KERO Mfumo wa malipo ya ardhi online haufanyi kazi wiki sasa hatuwezi kulipia kodi ya mwaka ya umiliki ardhi

KERO Mfumo wa malipo ya ardhi online haufanyi kazi wiki sasa hatuwezi kulipia kodi ya mwaka ya umiliki ardhi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
4,274
Reaction score
9,326
Kwako Mheshimiwa waziri wa ardhi na makazi mfumo wa wizara yako unaopatikana kwa njia ya mtandao HAUKO SAWA ndiyo maana tumeshindwa kupata control number kwa ajili ya kulipia malipo ya umiliki wa ardhi ya kila mwaka.

Hati ya Umiliki ardhi ninayo nahitaji kufanya malipo, Naomba uingilie kati suala tuweze kufanya malipo stahiki kwa wakati na kuepuka adhabu ya faini isiyo na ulazima wowote.

Kuna watu wanashauriwa waende manispaa husika kama Kinondoni lakini sio wote wapo Dar es Salaam hivyo tunaomba suluhisho linalofaa kwa wamiliki ardhi popote walipo nchni Tanzania Naomba kuwasilisha
 
Ni kero, hati yenyewe niliipata kwa tabu, mara mtandao unaambiwa upo low njoo kesho. Hii ni pale ofisi za wizara kivukoni. sasa Mwaka umepita hata kulipia hakuna control namba mpaka uende ukaiombe pale! kwa nini mtandao ofisi za serikali unakuwa slow??
 
Idara na Wizara ya Ardhi ni janga la Taifa

Huduma mbovu, utapeli, rushwa, ufisadi ndio wanachoweza kwa ufanisi

Nchi ilipaswa yote iwe imepimwa na wamiliki kupewa hati zao na kuongeza mapato ya kodi ya ardhi
 
Hii bado naona ni kero kubwa . Inakuwaje mtu unataka kulipa kodi lakini inashindikana kwa sababu tu ya mfumo. Wahusika wachukue hatua. Kwa sasa, hii inahusu zaidi Hati za mfumo mpya kwa mkoa wa Dar es salaam - ukitaka ku-search kwa hati - mara inasema HUDAIWI, mara Taarifa hazipo ... ni SHIDA sana !!! Mifumo yote - kupitia website na hata e-Ardhi. Nilijaribu kwenda kwenye Halmashauri husika, wakaniambia niende Ofisi za Mkoa/Wizara.
 
Back
Top Bottom