Mfumo wa mashitaka wa Marekani ni wa ajabu sana, kosa moja dogo unaweza kusomewa mashitaka 20

Mfumo wa mashitaka wa Marekani ni wa ajabu sana, kosa moja dogo unaweza kusomewa mashitaka 20

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
5,082
Reaction score
20,806
Sijajua kama ni Marekani peke yake ama kuna nchi nyingine zina mfumo wa mashitaka wa ajabu namna hii. Kwakuwa Marekani mambo yao mengi yako wazi inakua ni rahisi kujua.

Kosa moja dogo kwa Marekani unaweza kusomewa mashitaka 20. Kwa mfano, hapa kwetu ukiua mtu, utasomewa tu shitaka la kuua lakini kwa Marekani hayo mashitaka yake utazimia mwenyewe.

Ukiua mtu kwa mfano na bunduki, risasi, utasomewa kuua, kumiliki bunduki, kumiliki risasi, kufyatua risasi, kula njama ya kuua, kama umeenda pale kwa gari, utashitakiwa kuendesha gari kwenda kuua, kama risasi ulifyatua ukiwa kwenye gari utashitakiwa kufyatua risasi kwenye gari, kutokusubiri ukamatwe na polisi baada ya kutenda kosa, kukimbia polisi, kutoroka eneo la tukio, kutoroka kuwekwa kizuizini, kama ulifatua risasi kwenye nyumba ama jengo utaongezewa kosa kunyatua risasi kwenye jengo, kama kuna shule hapo jirani ama utawekewa kosa kufyatua risasi karibu na shule, kuhatarisha maisha ya wapita njia, kuleta taharuki kwenye jamii, uzembe kufyatua risasi mbele ya watoto wa shule nk nk, kosa moja linazaa makosa 20.

Mbaya zaidi wao kosa moja lina kifungo kirefu, kosa dogo tu linakutupa jela miaka.

Mimi naona huu mfumo ni mbovu, kosa moja linazaa makosa 20.
 
Kule Jela na magereza ni biashara nzuri..
Hata hivyo kwa watu wa Judicial System hiki si kigeni..kipo sehemu nyingitu,hats hapa kwetu.
 
Hata South Africa wana mfumo mbovu wa makosa. Mtu akifanya kosa anawekewa mashitaka kibao ila akifanya kazi mshahara uleule na marupurupu kiasi kidogo tu. Mbona hawalipi kufanya kazi, kuondoa uwezekano wa kuwa ombaomba, kusaidia mzunguko wa fedha, kutumikia serikali/private sector, kulinda thamani ya fedha, kutatua matatizo ya jamii.

Nchi nyingjne ubakaji ni mpana sana, mtu aliolewa miaka mitano iliyopita ila wakaachana ex wake akienda kugombea anakuja mbele ya vyombo vya habari kuwa alikuwa anabakwa nae. Uko UK ndio wanaume wananyanyaswa
 
Io ni kila sehemu dunian mfano ukiiba utafunguliwa kesi ya kuiba .kutumia silaha .kuzurumu haki.kuisumbua mahakama .kuisumbua polis .kuleta kashikash .kupotezea watu mda nk
 
kwa mfano Kesi ipi, ungetuwekea reference
kwa mfano Kesi ya Peter Kupaza aliyemuua ndugu yake wa kike Mwivano Mwambashi Kupaza alihukumiwa kwa Kesi moja tu huko Wisconsin USA
 
Hahaha Inaonekana kigwangwala kwa yale mapesa yote aliyochota angekuwa huko kila kuiba shilingi moja ni kosa linalojitegemea mfano kigwangwala alichota buku inamaana kila shilingi moja katika buku ni kosa
 
Wapo sahihi. Hata huku ukiamua kuyaweka inawezekana, sema kauvivu kakiniingia nakuandikia makosa mawili tu au moja
 
Hata hapa kwetu yapo hayo, tatizo ni PPs wenyewe katika uaandaaji wa charge sheet hufanya 'kibabaishaji' sana.
 
Back
Top Bottom