele cha preliminary information, ukiweka taarifa za mzazi aliyefariki, unatakiwa uweke RITA Verification Number ambayo ni ile namba inayotolewa baada ya kuhakiki cheti cha kifo kupitia mfumo wa RITA.
Tatizo kubwa ni kwamba, baada ya kuiweka namba hiyo halali kabisa kutoka RITA, mfumo wa HESLB unatoa ujumbe kwamba "Details not found" yaani taarifa hazionekani. Hali hii imekuwa kikwazo kikubwa sana kwa maombi ya mkopo, na wakati mwingine huleta hofu ya kufutwa kwa maombi au kutopata kabisa mkopo.
Nimejaribu kupiga simu RITA hawapokei kabisa. Nimejaribu HESLB – bado hawapokei. Nikaamua kwenda moja kwa moja kwenye ofisi za HESLB Zanzibar nilichokutana nacho ni majibu mepesi kama "piga tena RITA", "ni shida ya mfumo", "subiri kidogo", bila suluhisho la maana. Wengine wakasema ni tatizo la watu wote. Swali ni moja tu: Iwapo hili ni tatizo la wote, kwa nini hakuna taarifa rasmi wala msaada wa dharura unaotolewa kwa wananchi wanaoumia kimya kimya?
Maisha nyumbani ni magumu. Huyu dogo anahitaji msaada wa kusoma. Serikali imetangaza kuwa elimu ya juu ni kwa wote lakini kwa hali kama hii, watoto wa maskini wanazuiliwa kwa njia ya mifumo isiyosoma au isiyojali. Mifumo inakataa taarifa ambazo tayari zimehakikiwa na taasisi ya serikali yenyewe (RITA). Sasa mwananchi afanye nini?
Ni matumaini yangu kuwa ujumbe huu utawafikia wale wenye dhamana ya kweli kwa wananchi, si kwa maneno bali kwa vitendo. Tunahitaji msaada. Tunahitaji uwajibikaji. Tunahitaji mifumo inayofanya kazi.
Tunaumia kimya kimya lakini ukweli huu hauwezi kufichika milele.