Mfumo wa huduma za fedha kikwazo katika kuwekeza mawazo mapya ya Kiuchumi nchini

Mfumo wa huduma za fedha kikwazo katika kuwekeza mawazo mapya ya Kiuchumi nchini

Hypasonic

Member
Joined
Aug 8, 2014
Posts
14
Reaction score
6
Ndugu wana jamvi....Nawasalimu!!!
Nimekuwa mfuatiliaji wa mada nyingi sana katika uwanja huu na kuvutiwa kwa mada kadha wa kadha..nikaona ni vyema nami niwe mmoja wenu. kama mtanzania kijana, niliyepata kuhangaikia maisha, kusoma, kuajiliwa na baadae kukana kuajiliwa napenda kuwashirikisha jambo hili la upatikanaji wa fedha kwa vijana/wananchi wenye mawazo mapya ya kufufua uchumi wa nchi yetu...mimi ni mmoja wa wenye hamu ya kuinua uchumi wa nchi yetu kwa kuwekeza mawazo yangu binafsi kwa upana wa uelewa na utafiti juu ya mawazo hayo.

Benki za hapa nchini zipo katika mitazamo miwili, yaani benki zinazofanya biashara ya fedha na benki zinazotoa huduma ya mitaji (corporate bank, investment bank). Kwa wazo jipya la biashara ama huduma nyingine toka kwa mwananchi asiye na chochote kama biashara ama, dhamana hatambuliwi na mfumo wa kifedha kwa aina zote mbili za benki.

kwa vijana wenzangu wote..ni muhimu ni kushirikisha mawazo kama kwenye jamvi hili, jambo moja unalotakiwa kujua ni kwamba lugha ya uanzishaji mradi na mawzo mapya si lahisi kueleweka na kila mtu hivyo ni vyema ukajua nani unaweza mshirikisha mkawa mnazungumza lugha zinazofanana.

Mfano: mwenzenu nimeefanya tafiti nyingi (hasa katika eneo nililofanyia kazi vyema na kwa muda mrefu la uendelezaji rasilimali watu katika sekta ya afya) lakini elimu yangu ni mchanganyiko iliyojikita katika masuala ya baishara kwa ujumla. Mwezi wa pili mpaka mwezi wa nne 2013, nilikua nafanya analysis ya upatikanaji na utoaji wa huduma muhimu katika vyuo vya elimu ya juu jijini Mbeya. Baada ya kupata ushirikiano mzuri na taasisi mbalimbali nikaandaa. Nikiwa nakusanya taarifa mbalimbali nikakutana na wazee maofisa mifugo jijini pale na katika mazungumzo ya nini ninachokifanya wakaniambia habari moja juu ya mpango uliokuwepo wa uboreshaji huduma ya uuzajwi vitoweo na jinsi mpango huu ulivyogonga mwamba kwani sehemu kubwa ya kilichokuwa kimepangwa kufanyika kimetoweka. tatizo kwa jiji sasa ni upatikanaji wa mifaa vya mabucha vya kutunzia na kukatia pamoja na vifaa vyote muhimu vya bucha za kisasa kama mpango huo unavyopendekezwa. uongozi wa wamiliki wa mabucha wamekubali kufanya mabadiliko yanayohitajika na mamlaka husika, lakini wameiomba ofisi ya jiji iwasaidie upatikanaji wa vifaa hivyo. jiji wameshindwa kuwalink wafanyabiashara wa nyama na kampuni au taasisi inayoweza kutoa huduma hiyo. Taarifa hizo zikanifikia kwa nusu furha nusu maswali mengi, hatimaye nikaamua kufanya utafiti mdgo nikijiuliza kama niko tayari kuwekeza katika enero hilo je nini nitahitaji na namna gani nitawekeza, na faida yake ni nini. Baada ya utafiti wangu nikapata majibu ambayo sikuwaza hata siku moja, kwamba huo ni mradi mzuri wenye kipato ambacho sikukitegemea, nikaandaa plani ya mradi, nikatengeneza fomu maalumu za usambazaji mradi, nikapeleka ofisi husika jijini, nikazungumza na uongozi wa maduka ya nyama jijini tukakubaliana mpaka taratibu za upatikanaji wa vifaa hivyo, bei zake, teknolojia rafiki, nikasambaza fomu nikihitaji kadirio la chini la maduka 150,kuanza mradi, nikawapata na wengi wakihitaji sana.
Tokea mwaka jana mwezi wa sita nimetafuta funds katika mabenki aina zote mbili nimekosa, ambapo mimi nilihitaji hata tajiri mmoja alipie vile vifaa kule afrika kusini, mimi na kampuni yangu nibaki na usambazaji, masoko na ukusanyaji fedha...... Siamini nimeshindwa kuifanya biashara ile, miradi yangu mingine ni mikubwa lakini ule ulikuwa straight forward na ungefanikisha fedha za miradi yangu mingine yote.....
Hapa nilipo sasa nipo mapumziko ya akili kidogo maana siielewi nchi yangu kabisa...

Mwenye kupenda kushirikishana mawazo na jitihada za kujikwamua kiuchumi kwa vijana wengi na taifa zima...unakaribishwa....
Asanteni
 
Naona watu hawajakuelewa nafikiri ni kwasababu watanzania tunaasili ya kupenda kufanya biashara tulizozizoea yan kama vile kuchukua biashara china,dubai etc concept ikiwa mpya wstu hawapendi kabisa wanadubiria copy and paste kwani hivyo vifaa vitagharimu kiasi gani mkuu?
 
Naona watu hawajakuelewa nafikiri ni kwasababu watanzania tunaasili ya kupenda kufanya biashara tulizozizoea yan kama vile kuchukua biashara china,dubai etc concept ikiwa mpya wstu hawapendi kabisa wanadubiria copy and paste kwani hivyo vifaa vitagharimu kiasi gani mkuu?

unachosema ni kweli hapa weng wakaririshwa biashara, sio hapa tu n karibia watu wote wale wenye akili ya kijasiliamali ndo hufanikiwa. nakumbuka nilipomaliza nilikataa kutafuta kazi kabisa na sikuwa na hata na mtaji wa kuanzia lakin miaka mitatu baadae ndo nimeweza kupata hata kianzio lakin nilistik kwenye wazo lang. mimi nilichokuwa nafanya nilikuwa natembelea mashamban naongea na wakulima wa mazao mfano labda vitunguu mbeya. kipindi hicho unakuta mttu labda kiplot cha robo eka anauza laki mbili na mimi kwa hesab zang labada ninapata gunia kama 6. nilikuwa naenda naongea na kina mama wale wanauza barabaran kuwa nina vitunguu na kwa gunia kipindi kama hiki kama mwaka jana niliuza elfu 70 gunia at the end of the day capital niliweza pata kaka hamna kitu ambacho nachukia kama benk za kitanzania miaka miwili nyuma hawa hawa access niliwafuta wanipe wakanitosa this time nina kijibanda changu ndo hao wanajifanya kujileta. benk zet hazina misaada yoyote ila ni wanyonyaji tu
 
Back
Top Bottom