Nyamtajanyalwa
Member
- Jan 31, 2021
- 15
- 10
Tanzania ni nchi inayotambulika kama nchi ambayo inafuata misingi ya kidemokrasia africa na duniani,ni jambo la kupongezwa na kuendelezwa pia kulindwa vizazi na vizazi
Uongozi na viongozi wamekuwa wakipatikana kwa njia ya kuchaguliwa na kuteuliwa, suala la kuchaguliwa halina mashaka wala shida japo zipo dosari mbalimbali ambazo vyama shindani hasa upinzani wakiwa wanazilalamikia, ikiwemo katiba mpya pia tume ya uchaguzi.
Leo ninataka kujikita zaidi katika kujadili upande huu wa viongozi wanaopatikana kwa njia ya teuzi, kwanza ni jambo ambalo linasikitisha kuona ni idadi kubwa sana ya viongozi ambao ni wqzee wakiteuliwa tena kwa kujirudia rudia, pia hakuna uwazi ni vigezo vipi ambavyo mtu unapaswa kuwa navyo ili uweze kuteuliwa.
pia kuna idadi kubwa sana ya vijana wenye uwezo na elimu kubwa ya kuongoza ama kuwa viongozi na wapo mtaani hawana kazi yoyote wakati huo wakiwa wamesoma kwa fedha za serikali.
Kitu kingine ni hali ya viongozi kuteuliwa kwa kujirudia na wakati mwingne unakuta anateuliwa kiongozi ambae awamu iliyopita aliachishwa kazi kwa maslahi ya umma, inakosekana link au muunganiko wa viongozi wateuaji kuhusu nani wa kumteua na nani si wa kumteua.
Pia vijana wengi wanatamani hizo nafasi zigeuzwe kuwa za kitaaluma na sio kisiasa, ili kuwe na utaalamu katika utekelezaji wa majukumu,ikifuatiwa kuonekana kwa baadhi ya viongozi wateuliwa wakifanya vibaya katika kuongoza kwao ama wanaenda kinyume na utaalamu wa nafasi aliyoteuliwa nayo.
Uwepo utaratibu wa kustaafu katika nafasi hizi za uongozi wa kuteuliwa pia iwepo sheria kama iliyopo katika utumishi wa umma kuwa mtumishi akifukuzwa ama kuachishwa kazi kwa kosa kubwa hapaswi na hawezi kurudi katika utumishi wa umma vivyo hivyo iwe kwa viongozi hawa wa kuteuliwa,kwa maana wengne huachishwa kazi kutokana na ubadhirifu wa mali za umma ama uharifu dhidi ya raia lakini baada ya muda viongozi hao hurejea tena katika nafasi zilezile ama zingine za uongozi ,bila kuonekana kama walifanya ama hawakufanya yale makosa walotuhumiwa nayo .
✍️Hii ndio Tanzania tuitakayo🙏

Upvote
2